Nina Milioni 45, msaada wanaJF

Huwa nachukia idea ya kununua nyumba iliyojengwa, kwanini usianze yako na ramani yako jinsi unavyopenda,
Ni kweli kuna uzuri wa kujenga mwenyewe hasa nyumba yako ya kuishi sio ya biashara, Lakini kumbuka GHARAMA za kujenga ni almost 2x ya kununua hasa ukivizia wale walio na changamoto za kifedha kama mikopo ya bank, Kununua kunaokoa sana pesa , muda, usumbufu.
 
Asante sana kwa mawazo yako naendelea kujifunza mengi kupitia jukwaa ili japo kuna wengine wananibeza na kuona kama sina akili .Ndugu zangu Tambua sisi binadamu tumezidiana uelewa wa mambo ata mimi ukija katika upande wangu wa kazi basi najua kila kitu mpka nisipokuwepo kazini dhairi ofisi inaona pengo langu pia ndo hivyo hivyo kwa maisha ya mtaani kuna watu wanajua mambo mengi kulingana na sector mtu anayoitegemea kuingizia kipato kwahiyo msinibeze na kuona kama nimekurupuka kuchukua huo mkopo. Ndo maana nimesema kuwa hizi hela sio kama narudisha mkononi hapana nakatwa moja kwa moja kwenye mshahara kwahiyo ata ningefeli au kufanikiwa sio kama benki itanifilisi hapana
Usivunjike moyo na wanaokubeza mkuu, ndo binadamu walivyo, hatufanani
 
Mimi pamoja na mke wangu ni watumishi wa serikali tumekaa pamoja tumeshauliana tumeamua kuchukua mkopo wa mil 45 lakini tatizo tulilonalo hatuna idea yoyote ya biashara maana kazini tunaenda asubuhi na kurudi jioni.

Japo mungu ametujalia tumeweza kujikwamua na kujenga nyumba ya kuishi maeneo ya boko chasimba

Shida yangu kwenu je ni biashara gani naweza kufanya ili tuweze kujipatia kipato cha ziada bila kuaribu utaratibu wa kazi maana ikifika tarehe 14 wote tunakuwa tumeishiwa tunabakia ndani kuangalia CD za kikorea na kijapani.
Mawazo niliyokuwa nayo ni÷

1. Ninunue daladala ya habiria
2. Ninunue bodaboda 5
3. Ninunue bajaji mbili
4. Nifuge kuku wa nyama

Maana siwezi kuweka fixed account kwakuwa pesa yenyew ni ya mkopo ushauri wenu ndugu zangu lakini wazo la daladala ndo tumelipa kipau mbele kikubwa naomba kwa mwenyewe uzoefu na iyo biashara ya daladala anipe msaada kwa umakini maana makato ya miaka 5 sio powa kabisa
Katoe sadaka, fungu la kumi, limbuko then utabarikiwa zaidi
 
Nasikitika kufahamu kuwa kuna mtu anaweza akachukua mkopo tena wa 45 million bila na plan yoyote ya kufanyia huo mkopo.

It sounds strange
Kuna mimi pia nasikitika kuona mtu ana milioni 45,tunashindwa kumpa wazo la biashara kwa sentensi kadhaa,suppose asingesema katoa wapi hizo hela😃.Tungemjibu nini?
 
Usijichanganye hata kidogo kununua daladala....utalia.
Ukinunua daladala basi we uwe konda mpk pale utakapoona pesa yako atleast imerudi.
Zingatia nnayokwambia, yalishanikuta.
Ulishawahi kufanya biashara ya daladala? Kama jibu ni ndiyo tuambie ulikwama wapi. ?
 
Haya maisha nilikataa kabisa
Atleast mmoja wenu angekuwa hivi ila sio wote
Anyway am sorry kuwa too emotional kwenye maisha yenu
Atleast wanashirikiana na kujadiliana vizuri,watafika tu.
Tatizo ni moja humu watu wengi,SIO WOTE, hawana hiyo fani na uzoefu wa biashara
 
Nilitaka nisome comments nicheke wee alafu niende kwenye uzi mwingine. Tayari nimecheka ila nimekuonea huruma kwa sababu mzazi wangu aliwahi kupitia hali kama yako na kiukweli ilikuwa kipindi kigumu kwake.

