Nina milioni 20 nataka kujenga nyumba ya vyumba 3 Dar es Salaam. Naweza fikia hatua gani?

Hapo inategemea na aina ya nyumba(mchoro/ramani)
Ila ikiwa ni hizi za kawaida tu, Mzee ukiwa mwenyewe site, unaweza jenga na kuhamia, ukaja kuimalizia baadae

Kujenga na kuhamia namaanisha utaezeka, utaweka milango na madirisha, ukapiga plasta, unaweza kupiga na ceiling board juu..
 
Sisi kuna sehemu tulimpa ramani ya ujenz wa kanisa, mafund wote waliotangulia kuanzia vifaa mpaka ujenz ni zaidi ya 30ml, hiyo ilkuwa kusimamisha nguzo 30 za jengi n.k

Kutoka kwake yeye, mambo yafuatayo akaanza kutueleza.

1. Raman inasema kila nguzo ni nondo 6 za 16mm, ila yeye ametuambia kwa ghorofa moja tu inayobeba watu 50 mpaka 70 na wingi wa nguzo, kila nguzo nondo 4 za 16mm zinatosha sana.

2. Mainjinia wanaweka mambo mengi ktk raman ili kusaidia kupatikana kwa kibali cha ujenzi.

3. Mafundi walipendekeza zile kokoto nyeusi, ila yeye akatuambia tutafute zile kokoto ambazo ni jiwe, na kweli tulizipata uko mbutu kwa 700k kipind kile, ile Mende Scania.

Mambo ni mengi sana, sio rahisi kuyaandika yote kupitia siimu.
Tunasubiri utuandikie hayo maelezo murua kupitia computer ukitulia au siyo!?
 
Pia msipende kujibu maswali kiurahisi ili uonekane wewe ni mtu wa maana kwa sababu unampa mtu moyo.
Sometimes mtu inatakiwa aondolewe kutoka fikra fulani kabla ya kuanza project yake.
Kwa mfano, mleta mada ni vizuri akishauriwa kuwa nyumba vyumba vitatu haielezi nini unachohitaji.
Angeleta ramani, au akaelezea size ya vyumba etc...
La sivyo tutakuwa tunajibishana tu, unaweza, huwezi, unaweza, huwezi ... kwa siku kumi. No description.
Ameshakueleza bajeti yake ni mil.20,wewe bado unakomaa na descriptions.

Mjibu kwa hiyo bajeti ya mil.20 kwa vyumba vitatu
 
Option hapo imetoka wapi?
Saa zingine, kumwambia mtu afunguke zaidi ndiyo jibu bora na lenye msaada zaidi kuliko kumwambia mtu ahamie halafu atamalizia akiwa ndani.
Nyumba ya vyumba 3 kwa mil.20 mkuu unataka afungukeje? Akutajie rangi ya nyumba?
 
Tufanye hivi f
Fundi Msingi 700,000
Tofari 800 za msingi @1200 =960,000
Mchanga trip 5@ 60,000= 300,000
Nondo 25 @ 26,000=650,000
Cement 40@ 15,000= 600,000
Kokoto 3" = 300,00
Mbao
Chepe
Ndoo
Rings
Kifusi
Jumla msingi tuweke 4,500,000
Boma
Tofari 1500
Cement 40
Koto lori moja
Mbao za renta (utakodi)
Ufundi

Nazo tuweke 4,500,000

Kupaua
Mbao
Mabati(inategemea ni aina gani siku hizi yanepanda sana ) pia na aina ya paa unayoitaka kama nyumba ina kona nyingi mabati yatakatwa sana na mbao zitaenda nyingi pamoja na ufundi

Makadilio milion 7

Grils Madirisha na frem za milango pia nayo itategemea nyumba ina madirisha mangapi
Makadilio 1,500,000

Mfumo wa maji taka makadilio na shimo 1,500,000
Floor makadilio 1,000,000
Nyavu za madirishani 100,000
Unahamia tu fresh
 
Tufanye hivi f
Fundi Msingi 700,000
Tofari 800 za msingi @1200 =960,000
Mchanga trip 5@ 60,000= 300,000
Nondo 25 @ 26,000=650,000
Cement 40@ 15,000= 600,000
Kokoto 3" = 300,00
Mbao
Chepe
Ndoo
Rings
Kifusi
Jumla msingi tuweke 4,500,000
Boma
Tofari 1500
Cement 40
Koto lori moja
Mbao za renta (utakodi)
Ufundi

