Nina milioni 20 nataka kujenga nyumba ya vyumba 3 Dar es Salaam. Naweza fikia hatua gani?

Pia msipende kujibu maswali kiurahisi ili uonekane wewe ni mtu wa maana kwa sababu unampa mtu moyo.
Sometimes mtu inatakiwa aondolewe kutoka fikra fulani kabla ya kuanza project yake.
Kwa mfano, mleta mada ni vizuri akishauriwa kuwa nyumba vyumba vitatu haielezi nini unachohitaji.
Angeleta ramani, au akaelezea size ya vyumba etc...
La sivyo tutakuwa tunajibishana tu, unaweza, huwezi, unaweza, huwezi ... kwa siku kumi. No description.
Hili nalo neno
 
Habari za Mchana wadau

Nashukuru saana kwa michango yenu ambayo imenipa moyo na changamoto pia. Labda niweke wazi kidogo mahitaji ya nyumba ninayotaka kujenga labda naweza kupata mawazo mazuri zaidi yatakayonisaidia.

Kwanza huu ndio ujenzi wangu wa kwanza na sina uzoefu katika masuala ya ujenzi ila nimejaribu kufanya research kwa baadhi ya vitu ambavyo naweza kuanza navyo.

Kiwanja changu kipo sehemu tambarare kabisa na kimezungukwa na majirani ambao wameshajenga. Maji yapo na umeme upo mita 100 tu. Nimeshavuta Maji ya Dawasa katika plot yangu.

FLOOR PLAN YA NYUMBA
Nyumba ni ya vyumba 3 yenye
_ Master Bedroom yenye WIC
_ Vyumba 3 plain
_ Living/Sitting Room
_ Dinning
_ Jiko na Stoo
_ Public Washroom

Kianzio nilichonacho kama nilivosema hapo ni 20mn so nataka walau kupata muelekeo wa wapi naza kufika lakin pia kujua mahitaj muhimu

Mfano
Matofali
Cement
Ni hatua ipo Nondo zitahitajika
Nk
Unazungumzia vyumba 4 vya kulala! Tayari huo mradi ni mkubwa. Ingekuwa vyumba 3 ya kawaida isiyo na mbwembwe, pesa ingetosha 95%. Kwa kupanga, yaani mbao za kenchi unapaka oil. Tiles za Tz. Bati iliyo nafuu no colour. Ramani punguza corridor kuokoa blocks. Milango ya ndani "flush doors" na mengine mengi. Ila usibane cement katika ujenzi wako. Simamia fundi material yote itumike sawa na hakikisha nyumba inanyooka. Wewe uwe pima maji. Nunua Square, kila kona pima.
 
Ni typing Error! Master Bedroom na Vyumba viwili Plain
 
Unazungumzia vyumba 4 vya kulala! Tayari huo mradi ni mkubwa. Ingekuwa vyumba 3 ya kawaida isiyo na mbwembwe, pesa ingetosha 95%. Kwa kupanga, yaani mbao za kenchi unapaka oil. Tiles za Tz. Bati iliyo nafuu no colour. Ramani punguza corridor kuokoa blocks. Milango ya ndani "flush doors" na mengine mengi. Ila usibane cement katika ujenzi wako. Simamia fundi material yote itumike sawa na hakikisha nyumba inanyooka. Wewe uwe pima maji. Nunua Square, kila kona pima.
Asantee kwa mawazo yako Kaka
 
Habari wadau! Naomba kuuliza ukiwa na TZS 20 Milioni na unataka kujenga nyumba ya Vyumba 3 na Master unaweza kuanza na kufika hatua Gani?

Ntashukuru kama mtanipa estimate za kila hatua

Asantee
Utamaliza hadi kupaua, finishing ndo itakubidi ujikusanyekusanye tena kulingana na kiwango unachotaka. Utaweza kuhamia kabisa japo ni kukiri udhaifu
 
Vitisho vimeanza. Nyumba zetu za kawaida anaweza kuhamia kabisa akaremba akiwa ndani
Amna bana jamaa kaongea ukweli lakini, usije kumpa mtu moyo akapewa liramani la kufa mtu uko kwasababu tu ni ya room 3 akaishia kwenye lenta
 
Sisi kuna sehemu tulimpa ramani ya ujenz wa kanisa, mafund wote waliotangulia kuanzia vifaa mpaka ujenz ni zaidi ya 30ml, hiyo ilkuwa kusimamisha nguzo 30 za jengi n.k

Kutoka kwake yeye, mambo yafuatayo akaanza kutueleza.

1. Raman inasema kila nguzo ni nondo 6 za 16mm, ila yeye ametuambia kwa ghorofa moja tu inayobeba watu 50 mpaka 70 na wingi wa nguzo, kila nguzo nondo 4 za 16mm zinatosha sana.

2. Mainjinia wanaweka mambo mengi ktk raman ili kusaidia kupatikana kwa kibali cha ujenzi.

3. Mafundi walipendekeza zile kokoto nyeusi, ila yeye akatuambia tutafute zile kokoto ambazo ni jiwe, na kweli tulizipata uko mbutu kwa 700k kipind kile, ile Mende Scania.

Mambo ni mengi sana, sio rahisi kuyaandika yote kupitia siimu.
Ficha ujinga wako mkuu
 
Back
Top Bottom