NINA MAUMIVU MAKUBWA SANA

NINA MAUMIVU MAKUBWA SANA

Kwa hali hii sisi wa simbe tuta oa kweli
Kuoa lazima, kila mtu ana wakwake, kila ndoa ina changamoto zake, je mke awe safi halafu wewe
uwe ndiye mwenye shida, wewe oa tu mkuu [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] usikwepe jukumu kuoa.
 
Kuoa lazima, kila mtu ana wakwake, kila ndoa ina changamoto zake, je mke awe safi halafu wewe
uwe ndiye mwenye shida, wewe oa tu mkuu [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] usikwepe jukumu kuoa.
Tatizo walio oa wengi wanalalama najaribu kuwaza na kuwaza nabaki kumpiga tarehe tu mchumba wangu [emoji51][emoji51]
 
Tatizo walio oa wengi wanalalama najaribu kuwaza na kuwaza nabaki kumpiga tarehe tu mchumba wangu [emoji51][emoji51]
Wanalalamika lakini hawavunji ndoa, chukua hizo changamoto fanyia kazi
 
Hii Leo Sijui ni thread ya ngapi huko ya Vijana kuumizwa na Wapenzi wao WA Kike. Poleni Sana
 
Wazazi wanaovuruga ndoa za watoto wao huwa wanataka nini?

Halafu mtu ukishaingia ndoani kisha ukaruhusu watu wa nje hata kama ni wazazi wakuendeshe akili hovyo basi ndoa haikufai.
 
Kuna mtu aliimbia " MAGUMU HUYAPITII PEKE YAKO,HAKUNA AMBAE HAJATOKA MBALI"
baba yaongee upate ushauri yasije kutokea ya polisi
 
Pole mkuu. Tuliza mawazo. Jipe kama wiki moja ya kutafakari kilichotokea na nini kifuate. Ukikwama piga namba hiiii... Ops au nichek inbox
 
Kiufupi tu,mke wangu kipenzi nimeishi nae zaidi ya miaka 5,kaamua kusikiliza wazazi wake na kufuata wanavyotaka wao,uvumilivu umenishinda imenibid kuvunja familia hii,tuna watoto wawili kila nikiwaza kutengana nao nabaki naumia sana,maamuzi niliyokua nimefikia mungu ndo anajua,nateseka sana ndugu zangu nikija kutulia nitaleta mkasa mzima hapa na wengine wenye situation ngumu mpate kujifunza chochote
Pole sana ndugu yangu,mungu atakunyoshea mkono na nakuomba husiwaache wanao kwa kuwa ameamua hivyo wewe muombe mungu atakusaidia na hili litapita.Kama unekuwa ukifatilia mada zangu hapa jamvini nimekuwa mara nyingi nongelea juu ya hii tabia ya wenzetu ambayo si nzuri.
 
Pole kiongozi, wengi tunamitihami mikali sana kwenye hizi family. Mungu akutie nguvu
 
Pole Mkuu. Na siku zote ndoa ikishaingiliwa na Wakwe kwa upande wowote lazima kuwe na mawili kuijenga au kuibomoa.

Maana unakuta kama ni Mume au Mke hawezi fanya kitu hasa kinachousu familia yake bila kushirikisha wazazi wake.
Basi mwenzio eti nimehisi ndo ile strategy yetu ileeeee.....tuliwahi discuss kitambo kidogo
 
Pole rafiki.

Take it easy na mfanye Mungy kuwa kimbilio lako.

Kumbuka Mwenyezi Mungu hakupi mzigo unaozidi uwezo wa mabega yako.

You never know, maybe its better things turned this way. Time will tell hun. So for now relax, take a deep breath and let God take over.
 
sikuukitoa mkasa mzima,nitashauri

kwa sasa nasema pole kwako na mke wako, maana sijui nani tatizo,

Huzuni yangu kwa watoto
 
Pole sana ila kafanya sahihi hujajua tu .
Ngoja nikupe kasomo japo sijaolewa ni hivi mkioana kuna mengi .
Kukwaruzana
Kusikilizana
Hata kuaminiana ila usitarajie mtu akusikilize wewe no ikija kwa ndugu zake au wazazi aise yupo radhi kukuacha kama ndugu wakimshauri au wazazi .
Kwanini hapo sasa ndipo patamu.
1.wanaume hamtabiriki mnaweza kumuacha nakuoa kwingine
2.unaweza kumnyanyasa nakumtesa kwa njia mbali mbali ila ndugu zake hawatamfanyia hivyo ni ngumu au wazazi wake.
Yaani familia yako ni ngumu sana kukutenga kam mume unayeishi naye ndani.
Ni asilimia ndogo sana ndugu sio msaada kwao.
Kwa hiyo familia ni bora siku zote kushinda mume.
Vile vile hata kwa mke anaweza olew tena anaweza kukutenda au kukutenga ila familia yako ni ngumu kufanya hivyo msamehe tu kwani ndoa ni ngumu siku zote .
Maisha ni mabaya endapo umeoa ndivyo sivyo pole sana.
Ila huo ni ukweli kuoa sio kuaminika bali nikupata familia ila usitegemee mke au mume atenge familia yake kisa kaoa au kaolewa mke au mume niwa pitaji ila Mungu na familia yako ndiyo watasimama daima na wewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom