Nina milioni 20 nataka kujenga nyumba ya vyumba 3 Dar es Salaam. Naweza fikia hatua gani?

Ramani ya hivyo vyumba vi3 ikoje? Ni muundo wa moja kwa moja (darasa?) Au L?
Kama ni darasa gharama zitapungua kidogo,kama ni ramani ya L gharama itazidi kidogo (haswa kwenye upauaji)
Ukubwa wa hivyo vyumba ukoje? Ukubwa wa vyumba uta_determine idadi ya tofali utakazozitumia kwenye ujenzi. Kwa uzoefu na kimakadirio haijalishi ukubwa wa hivyo vyumba kwa vyumba vi3 na hiyo master unayoitaka,complete kuanzia msingi mpaka level ya kuezeka andaa tofali 3000,shimo la choo andaa tofali 450 appr shimo liwe ft 12ur*8 mzunguko..tofali jumla itasoma 3450
Jitahidi ku_survey maduka tofauti ya ujenzi ili upunguze gharama za manunuzi ya vifaa,maduka ya Dar yana utofauti wa bei,ila uwe makini,utofauti ukiwa mkubwa sana hiyo bidhaa inaweza kua ni copy,so ukauziwa copy kwa bei ya original
Mafundi pia wana bei za kuropoka,jitahidi kupata mwenye nafuu na mzoefu wa kazi.
Kimsingi pesa yako inatosha ila sio mpaka finishing,kama huna haraka na kuhamia unahamia mengine mbele kwa mbele,ujenzi huwa hauishi utaimalizia polepole..
 
Kama una kiwanja tafuta ramani uanze kujenga, ukiisimamia mwenyewe naamini utafikia hatua nzuri tu, kila la heri
 
Asilimia kubwa ya wabongo wa maisha ya Kati nyumba wanamalizia wakiwa ndani. Kuna watu kibao wanajenga magorofa na wanamalizia wakiwa ndani, mkuu labda wewe si mtanzania wa maisha ya kawaida.
Mkuu labda unalazimisha tu ubishi.
Hakuna niliposema watu wengi wanamalizia nyumba na kwenda kuishi.
Tatizo ni unapomwambia mtu atamalizia mbele kwa mbele utakua hujamsaidia.
Afadhali umwambie mtu specifically nyumba ya aina hii, yenye vitu hivi itakugharimu kiasi fulani. Ajue kabisa.
Mimi nimefunga nyumba (paa na grills/rough floor) kwa milioni 9 kasoro, vyumba vitatu vyenye 4mx4m December mwaka jana.
Kwanini nisiamini mtu anaweza kuhamia kwake kwa 20m? Naamini, ila nyumba ya aina gani?
Usichukulie nyumba anayoiwaza mleta mada wewe unaijua .... That's wrong and misleading.
Nyumba ni yake siyo yako, mwambie afunguke ndiyo utamsaidia vizuri zaidi.
 
Nna fund ana bei za kawaida mno, labda nikupatie mawasiliano yake, yeye atakupa ushaur mzuri.

Mafund wa kisasa watakwambia mpaka kokoto ununue zile nyeusi wakat kokoto jiwe zipo kibao kigamboni, mara cement mifuko kibaoo, mafundi wenye uzoefu ni wazuri mno.
Naomba unipatie mawasiliano yake Ndugu
 
Hatua utakayofikia inategemea na aina ya nyumba unayoitaka.
3 bedrooms ni too general. Kuna 2 bedroom houses zipo expensive kuliko 6 bedroom houses.
Yaani swali ni too general.
Ni kweli Kaka! Nyumba ya Kawaida tuu
 
Kwa pesa hiyo kama una kiwanja , unahamia kabisa , ila bila finnishing
Wengi wetu tunahamia nyumba ikimalizika tuu. Finishing unafanya ukiwa ndani. Hapo nimeuliza nyumba tuu itafika hatua gani bila kuweka Finishing
 