Nazo tuweke 4,500,000

Kupaua
Mbao
Mabati(inategemea ni aina gani siku hizi yanepanda sana ) pia na aina ya paa unayoitaka kama nyumba ina kona nyingi mabati yatakatwa sana na mbao zitaenda nyingi pamoja na ufundi

Makadilio milion 7

Grils Madirisha na frem za milango pia nayo itategemea nyumba ina madirisha mangapi
Makadilio 1,500,000

Mfumo wa maji taka makadilio na shimo 1,500,000
Floor makadilio 1,000,000
Nyavu za madirishani 100,000
Unahamia tu fresh
Fundi msingi laki 7! Nieleweshe mkuu

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
We tuambie tu kwanza nyumba yako inaukubwa gani alaf tukukadirie,kuna nyumba inavyumba 3 inaukubwa wa sqm 220 huko,mf. kwa ukubwa kama huu 20m inafunga lenta tu na kujenga mashimo ya choo ,
 
Tufanye hivi f
Fundi Msingi 700,000
Tofari 800 za msingi @1200 =960,000
Mchanga trip 5@ 60,000= 300,000
Nondo 25 @ 26,000=650,000
Cement 40@ 15,000= 600,000
Kokoto 3" = 300,00
Mbao
Chepe
Ndoo
Rings
Kifusi
Jumla msingi tuweke 4,500,000
Boma
Tofari 1500
Cement 40
Koto lori moja
Mbao za renta (utakodi)
Ufundi

Nazo tuweke 4,500,000

Kupaua
Mbao
Mabati(inategemea ni aina gani siku hizi yanepanda sana ) pia na aina ya paa unayoitaka kama nyumba ina kona nyingi mabati yatakatwa sana na mbao zitaenda nyingi pamoja na ufundi

Makadilio milion 7

Grils Madirisha na frem za milango pia nayo itategemea nyumba ina madirisha mangapi
Makadilio 1,500,000

Mfumo wa maji taka makadilio na shimo 1,500,000
Floor makadilio 1,000,000
Nyavu za madirishani 100,000
Unahamia tu fresh
Wewe ndo umeandika uhalisia sasa... Mimi nna makadirio mezani hayatofautiani na ulichoandika...
 
Nna fund ana bei za kawaida mno, labda nikupatie mawasiliano yake, yeye atakupa ushaur mzuri.

Mafund wa kisasa watakwambia mpaka kokoto ununue zile nyeusi wakat kokoto jiwe zipo kibao kigamboni, mara cement mifuko kibaoo, mafundi wenye uzoefu ni wazuri mno.
Naomba namba zake
 
Ujenzi unategemea unaufanyia wapi, mara nyingi ujenzi nje ya mji unakuwa kidogo nafuu. Kwa sie tuliojenga Dar katikati ya mji tunaelewa. Kuna tofauti ya kujenga nyumba na mchoro maana wengi wanapachika marofali tu, ndio hao wanaosema nyumba unajenga kwa million 20 mpaka finishing, ushawahi kuona wapi?

Nina nyumba nilijenga ya kibabe huo msingi tu ulikula million 20, hapo sijasimamisha. Hapo chini tu nilitumia tofali elfu 4, nyumba ya appartment ya wapangaji wanne chumba sebule vyoo viwili, jiko na dining ya kizushi, na kibaraza. .

Nyumba yangu ya vyumba viwili, kimoja self, kuna public toilet, kuna sebule na dining ya kizushi, kuna jiko ndani na baraza za ft 4 mbele na nyuma ilinigharimu 70 millions. .

-Msingi tu nilijenga course kumi matofali ya kulala ili niongeze uimara
-Grills nilinunua nondo nikachongesha mwenyewe zile ngumu kutoka kamata
-Milango yangu ya mkongo nilitengeneza kipindi hicho tabora, milango 15 iligharimu 7 million
  • Tiles nimeweka granite nyumba zimegharim 5.5 million na ufundi
  • Baada ya lender juu baraza mbele na nyuma nimejenga course tisa mpaka kwenye bati kuzuia watu wasitoboe barazani wakarukia ndani
-Nyumba nzima iko na gypsum sebuleni nimeweka urembo wa kawaida na taa juu kwenye gypsum inapendeza sikutaka niweke mambo mengi sana
-Nyumba yote nimefunga Aluminium
-Jikoni nimeweka makabati ya juu mbao mpodo sikutaka kuweka makabati mninga wala mkongo kwa sababu yatakuwa mazito sana imenigharim laki 5
  • Bati nimeweka msauzi ufundi nakumbuka pamoja na blandering uligharimu 2,500,000 TZS
  • Mbao zilinigharimu 4 million, nilinunua na za kupigia lenter
-Plasta ilinigharimu 1.2 million
-Kuchimba karo la choo ilinighaarimu 250000/- ufundi uligharimu 240,000/ TZS
- Kujenga nyumba mpaka lenta ufundi ulinigharimu 4 million.
-Geti mbele na nyuma na grills iligharimu 3,500,000/-

