Nina milioni 20 nataka kujenga nyumba ya vyumba 3 Dar es Salaam. Naweza fikia hatua gani?

Pia msipende kujibu maswali kiurahisi ili uonekane wewe ni mtu wa maana kwa sababu unampa mtu moyo.
Sometimes mtu inatakiwa aondolewe kutoka fikra fulani kabla ya kuanza project yake.
Kwa mfano, mleta mada ni vizuri akishauriwa kuwa nyumba vyumba vitatu haielezi nini unachohitaji.
Angeleta ramani, au akaelezea size ya vyumba etc...
La sivyo tutakuwa tunajibishana tu, unaweza, huwezi, unaweza, huwezi ... kwa siku kumi. No description.
Ni sahihi kabisa, milioni 20 inaweza ikaishia kwenye boma tu bila kuezeka kutegemea na factor mbalimbali, mfano nyumba utaweka beam kwenye msingi? Utaweka NONDO ngapi kwenye hiyo beam? Unataka msingi unyanyuke au nyumba iwe kama imekaa ardhini? Ukubwa wa vyumba ukoje? Strength ya linta yako iweje? Hizo zote ni factor katika ujenzi, nyumba A na B zinaweza tumia ramani moja lakini kabla ya finishing nyumba A ikatumia mara mbili ya gharama zilizotumika katika nyumba B. Baada ya finishing nyumba hizo mbili zinaweza kutofautiana gharama hadi mara tano. Factor kubwa ni uimara na ubora wa vitu vitakavyotumika
 
Sisi kuna sehemu tulimpa ramani ya ujenz wa kanisa, mafund wote waliotangulia kuanzia vifaa mpaka ujenz ni zaidi ya 30ml, hiyo ilkuwa kusimamisha nguzo 30 za jengi n.k

Kutoka kwake yeye, mambo yafuatayo akaanza kutueleza.

1. Raman inasema kila nguzo ni nondo 6 za 16mm, ila yeye ametuambia kwa ghorofa moja tu inayobeba watu 50 mpaka 70 na wingi wa nguzo, kila nguzo nondo 4 za 16mm zinatosha sana.

2. Mainjinia wanaweka mambo mengi ktk raman ili kusaidia kupatikana kwa kibali cha ujenzi.

3. Mafundi walipendekeza zile kokoto nyeusi, ila yeye akatuambia tutafute zile kokoto ambazo ni jiwe, na kweli tulizipata uko mbutu kwa 700k kipind kile, ile Mende Scania.

Mambo ni mengi sana, sio rahisi kuyaandika yote kupitia siimu.
Huo si unafuu wa gharama bali ni kuweka rehani maisha ya watu watakaotumia jengo hilo. Huyo fundi anajua chochote kuhusu sayansi ya structural design?
 
Ni sahihi kabisa, milioni 20 inaweza ikaishia kwenye boma tu bila kuezeka kutegemea na factor mbalimbali, mfano nyumba utaweka beam kwenye msingi? Utaweka NONDO ngapi kwenye hiyo beam? Unataka msingi unyanyuke au nyumba iwe kama imekaa ardhini? Ukubwa wa vyumba ukoje? Strength ya linta yako iweje? Hizo zote ni factor katika ujenzi, nyumba A na B zinaweza tumia ramani moja lakini kabla ya finishing nyumba A ikatumia mara mbili ya gharama zilizotumika katika nyumba B. Baada ya finishing nyumba hizo mbili zinaweza kutofautiana gharama hadi mara tano. Factor kubwa ni uimara na ubora wa vitu vitakavyotumika
Msipende kutisha sana watu mil.20 inajenga vizuri tu nyumba ya room 3,hayo unayoyataka wewe ata nyumba ya room2 tu inaweza kufikia ata mil.800!

Haitaji vitasa vya dhahabu,anahitaji nyumba ya kuishi binadam
 
Habari wadau! Naomba kuuliza ukiwa na TZS 20 Milioni na unataka kujenga nyumba ya Vyumba 3 na Master unaweza kuanza na kufika hatua Gani?

