Nina maumivu sana jamani, nahitaji msaada wenu

virginity

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
882
908
Habari zenu,

Nilikua na mpenzi ambae tumedumu kwa miezi minne sote tulipendana kwa dhati na kwa kipindi hicho yeye ndio alikua ameanza kazi hivyo mshahara alikua hajaanza kupata hivyo kila nilipokua na kidogo sikusita kumpatia.

Kilichonifanya nije hapa jamvini ni kwamba mwanaume huyu amebadilika sana, hapigi simu nikipiga hapokei, nikimtumia jumbe hajibu kiukweli hali hii inaniumiza sana nashindwa hata kula, nimekua mtu wa kulia lia kila mara.

Tafadhali naombeni msaada wenu maana maji yamenifika shingoni.
 
Mahusiano mazuri hujengwa na mawasiliano mazuri kwa kiasi kikubwa bila hivyo kutakuwa na tofauti baina ya ninyi wawili , nakushauri mtafute akueleze tatizo ni nini linalopelekea kupunguza mawasiliano

Wahenga walisema pata pesa tujue tabia yako ,sijui walimaanisha nini...
 
Nilimuuliza ktk hali ya ukali alisema kwamba anastress za kifamilia na hafkirii kuhusu mapenzi kwa sasa hivyo nimuache
 
Habari zenu!
Nilikua na mpenzi ambae tumedum kwa miezi minne sote tulipendana kwa dhat na kwakipindi hicho yeye ndio alikua ameanza kaz hivyo mshahara alikua hajaanza kupata hivyo kila nilipokua na kidogo sikusita kumpatia.
Kilichonifanya nije hapa janvini ni kwamba: mwanaume huyu amebadilika sana, hapigi cm nikipiga hapokei, nikimtumia jumbe hajibu.kiukweli hali hii inaniumiza sana nashindwa hata kula,nimekua mtu Wa kulia lia kila mara, tafazali naombeni msaada wenu maana maji yamenifika shingoni
Virginity mbona halijawa tatizo kama unavodhani? Hujui kwanini hapigi au hapokei simu zako na hujajipa muda kujua ni kwanini, pia hujasema amedumu na tabia hiyo kwa muda gani. Miezi minne katika mapenzi sio muda mrefu sana kukufanya upoteze umakini wa kushughulikia mahusiano yenu. Nnachokiona umempenda saana jamaa na huwezi kukaa mbali nae! Kama ukiweza endelea na shughuli zako za kazi/biashara, socialize na watu au kama mtu wa ibada concentrate huko jifanye kama hayupo na muda utaamua hatima yenu bila maumivu
 
Msaada uta upata kwangu plz ni pm ili uc lie tena
 
Yaani huu ambao nimeuesabu wanne wote mawasiliano c mazuri kakaangu, ni kweli nilimpenda sana sifichi. Lakini hali yake yakukaa kimya ndio inaniumiza
 
Pole sana dada angu, inabid uchukue maamuz magumu kutengeza furaha ya mbeleni uendako kuliko kuendelea kuumia!
 
Hilo jina lako limenifanya nikupende gafla karibu ktk ulimwengu wangu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom