Mkopo kwa ajili ya kuendesha mradi wa ujenzi

Embe Bichi

Member
Feb 1, 2024
87
206
Habari za mchana wanajamvi, mimi ni kujana mwenye miaka 33, katika kujitafuta baada ya mapambano ya muda mrefu ya hapa na pale nimefanikiwa kupata kandarasi ya kutekeleza mradi wa taasisi mojawapo ya serikali. Mradi huo una thamani inayofikia 120M, changamoto inayonikabili kwa sasa ni mtaji wa kuanza utekelezaji wa mradi huo, mradi ni miezi sita. Sina dhamana yoyote ya kuweka ili nipate mkopo angalau 20M ili nianze utekelezaji wake.

Ninaomba msaada katika jukwaa hili, je kuna taasisi yoyote ya fedha inayoweza kunikopesha kiasi hicho cha hela pasipokuwa na dhamana yoyote nikapata fedha kwa ajili ya kuendesha mradi huo?

Kama siwezi kupata mkopo, ni njia gani nitumie kupata support ili niweze kutekeleza mradi huo.

Note: Nina Nyaraka za mkataba halali ambao nimesaini na Client wangu (Gorvernment Institution)
 
Nadhani ungemtafuta mtu wa karbu ambaye anacho kitu Cha kuweka dhamana mf. Nyumba then ukamshirikisha mradi wako akiridhia anaweza kuwa kama mdhamini wko wew kupata mkopo.
 
Nadhani ungemtafuta mtu wa karbu ambaye anacho kitu Cha kuweka dhamana mf. Nyumba then ukamshirikisha mradi wako akiridhia anaweza kuwa kama mdhamini wko wew kupata mkopo.
Siwezi kupata msaada kwenye taasisi yoyote ya kifedha kwa kutumia mkataba nilionao
 
Kaulizie kwaza NMB may be inawezekana
Hili jukwaa ni pana sana, ninaamini wamo humu ndani, wakiweza kujibu au kuelimisha hapa jamvini itakuwa na faida kwa wadau wengine, inawezekana wapo wengine wanachangamoto kama yangu pia wanaweza pata ufafanuzi hapa
 
Naamini ulifanikiwa
 
Back
Top Bottom