Nina 'supp', naweza kuajiriwa?

Nina 'supp', naweza kuajiriwa?

Asalam wakuu!

Nimemaliza chuo mwaka jana na nimesomea degree ya ualimu chuo kikuu cha UDOM tatizo langu ni kwamba nimeshikwa kozi moja ambayo natakiwa niirudie kuisoma semister ya pili pamoja na hawa mwaka wa tatu, kuhusu fomu zakuchagua halmashauri/wilaya za kwenda kufanyia kazi tulishajaza tangu mwaka jana, swali langu ni je kuna uwezekano wa kutochaguliwa mwaka huu kwa sababu a hicho "kimeo" changu?

Mwenye uzoefu na hii naomba anijuze.
Kuna tofauti kati ya "Sup" na "carry" ....kimeo chako ni carry forward ndio maana unarudia somo upya.........umemaliza chuo lakini hujahitimu !!!!!!!!!
 
Ajira uanweza kupata isipokua hapo Kwenye Salary ndo HUPATI
 
Utaajiriwa mkuu ila kaza msuli ukitoe usije ukang'ang'aniwa
 
Kwa maelezo hayo wewe bado haujagraduate na ikitokea bahati ukapangiwa ajira siku ukiripoti wakatazama vyeti vyako watakurudisha. Wasipogundua (overlook) na wakajikuta taarifa zako wamescan na kuzituma utumishi HQ basi hautapata mshahara kwani mfumo hautakubali
 
Ajira uanweza kupata isipokua hapo Kwenye Salary ndo HUPATI
Mkuu usimtishe hiyo salary ataipata sana ila awe private serikalini wanahitaji chetu na hawezi kupewa cheti kama hajachomoa kimeo chake
 
pole sana mkuu...nadhani hicho kimeo ni cha yule mama wa ile course ya masterpiece
 
kama matokeo yako ya semester 5 yalikuwa poa ajira inakuhusu but huko uendako ndo unaweza kukutana na mziki
 
Zamani ulikuwa unaajiriwa Siku hizi wanazingua....mi nilicary coz mwaka Jana walinizingua mbaya
 
Ajira mara nyingi wanafundisha ila ukiwa unafundisha tuition awazingui kiiivo
 
Back
Top Bottom