Nina Milioni 45, msaada wanaJF

kisumapai

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
544
219
Mimi pamoja na mke wangu ni watumishi wa serikali tumekaa pamoja tumeshauliana tumeamua kuchukua mkopo wa mil 45 lakini tatizo tulilonalo hatuna idea yoyote ya biashara maana kazini tunaenda asubuhi na kurudi jioni.

Japo mungu ametujalia tumeweza kujikwamua na kujenga nyumba ya kuishi maeneo ya boko chasimba

Shida yangu kwenu je ni biashara gani naweza kufanya ili tuweze kujipatia kipato cha ziada bila kuaribu utaratibu wa kazi maana ikifika tarehe 14 wote tunakuwa tumeishiwa tunabakia ndani kuangalia CD za kikorea na kijapani.
Mawazo niliyokuwa nayo ni÷

1. Ninunue daladala ya habiria
2. Ninunue bodaboda 5
3. Ninunue bajaji mbili
4. Nifuge kuku wa nyama

Maana siwezi kuweka fixed account kwakuwa pesa yenyew ni ya mkopo ushauri wenu ndugu zangu lakini wazo la daladala ndo tumelipa kipau mbele kikubwa naomba kwa mwenyewe uzoefu na iyo biashara ya daladala anipe msaada kwa umakini maana makato ya miaka 5 sio powa kabisa
 
Sio uchawi, lakini naona ukienda kuanguka.
Mmechukua mkopo bila kuwa na plan.
Halafu ni risk sana kuanzisha biashara kwa kuutegemea mkopo 100℅

Mna uzoefu na biashara gani?
Kwa usalama wa hiyo pesa kama una kiwanja ni heri ujengee nyumba upangishe.

Neno langu si sheria. Zaidi labda wataalamu waje
 
Fuga kuku
WA nyama
Na kuku wa kienyeji..


Ila unaweza Jenga nyumba na ukauza ni sure bussines kipindi hujaiuza unapangisha
Tatizo ninapoishi nina eneo dogo sana kwahiyo naona kama ntaingia Gharama kubwa kununua eneo lingine ndugu .na pia swala la kujenga nyumba ni ngumu maana sina eneo ntakuta naishia katikati na hela ya kumalizia itanishinda hivyo itabidi nisubilie baada ya miaka mitano nimalize mkopo ndo nikope tena kumalizia nyumba
 
Ntakutumia link za dala dala uchague moja!
Bajaj, utalia, boda boda, utaomboleza...Kuku, sikushauri.. Ndugu yangu wa karibu anafuga.. Inabidi uwe na uzoefu kabla hujazamisha pesa ndefu.
Dala dala ikija, katia bima kubwa.
Used 1998 NISSAN CIVILIAN BUS/KC-RYW40 for Sale BH241062 - BE FORWARD
Utakuwa umenisaidia sana ndugu maana naona Giza mbele yangu mpka nawaza nimchukue kijana kijijin nimpeleke NIT fasta apige kozi ya miezi 4 nimuingize barabarani apambane maana madereva wa DSM kidogo wanahitaji mtu ambae ni mzoefu kwenye biashara maana sisi tunaotaka kuanza inakuwa changamoto kwelikweli
 
Tatizo ninapoishi nina eneo dogo sana kwahiyo naona kama ntaingia Gharama kubwa kununua eneo lingine ndugu .na pia swala la kujenga nyumba ni ngumu maana sina eneo ntakuta naishia katikati na hela ya kumalizia itanishinda hivyo itabidi nisubilie baada ya miaka mitano nimalize mkopo ndo nikope tena kumalizia nyumba
Milioni 45 ushindwe kujenga na kumaliza?

Unaweza nunua hata pagala kuna mapagala unanunua 20 unatumia million 10 kumalizia..

Naona wewe ulivyojenga mwanzo ulipigwa Sana na mafundi..
 
Formula ya daladala ikiharibika tengeneza mwenyewe
na services pia fanya mwenyewe
 
Sio uchawi, lakini naona ukienda kuanguka.
Mmechukua mkopo bila kuwa na plan.
Halafu ni risk sana kuanzisha biashara kwa kuutegemea mkopo 100℅

Mna uzoefu na biashara gani?
Kwa usalama wa hiyo pesa kama una kiwanja ni heri ujengee nyumba upangishe.

Neno langu si sheria. Zaidi labda wataalamu waje
Ndugu sisi watumishi wa serikali maisha yetu asilimia kubwa tunategemea Mikopo maana ukisema ujichange uje kupata 45 mil karibia miaka kumi na marejesho yetu sio cash in hands Bali wanakata moja kwa moja kwenye payslip kwahiyo ni swala la kawaida na ndo maisha yetu ndugu
 
Usijichanganye hata kidogo kununua daladala....utalia.
Ukinunua daladala basi we uwe konda mpk pale utakapoona pesa yako atleast imerudi.
Zingatia nnayokwambia, yalishanikuta.
Je nifanye nini ndugu maana na hela nshaichukua
 
Usijichanganye hata kidogo kununua daladala....utalia.
Ukinunua daladala basi we uwe konda mpk pale utakapoona pesa yako atleast imerudi.
Zingatia nnayokwambia, yalishanikuta.

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
Ukitaka dala dala ikulize, upate gari mbovu au nzee, uwe na bima ndogo, upate ruti mbaya au dereva mbaya.. Uwe mvivu kutengeneza gari au uwe unakomaa sana kuwa lazima kipande litimie.
 
Vyovyote unavyochagua Biashara ya kuifanya hakikisha inasifa hizi.

1)Sustainable; ikufadishe mpaka unazeeka na kufa.

2)Profitable; kwa Mtaji uwo faida isipungue 80,000 Tzs minimum na hapo kwasabu husimamii mwenyewe 100℅.

3)Managable; inajiendesha bila wewe kuhusika (kwasababu wewe sio enterprener).

Hizo idea zako zote hazi-feet humu.



Be forward inaingiza magari sichini ya 50 kwasiku Tzs especially DSM miaka 20 mbele gari itakuwa kawaida kumili na Network ya balabala inapanuliwa unashindwa kupata wazo lenye Sustainability hapa.
 
Back
Top Bottom