Mimi nafanya biashara. Nimewahi kujaribu biashara 17. Biashara tatu tu ndio zimeingiza faida. Na ni biashara moja tu katika hizo tatu zimeniletea mafanikio makubwa. Katika safari hii nimegundua kitu kimoja. Unatafuta biashara kwanza ndio ufikirie pesa ya kuifanya na sio kupata pesa kwanza kisha ndio uamue biashara.

Nakushauri kaa chini wewe na mkeo na fanyeni tathmini ya nini nguvu zenu. Mna ujuzi gani ambao mnadhani utakuwa wa manufaa kwa watu wengine? Au mnajuana na nani ambae ana ujuzi unaoweza kusaidia watu wengine? Kuna kitu ambacho nyinyi wenyewe kinawasumbua na hamjapata suluhisho? Kuna kitu ambacho watu wanakusifia wewe au mke wako mnajua au mmebarikiwa?

Nasema hivi kwa sababu kuna biashara aina mbili kuu. Kuna hizi za trading ambazo zimezoeleka mfano mayai, kilimo na pia kuna biashara za huduma ambazo ni kama kuosha magari na watu kama tax consultant. Katika kufikiria nguvu zenu na ujuzi wenu fikirieni jinsi mnaweza kutumia katika huu upande wa huduma kwa kuwa mtaji unaohitajika huwa si mwingi ukilinganisha na upande wa pili ya bidhaa za kushikika. Pia faida huwa kubwa zaidi.

Kama haujui mifano ya biashara hizi za huduma, unaweza kugoogle 'service and knowledge businesses to start' kupata mifano.

Mfano mimi nilikuwa na biashara ya kufundisha wanafunzi wa A level kufaulu mitihani ya kuingia vyuo vya Marekani na Uingereza. Nilianzishaje? Baada ya kuambiwa kipindi niko shule kuwa ninajua kuelezea somo likaeleweka. Biashara ile ilikuja kuajiri hadi watu 5 kabla ya mimi kubidi kumuachia partner wangu ili nikuze biashara nyingine.

Ni ngumu sana kufanya tathmini ya undani na ukashindwa kugundua chochote katika maswali niliyokuwekea awali. Ila kama hilo la kwanza likishindikana fikiria ni nani unamjua ana jambo la kusaidia watu wengine ili pamoja muweze kuanzisha biashara.

Ni vizuri ukiamua kufanya partnership na mtu ikajulikana mapema kabisa yupi anapata lipi. Na ni vizuri ikawa mtu ambae ulishamuamini na jukumu kubwa kabla ya kuanza nae biashara. Sio jambo jema kufanya kazi na mtu ambae haujawahi kumuamini katika jukumu lingine au hauna historia yake ya jinsi alivyofanya kazi na watu wengine kabla yako. Na hapa bado nashauri kuangalia jinsi ya kufanya biashara ya huduma.

Mfano katika biashara yangu moja nina mfanyakazi ambae anapenda sana urembo. Nilipoona hili nikamuambia tuanzishe biashara ya urembo wa asili kutumia bidhaa kama aloevera na zinginezo kutatua matatizo ya ngozi. Jukumu lake ni kuandaa masomo katika mitandao ya kijamii kuvutia wateja na jukumu langu ni kutengeza mifumo itayohakikisha wateja wananunua. Mimi nimemuongezea mshahara kiasi kizuri kwa kazi yake na upande wa pili mimi nachukua mzigo wa faida au hasara katika biashara. Kila mmoja ameridhika.

Hivyo ndugu tafuteni jambo ndani yenu ambalo mnaweza kutumia kuanzisha biashara ili mtapoanzisha na kuanza kuona mafanikio, mkopo huo utumike kuikuza. Hii itaepusha kuchoma hela ya mkopo kwa kujaribu hili na lile.
 
Nashukuru sana kwa ushaur wako hakika nimeusoma law makini sana maana nimekuwa njia panda kile nilichotegemea kufanya naona kama kinakuwa na changamoto sana kuliko nilivyofikiria mwanzo
 
Atleast wanashirikiana na kujadiliana vizuri,watafika tu.
Tatizo ni moja humu watu wengi,SIO WOTE, hawana hiyo fani na uzoefu wa biashara
Bora ndugu umeliona ilo kuna watu wanaona kama nimekosea sana hakika kila mmoja anakuwa na uelewa wake katika kuwaza jambo
 