Uko sahihi sana.
Nb: pia wapo wanaomini ghorofa daima ni expensive kuliko bungalow
Na zaidi Yaani katika vitu vinavyonishangaza hua ni hili la mtu kudefine nyumba kwa idadi ya vyumba..wakati hiyo ni spatial arrangements tu. Bora wanaoeleza kwa ukubwa wa skwea mita.
Kweli Kaka! Kama kuna wajuzi wa kuelezea kwa kutumia Sq M wanaweza kutupa muongozo
 
Mkuu labda unalazimisha tu ubishi.
Hakuna niliposema watu wengi wanamalizia nyumba na kwenda kuishi.
Tatizo ni unapomwambia mtu atamalizia mbele kwa mbele utakua hujamsaidia.
Afadhali umwambie mtu specifically nyumba ya aina hii, yenye vitu hivi itakugharimu kiasi fulani. Ajue kabisa.
Mimi nimefunga nyumba (paa na grills/rough floor) kwa milioni 9 kasoro, vyumba vitatu vyenye 4mx4m December mwaka jana.
Kwanini nisiamini mtu anaweza kuhamia kwake kwa 20m? Naamini, ila nyumba ya aina gani?
Usichukulie nyumba anayoiwaza mleta mada wewe unaijua .... That's wrong and misleading.
Nyumba ni yake siyo yako, mwambie afunguke ndiyo utamsaidia vizuri zaidi.
fundi akipewa budget anajiongeza kwa kumpa options zinazoendana na budget yake
 
fundi akipewa budget anajiongeza kwa kumpa options zinazoendana na budget yake
Hizo options zinatokana na yeye alitaka nini kwanza. Halafu atajua pa kuongeza na pa kupunguza.
Unaweza kupewa vyumba vya mita 2.5 kwa 2.5 lakini wewe bora uwe na vyumba vikubwa na public toilet kuliko vyumba vidogo master.
Au unataka sebule kubwa jiko dogo.
Au jiko kubwa sebule ndogo (labda mama anafanya catering).... etc
Cha muhimu ni kujieleza matamanio yako, halafu utashauriwa kwa bajeti yako.
Siyo kinyume, yaani bajeti halafu unaambiwa ujenge banda la "L" lenye ma-gypsum ya urembo.
 
Habari wadau! Naomba kuuliza ukiwa na TZS 20 Milioni na unataka kujenga nyumba ya Vyumba 3 na Master unaweza kuanza na kufika hatua Gani?

Ntashukuru kama mtanipa estimate za kila hatua

Asantee
Habari za Mchana wadau

Nashukuru saana kwa michango yenu ambayo imenipa moyo na changamoto pia. Labda niweke wazi kidogo mahitaji ya nyumba ninayotaka kujenga labda naweza kupata mawazo mazuri zaidi yatakayonisaidia.

Kwanza huu ndio ujenzi wangu wa kwanza na sina uzoefu katika masuala ya ujenzi ila nimejaribu kufanya research kwa baadhi ya vitu ambavyo naweza kuanza navyo.

Kiwanja changu kipo sehemu tambarare kabisa na kimezungukwa na majirani ambao wameshajenga. Maji yapo na umeme upo mita 100 tu. Nimeshavuta Maji ya Dawasa katika plot yangu.

FLOOR PLAN YA NYUMBA
Nyumba ni ya vyumba 3 yenye
_ Master Bedroom yenye WIC
_ Vyumba 2 plain
_ Living/Sitting Room
_ Dinning
_ Jiko na Stoo
_ Public Washroom

Kianzio nilichonacho kama nilivosema hapo ni 20mn so nataka walau kupata muelekeo wa wapi naza kufika lakin pia kujua mahitaj muhimu

Mfano
Matofali
Cement
Ni hatua ipo Nondo zitahitajika
Nk
 
Jenga msingi wa nyumba nzima. Pili anza kujenga nusu nyumba, upande wa vyumba hadi ufanye finishing. Upande wa sebule utapambana nao chenji ikibaki.
 
Back
Top Bottom