Kipilipili
JF-Expert Member
- May 25, 2010
- 2,272
- 1,882
idea 1
nakushauri anzisha biashara ya kukopesha watu, weka riba ya 10% kila mwezi. kuna watu wengi wanataka mikopo midogo midogo hawapati. ila zingatia yafuatayo:
- kopesha mtu baada ya kujiridhisha anaenda kufanyia kitu kitakachozalisha
- mkopaji awe na mdhamini
- mkopaji aweke rehani kitu fulani
idea 2:
kama una eneo la kufugia, fuga kuku wa mayai uone faida zake. mnyumbulisho ni kama ifuatavyo:
- Banda la kuku (tumia vifaa used e,g,. mabati, mbao, wires)= 500,000
- Vifaranga 100 kila kimoja 2300 = 230,000
- Chakula (0.12kg kila siku kwa kuku *180 days kabla kuanza kutaga )/50kg*100kuku xTsh. 33,000 kwa mfuko=1,425,600
- dawa mbalimbali (chanjo, antibiotics, vitamins and minerals)= 70,000
- salary ya mfanyakazi = 50,000* miezi 6 =300,000
- utilities (maji, umeme/mkaa/mafuta ya taa) = 50,000*miezi 6 = 300,000
- mengineyo = 174,400
- Jumla = 3,000,000
mapato
- kuku asilimia 75 watataga kila siku hivyo kuwa na tray 2.5. tray moja kwa dar ni Tsh 5,500. kwa siku utapata 2.5*5,500=13,750 na mwezi inakuwa 412,500/Tsh
- mbolea kwa mwezi unaweza kupata kama 5,000
- jumla ya mapato kwa mwezi 417,500
- matumizi kuku wakiwa wanataga ni nusu ya mapato , hivyo faida kwa mwezi ni 208,750
- faida kwa mwaka ni 208,750*12 = 2.5m
- kumbuka ili kufanya biashara hii zingatia misingi ya ufugaji bora ili kuzuia vifo. pia weka kumbukumbu vizuri kijana asikuibie
- anzisha biashara ya kuuza mazao, unakusanya vijijini na kuja kuuza mjini
- Nunua hisa za precision Air
mkuu umenisaida na mimi,asante sana,hao wengine wanaotoa mawazo hasi,nadhani ni wale wenzetu waliozoea kuuza sura kule FACEBOOK,sasa wanadhani hapa pia tuna utamaduni huo.inahitaji uvumilivu sana kuishi na watu kama hawa