Ni kweli kuna uzuri wa kujenga mwenyewe hasa nyumba yako ya kuishi sio ya biashara, Lakini kumbuka GHARAMA za kujenga ni almost 2x ya kununua hasa ukivizia wale walio na changamoto za kifedha kama mikopo ya bank, Kununua kunaokoa sana pesa , muda, usumbufu.
Gharama ya kununua nyumba kwa mtu ndiyo inazidi hata ile ya kujenga, maana hakuna kitu kinaingiza gharama kama ku repair, nina uzoefu huo, jenga nyumba yako utafurahi mwenyewe, lakini sio kununua iliyojengwa
 
Kuna mimi pia nasikitika kuona mtu ana milioni 45,tunashindwa kumpa wazo la biashara kwa sentensi kadhaa,suppose asingesema katoa wapi hizo hela😃.Tungemjibu nini?
Mtu anachukuaje mkopo mkubwa hivyo bila kuwa na plan ya kufanya?

Anyway let's say anazipata kwa njia nyingine ni ngumu kumshauri mtu kwa hela zote hizo bila kuwa engaged professionally mkuu
 
jar
Mimi pamoja na mke wangu ni watumishi wa serikali tumekaa pamoja tumeshauliana tumeamua kuchukua mkopo wa mil 45 lakini tatizo tulilonalo hatuna idea yoyote ya biashara maana kazini tunaenda asubuhi na kurudi jioni.

Japo mungu ametujalia tumeweza kujikwamua na kujenga nyumba ya kuishi maeneo ya boko chasimba

Shida yangu kwenu je ni biashara gani naweza kufanya ili tuweze kujipatia kipato cha ziada bila kuaribu utaratibu wa kazi maana ikifika tarehe 14 wote tunakuwa tumeishiwa tunabakia ndani kuangalia CD za kikorea na kijapani.
Mawazo niliyokuwa nayo ni÷

1. Ninunue daladala ya habiria
2. Ninunue bodaboda 5
3. Ninunue bajaji mbili
4. Nifuge kuku wa nyama

Maana siwezi kuweka fixed account kwakuwa pesa yenyew ni ya mkopo ushauri wenu ndugu zangu lakini wazo la daladala ndo tumelipa kipau mbele kikubwa naomba kwa mwenyewe uzoefu na iyo biashara ya daladala anipe msaada kwa umakini maana makato ya miaka 5 sio powa kabisa
TAFUTA ENEO LENYE MAGEREJI JARIBU BIASHARA YA SPEA ZA MAGARI INALIPA SANA.
ILA USIANZE FULL BLAST ANZA MDOGO MDOGO KWANZA NA VITU KAMA ENGINE OILS, DIESEL /OIL FILTERS, MABUSHI, CHANGING TYRES, HALAFU KIDOGO KIDOGO UNAINGIA KWENYE PARTS
 
Humu mtoa mada km hunaisbia kuvurugwa basi kuna wazo utalichukua litakalokuingiza chaka..

Mm binafsi nilichoona ni kuwa mtoa mada kuna kitu ww binafsi unakipenda zaidi ila humu umekuja kujaribu kuona je atu watakisapoti au la au pengine umetaka upate wazo la ziada ulishindanishe na hilo lako ili ufanye maamuzi,Wazo lenyewe ni hilo la KUNUNUA DALADALA uipigishe kazi..

Sio mbaya itakujengea heshima mtaani nawe utaonekana bosi ila binafsi mm sikushauri hiyo biashara km unaweza fanya mchakato wa kufika mikoani hasa ile inayozalisha mpunga kwa wingi kata hata M30 nunua mpunga naamini hutokosa gunia around 500 weka stoo subiria muda ambao bei itakuwa imepanda ukiona kuna ongezeko la faida ya sh 30 elfu kwa kila gunia unaamua kuuza.Amini biashara hiyo haiwezi kukupotezea hela yako kwa namna yoyote ile na faida ni given.

Hiyo 15M inayobaki unaweza kutafuta wateja wa nafaka ukawa unazungushia biashara km ni mchele,mahindi au kinginecho huku gunia zako 500 zimetulia stoo.

Kila la heri.
 
... standard formula ambayo wanaitumia wafanyakazi wengi sana wa serikali.
Ambayo wengi inawaumiza na kuwaangamiza kiuchumi.

Work hard+save+borrow+pay excessive taxes...

...tafuta wataalamu wa mambo ya investment wakushaur nn cha kufanya unless utalizwa kuwaamini ndugu na marafiki.
 
Back
Top Bottom