Ntashukuru kama mtanipa estimate za kila hatua

Asantee
Kama huna kiwanja mkuuu ni ngumu na hata kama ungekuwa nayo bado haimalizi Bali utapaua
Finishing tafuta peas nyingine
 
Msipende kutisha sana watu mil.20 inajenga vizuri tu nyumba ya room 3,hayo unayoyataka wewe ata nyumba ya room2 tu inaweza kufikia ata mil.800!

Haitaji vitasa vya dhahabu,anahitaji nyumba ya kuishi binadam
Suala la kuweka beam kwenye msingi kwa wengine ni jambo la lazima na kwa wengine si lazima na kuna maeneo kama chalinze ukiikwepa hiyo kitu, ndani ya miaka mitano utaichukia hiyo nyumba kwa kupata nyufa nyingi na kubwa. Tunachumueleza tunamaanisha kuwa M20 inaweza ikafika mbali au isifike mbali kutegemea na eneo na factor nyingine anataka nyumba iwe na uimara wa kiwango gani, na eneo alipo lina dhuru kiasi gani majengo.

Ni observations unazozidharau lkn amini nakwambia ni muhimu sana. I was told by people like you kuwa msingi wa nyumba yangu utagharimu 5M but in reality ule msingi hadi kujaza kifusi uligharimu 9.7M. Tunapozungumzia gharama za ujenzi ni hadi wewe kuitembelea site yako kama kunahitaji transport ni sehemu ya gharama za ujenzi, hizo ni cost unaweza ignore but imagine huna hata bajeti ya kutembelea site yako inayojengwa, utawaachia mafundi waendelee na wewe utakutana nao wakimaliza nyumba?? They are small issues but they do add value to your project. Wacha tumueleza baadhi ya mambo anayopaswa kuwa nayo kichwani
 
Nna fund ana bei za kawaida mno, labda nikupatie mawasiliano yake, yeye atakupa ushaur mzuri.

Mafund wa kisasa watakwambia mpaka kokoto ununue zile nyeusi wakat kokoto jiwe zipo kibao kigamboni, mara cement mifuko kibaoo, mafundi wenye uzoefu ni wazuri mno.
Na Fundi mwenyewe ndiyo wewe. Nimeamini sasa kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake
 
Tunauza mbao kwa bei za jumla
2*4 fut 12=4400
2*4treated fut 12=4800
1*6 fut 12 = 4400
1*8 fut 12= 8500
1*8 ya fisherboard=9500
1*10=13500
1*10 ya fisherboard= 15000
2*2treated fut 12=2500
2*2 fut 12=2300
2*4treated fut 18=9500
2*6 fut 12=8500
2*6treated fut 18=16000
2*2treated fut 18=5000
2*3 fut 12=3500
1*4 fut 18=4000
1*4 fut 12=2500
Tunafanya delivery popote ulipo kwa Dar-es-salaam ,tunapatikana kwa namba hizi hapa 0759630751,
0654830416,
0687371138
vile vile huduma ya kuchana,kuranda na kusize mbao inapatikana ofisini kwetu ..
Ofisi zetu ziko Mbuyuni -Bagamoyo road
 
Kwa hio bei utajenga mbagala,kigamboni na kule kisemvule

Huku bagamoyo road ma morogoro road ni ngumu sana

Hizo ni semi prime areas
 
Nna fund ana bei za kawaida mno, labda nikupatie mawasiliano yake, yeye atakupa ushaur mzuri.

Mafund wa kisasa watakwambia mpaka kokoto ununue zile nyeusi wakat kokoto jiwe zipo kibao kigamboni, mara cement mifuko kibaoo, mafundi wenye uzoefu ni wazuri mno.
Huyo fundi wako baki nae mwenyewe mkuu....JF mafundi tupo ndio maana kauliza huku
 
Kwa mtu anaye strugle na cash , hutakiwi kumpa options ngumu ngumu
Uzuri ameweka wazi kabisa , ana 20 millions , huna sababu ya kumpatia extravagant options

Ndo vitisho vyenyewe hivyo.
Kuna watu kutisha ndio jadi yao
 
Back
Top Bottom