Nina milioni 5 nataka ninunue IST niifanye Uber

Hali kwasasa changamoto kidogo sasa nina kihela changu kama milioni 5 hivi sijui ninunue ist nifanye uber niendeshe mwenyewe sijui itanilipa
Tafuta wataalam wa green house wakufundishe kulima nyanya kwenye huo mjengo, Kwanza kabisa uwaeleze una huo mtaji hivyo wakupe mchanganuo wote wa gharama ya huo mjengo na gharama zingine za kama mbegu, drip pipes, water tanks, na vinginevyo, kwa sababu hela inaweza isitoshe Kuna wataalamu huwa wanauza green house na pia kukufundisha hadi zao likomae ibakie kwako tu kuamua unataka kuuza lini zao lako maana likiwa hata limeiva na lipo kwenye huo mjengo lina uwezo wa kukaa hadi miezi kadhaa bila kuharibika huku ukisubiria bei ya nyanya sokoni ipande madalali waanze kukumezea mate huku udende ukiwatoka

Hiyo biashara itakufanya utulie nyumbani ukiwa bizy na kilimo chako ambacho ni kidogo na cha kisasa na chenye faida kubwa huku ukiwa umekwepa msala wa kukimbizana na Uba ambayo itakufanya urudi na hela ya kula tu ya maendeleo haipo.

Cha msingi poteza mwezi mzima, ukitembelea wenye green house ulizia changamoto za hiyo biashara na faida ukiona inakufaa chukua hatua.
 
Kwanza naanza KWA kukupongeza HONGERA SANA

umewaza wazo zuri Sana kununua gari ni bora na kufanya Uber ama bolt? Na nasikia skuiz unaweza jiunga zote KWA mpgo Ili kutega liziki pande mbili

Uber ni bora kuliko mtaji kuuingiza kwenye biashara za ulanguzi na sio mzoefu na biashara hzo Uber kama gari Yako huwezi shindwa kwenda home hata na 30 elfu net profit na hata kama ikikushda huwezi poteza KILA kitu utabakiwa na gari na unaweza uza tena na kupata chochote

FANYA UBER AMA BOLT USITHUBUTU BIASHARA ZA ULANGUZI.
 
Kwa milioni tano ni ngumu kupata IST ya maana ili ufanye uber, pia biashara ya uber ni ngumu kwa sasa.

Ushauri wangu tu, chukua nusu ya hiyo pesa (2.5m) nunua pikipiki (boxer?) halafu fanyia biashara wewe wenyewe, hiyo hela nyingine weka akiba tu, wakati unapiga miche miche za bodaboda kuna deal za biashara zingine unaweza ukazijua then ukaitumia hiyo pesa iliyobakia kama mtaji. Kwa boda upo uhakika wa kulaza sio chini ya elfu 10 kwa siku.

Ushauri mwingine unaweza ukanunua bajaj used kwa hiyo milioni tano halafu ukapiga mwenyewe hiyo biashara, na kuwa na uhakika wa kulaza sio chini ya elfu 25 kila siku.
 
Kwanza naanza KWA kukupongeza HONGERA SANA

umewaza wazo zuri Sana kununua gari ni bora na kufanya Uber ama bolt? Na nasikia skuiz unaweza jiunga zote KWA mpgo Ili kutega liziki pande mbili

Uber ni bora kuliko mtaji kuuingiza kwenye biashara za ulanguzi na sio mzoefu na biashara hzo Uber kama gari Yako huwezi shindwa kwenda home hata na 30 elfu net profit na hata kama ikikushda huwezi poteza KILA kitu utabakiwa na gari na unaweza uza tena na kupata chochote

FANYA UBER AMA BOLT USITHUBUTU BIASHARA ZA ULANGUZI.
Ushauri mzuri na pia hizo app's unaweza kuanazo na kujisajili zote uber,bolt,Indriver na hadi Taxfy...hukosi 30 - 50 kwa siku lkn kwa milion 5 tafuta Passo ist haitakua nzuri
 
Ushauri mzuri na pia hizo app's unaweza kuanazo na kujisajili zote uber,bolt,Indriver na hadi Taxfy...hukosi 30 - 50 kwa siku lkn kwa milion 5 tafuta Passo ist haitakua nzuri
Vipi kuhusu vits au basi nipambane nipate japo ist niongeze ata ifike 7 au 8m naweza kupata ist mkuu ila madalali sasa ndio shida sana
 
Vipi kuhusu vits au basi nipambane nipate japo ist niongeze ata ifike 7 au 8m naweza kupata ist mkuu ila madalali sasa ndio shida sana
Milion nane uhakika kbs ingia fb kuna matangazo ya magari direct no udalali, vits hakina mvuto hata baadae kuuza ni hasara tu
 
Vipi kuhusu vits au basi nipambane nipate japo ist niongeze ata ifike 7 au 8m naweza kupata ist mkuu ila madalali sasa ndio shida sana

Jinsi unavyo elezea upambane uongezee ifike Million 7 au Million 8 ya kupata IST, ni bora uendeleze hayo mapambano hukohuko maana inaonekana ndo kuna hela, huku kwenye Uber na Bolt utapambana sana kuliko huko mkuu, ni ushauri tu
 
Inamana saizi hizi uber hazilipi??
 
Inamana saizi hizi uber hazilipi??
Yaani kwanini sasa hizi kauli ebu mtuelezee wanashughulika na hii habari uber na bolt nini changamoto mbona now hizi kauli zinakatisha tamaa mimi gari naendesha mwenyewe simpi mtu je bado kuna shida maana shida tulikuwa tunasikia ukimpa dereva
 
Back
Top Bottom