Nina milioni 45, nifanye biashara ipi kati ya hizi?

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,927
6,417
Wasalamu,kwa kuuza daladala zangu mbili sababu ya usumbufu wa kissing garage,plus mkopo nawezapata kama m45 nipo na mawazo kama matano hivi,ushauri muhimu ili nisiangamie maana pesa ikishapotea hairudi unabaki na majuto na maradhi ya moyo tu.

1. Nitafute eneo nijenge frem za kupangisha hapa takula hadi uzeeni shida utapata kodi itakayokusaidia kula na sio kukua haraka kibiashara lkn ni ya uhakika yaani ufi njaa.Mungu akijalia wawezazifungulia biashara zako kadri utakavyo na maisha yakaenda.

2. Ninunue trekta mpya zero kilometer katu sitonunua chombo cha moto used nchini tena kwa hasara nilizopata za kushinda garage kuliko kushinda barabarani.Trekta ni tegemeo ni johndeer,Massey,case,deutz ukitanguliza 45 anakupa inayobaki na riba ndani ya mwaka kwa mnyama deer miaka miwili yaani,zinauzwa kati ya 55m hadi 65m plus jembe.Niingie pori nikachane mbuga nalimia watu nami nalima yangu mazao tegemeo ni karanga,alizeti,mtama,mhogo,viazi,mahindi,mpunga nategemea kulima ekari 500 kwenda juu mashine Yangu nguvu yangu nasimamia mwenyewe iwe jua au mvua ni kula mbuga tu.

3. Nimpe muhindi 45m anipe tata marcopolo ya mkopo zero kilometa nikae mlangoni nipige ndefu sio daladala yaani ruti za nje ya mji nauli isiyo chini ya elf 15 yaani kupakia kwa foleni mfano moro ifakara,mbagala kusini,kambi popote.

4. Niagize fuso mnyama au scania kipisi nikae mwenyewe naenda shamba kununua mizigo mixer mfano viazi chips,ndizi,miwa,nyanya,vitunguu,ngombe,mbuzi,nk chochote kiuzwacho sokoni nakujauza bei ya jumla narudi shamba tena kwa kusomba mizigo ya duka kurudi shamba.

5. Nifungue kiwanda cha kusaga chupa na mifuko ya plastic kisha nauza viwandani.

6. Ninunue shamba nipande miti niendelee na umasikini wangu nisubirie miaka 10 hadi 15 niwe milionea baada ya kuvuna miti.

Naombeni idea kwa kuangalia risk,faida,mda,usalama wa fedha,uhakika wa kuishi, stress,nk
 
Kwakua una muda katika biashara ya magari nashauri chukua number 4 iyo itakuwa rahisi kwako

•haitasumbuana na dereva hesabu za kila siku
•utatunza mali yako(gari) ambayo ndio mtaji wako
•gari iyo itakusaidia pia kukuza mtaji wako kama utaamua kufanya baadhi ya biashara kaa kutumia gari yako kufata vitu sehemu mbali

Nikutakie kila la kheri ni ayo tu upande wangu
 
Mkuu hongera kwanza. Biashara zote hizo pasua kichwa. Nunua mpunga weka s tore. Mfano mpunga wakati wa kiangazi huwa ni kati ya elf 30 hadi 36 kwa ginia hapo ni july uweke store hado october hadi april then uuzekati ya miezi hiyo bei ya gunia la mpunga hupanda hadi elf 90. Nafikiri faida shilingi itazaa shilingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hongera kwanza. Biashara zote hizo pasua kichwa. Nunua mpunga weka s tore. Mfano mpunga wakati wa kiangazi huwa ni kati ya elf 30 hadi 36 kwa ginia hapo ni july uweke store hado october hadi april then uuzekati ya miezi hiyo bei ya gunia la mpunga hupanda hadi elf 90. Nafikiri faida shilingi itazaa shilingi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo nalo wazo nalowazia pia
 
Mkuu hongera kwanza. Biashara zote hizo pasua kichwa. Nunua mpunga weka s tore. Mfano mpunga wakati wa kiangazi huwa ni kati ya elf 30 hadi 36 kwa ginia hapo ni july uweke store hado october hadi april then uuzekati ya miezi hiyo bei ya gunia la mpunga hupanda hadi elf 90. Nafikiri faida shilingi itazaa shilingi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa si panatakiwa uzoefu kwenye manunuzi ya mpunga nisijeuziwapepe
 
Bana likasi, Hiyo pesa 45m ukiweka benki ya biashara kama fixed deposite kila mwezi unapewa 480,000 riba wakati unasubiria paka pale mazingira ya biashara ikae vizuri nchini, lasivyo uwezekano wa kupoteza mtaji ukiwa unaanza biashara mpya nimkubwa sana kipindi hiki cha JPM, labda kama unaendeleza biashara ulio kua nao....lakini jambo muhimu kipindi hiki sio faida ila ni kulinda mtaji wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo pesa 45m ukiweka benki ya biashara kama fixed deposite kila mwezi unapewa 480,000 riba wakati unasubiria paka pale mazingira ya biashara ikae vizuri nchini, lasivyo uwezekano wa kupoteza mtaji ukiwa unaanza biashara mpya nimkubwa sana kipindi hiki cha JPM, labda kama unaendeleza biashara ulio kua nao....lakini jambo muhimu kipindi hiki sio faida ila ni kulinda mtaji wako

Sent using Jamii Forums mobile app
Bank ipi iko vizuri,niliyokuwa nayo ni nzuri kosa nililofanya ni kununua daladala za kufufua sababu pesa ilikuwepo nimejikuta imeishia garage japo zimesimama lkn pasua kichwa zinakula Pesa kama jini mfilisi unarekebisha hiki kinaibuka hiki naona tafilisika japo wazoefu wanakwambia ndio gari zilivo vumilia zitatulia zikishajivubua magonjwa yote hata sisi tulianza hivo hivo.

Unagusa services ya pump ukicheki imeliwa laki nani hapo nikipiga sawa na mifuko ya cement kadhaa,Mara gari imekamatwa,najikuta natoa tu
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom