Je, kwa Tsh Milioni 40 tu GENTAMYCINE 'nikijibanabana' naweza Kuitumia Kukamilisha yafuatayo?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,037
1. Kununua Uwanja wa Ujenzi wa Tsh Milioni 4 na Laki Saba na Elfu Hamsini ( Tsh 4,750,000/= ) maeneo ya ndani ndani kiasi Kinondo, Mingoyo, Vikawe na Mapinga.

2. Kununua Ramani ya Nyumba Shilingi Laki Mbili na Elfu Hamsini ( Tsh 250,000/= )

3. Kujenga Nyumba ya Vyumba Vitatu kwa Tsh Milioni 25 huku na Gharama ya Ufundi / Mafundi ( Labour Charge ) ikiwemo

4. Kuiwekea Madirisha ya Kawaida na Kununulia Makochi, Vitanda, Jiko la Gesi, Masufuria, Ndoo, Vjiko, Umma, Upawa, Mabeseni, Friji, Makabati, Meza ya Chakula kwa Tsh Milioni 8.

5. Kuvuta Umeme na Maji kisha kuweka Taa ( Bulbs ) pamoja na Kuweka Feni za Kawaida tu kila Chumba ili wakati wa Joto Kali la Dar es Salaam nisibanikwe nalo.

Ukweli ni kwamba Kiasi nilichonacho / kilichopo ni Tsh Milioni 50 ila nataka Kujibana kwa Tsh Milioni 40 tu ya kufanya yote hayo niliyoyataja hapa juu ili hii Tsh Milioni 10 itakayobakia niitumie kwa Kununulia Pikjpiki ( Bodaboda ) zangu Nne ( 4 ) tu au niiweke katika Mfumo wa UTT AMIS ili niwe napata Interest ( Faida ) ya kila baada ya Miezi Minne au Miezi Sita au kwa Mwaka (Miezi Kumi na Mbili ) tu.

Tafadhali karibuni nyote katika Kuniongoza na Kunishauri vyema katika hili Jambo langu la Kimaendeleo baada ya Kuzichangachanga Kiubishi.

Pia kuwa Huru kabisa nawe pia kuja na Mtiririko wako (kama ambao Mimi nimeutoa) hapa juu ila hakikisha tu hutoki ndani ya Kiasi hicho cha Pesa cha Shilingi Milioni Arobaini ( Tsh 40,000,000/= )

Karibuni na Nitawashukuruni mno. Na tambueni Nyumba niitakayo ni ya Kawaida ( ya Maisha yangu tu ya Kawaida ) na si ile ya Kitajiri ( Kifahari ) kama mlizonazo wana JamiiForums wote hapa.
 
1. Kununua Uwanja wa Ujenzi wa Tsh Milioni 4 na Laki Saba na Elfu Hamsini ( Tsh 4,750,000/= ) maeneo ya ndani ndani kiasi Kinondo, Mingoyo, Vikawe na Mapinga.

2. Kununua Ramani ya Nyumba Shilingi Laki Mbili na Elfu Hamsini ( Tsh 250,000/= )

3. Kujenga Nyumba ya Vyumba Vitatu kwa Tsh Milioni 25 huku na Gharama ya Ufundi / Mafundi ( Labour Charge ) ikiwemo

4. Kuiwekea Madirisha ya Kawaida na Kununulia Makochi, Vitanda, Jiko la Gesi, Masufuria, Ndoo, Vjiko, Umma, Upawa, Mabeseni, Friji, Makabati, Meza ya Chakula kwa Tsh Milioni 8.

5. Kuvuta Umeme na Maji kisha kuweka Taa ( Bulbs ) pamoja na Kuweka Feni za Kawaida tu kila Chumba ili wakati wa Joto Kali la Dar es Salaam nisibanikwe nalo.

Ukweli ni kwamba Kiasi nilichonacho / kilichopo ni Tsh Milioni 50 ila nataka Kujibana kwa Tsh Milioni 40 tu ya kufanya yote hayo niliyoyataja hapa juu ili hii Tsh Milioni 10 itakayobakia niitumie kwa Kununulia Pikjpiki ( Bodaboda ) zangu Nne ( 4 ) tu au niiweke katika Mfumo wa UTT AMIS ili niwe napata Interest ( Faida ) ya kila baada ya Miezi Minne au Miezi Sita au kwa Mwaka ( Miezi Kumi na Mbili ) tu.

Tafadhali karibuni nyote katika Kuniongoza na Kunishauri vyema katika hili Jambo langu la Kimaendeleo baada ya Kuzichangachanga Kiubishi.

Pia kuwa Huru kabisa nawe pia kuja na Mtiririko wako ( kama ambao Mimi nimeutoa ) hapa juu ila hakikisha tu hutoki ndani ya Kiasi hicho cha Pesa cha Shilingi Milioni Arobaini ( Tsh 40,000,000/= )

Karibuni na Nitawashukuruni mno. Na tambueni Nyumba niitakayo ni ya Kawaida ( ya Maisha yangu tu ya Kawaida ) na si ile ya Kitajiri ( Kifahari ) kama mlizonazo wana JamiiForums wote hapa.

Ninaungana na TEC 100% kwa Tamko.
Hela nyingi sana hiyo inatosha.
 
Back
Top Bottom