Hata hivyo mie ni msomi vitu niliandika mwanzo mwisho gharama zote ninazo. Ujenzi ni gharama asikwambie mtu, mpaka lenta nilitumia 23 million kitu ambacho sikuwahi kutegemea kabisa. Finishing inakula hela hatari kuna vitu vingi kama vifaa vya bomba kifaa kigodo tu unaambiwa laki na nusu, gharama ni kubwa. .

Kuna gharama nyingi za ziada, kama ubebaji, usafiri, ulinzi, NK. Ila siwezi kataa wapo wanaofanya ujenzi mpaka finishing kwa million 20, ila nyumba kuagiza mchanga pwani kuleta huku lori tu laki tatu. Hapo sijapiga gharama za tofali na mambo mengine

IMG_20210122_184755_972.jpg


IMG_20210122_184817_495.jpg
 
Tofali za msingi 6'×1250@ fanya 500-600 kutegemea na mkao wa kiwanja kama kina sloop tofali zitakuwa nyingi kama eneo ni flat hata 300 tu zinatosha.
Kuset na kuchimba msingi 200,000
Tofali za boma 1300 hadi 1500×1100@
Ujenzi wa boma kupau na lipu fanya m3.5 kwa bei za Dar.

Mchanga trip 4 @ 130,000 itategemea ni wa wapi
Kokoto 2 trips chukua za mashine @ 300,000

Shimo la choo (soak away pit) lile la round tofati 300-350 za 5'@1100 Kuchimba shimo 150,000 urefu futi10 mzunguko futi 12 nondo za kufunika 12mm×8-10 @26,000 ufundi weka 300k jumla yake shimo 1 ni kati ya m1.2 hivi kila kitu. Ni vyema ukajenga mawili na lile la kupokea mzigo ila sio lazima kama budget yako ni ndogo.

Mbao za mkanda wa kiuno cha msingi (slab na renta) hizo utakodi kama 80×@2000 pale zitakapo hitajika.
Za kununua kwa kazi za zege ni kama 1/8 pc10@10,000 na 1/6 pc8@6,000 ni lazima uwe na mbao zako kadhaa. Ili ukate mahali ambapo kipimo cha mbao za kukodi kitapelea.

Nondo za mzunguko wa msingi utafanya 18@26,000 watafunga kwa triangle beam ya nchi 5/6 nondo za renta 26@26,000 upana wa nyumba utakuwa kati ya mita 10m/11 kwa vyumba standard sitaki kuingia sana kwenye vipimo najaribu kukupa estimation pekee

Cement ya kazi zote weka mifuko 120@15,000 kama upo Dar tumia Twiga plus.

Kuezeka
fuatavyo:
Bati kuanzia 76 zenye urefu wa 3mt @26000 araf old profile g30 za kawaida.
Mbao: Treated
4/2-100pcs za urefu wa>20ft
2/2-50pcs pia za urefu wa 20ft
1/8/10-15pcs zenye urefu wa 12ft
Bei futi 1 ya 4/2 ni 1000, 2/2 ni 480 na 1/10 ni 18,500 kwa ubao, bei hizi ni kwa dar.

Labour charge 1m
Tiles: Hapa itategemea na quality utakayo i.e china, india Tanzania or spain lakini inarange 15000-60000/sqm
Labour charge 4500-7000/sqm kutegemea na fundi
Kuhusu plaster/ripu inahitaji kuonyesha floor plan ili kujua idadi ya vyumba/partitions pia same to wiring ili kujua no of switches na taa nk.

Rangi pia itategeme ila weka btn 1.6m na 2.5m kuanzia nje na ndani.
Vyoo weka 1m kila choo vyoo viwili. Umeme wa tanesco na maji napo andaa 1m inaweza kushuka kidogo au kuzidi.

Fence weka 4m tofali na ujenzi itategemea na ukubwa wa kiwanja.

Garden kuindaa weka na 1m mbolea miti maua na gardener charges.

Do that math uone utakapo ishia.
 
Back
Top Bottom