Nina 70,000 niifanyie nini

Nina 70,000 niifanyie nini

Mtoa mada ulifanikiwa.
Idea niliyokupa ni nzuri sana.

Njoo kariakoo
Nakupeleka kwa mhindi unanunua flash disk na memory card 16 gb @8000 unauza 15,000/=
Hapo unachukua 4 inakua 32,000

Kuna taa za solar kali zinauzika sana wanuza 7500 jumla.... mtaani unauza 15000. Unanunua 3 kwa 22500.

Kuna feni flani zinauzwa jumla 8000 unauza 15,000/=




Vyote vinauzika kwa haraka
 
Mtoa mada ulifanikiwa.
Idea niliyokupa ni nzuri sana.

Njoo kariakoo
Nakupeleka kwa mhindi unanunua flash disk na memory card 16 gb @8000 unauza 15,000/=
Hapo unachukua 4 inakua 32,000

Kuna taa za solar kali zinauzika sana wanuza 7500 jumla.... mtaani unauza 15000. Unanunua 3 kwa 22500.

Kuna feni flani zinauzwa jumla 8000 unauza 15,000/=




Vyote vinauzika kwa haraka
Ntakutafuta soon mzee
 
Hakuna aliyeanzia pakubwa, hiyo 70, 000 japo ndogo, lakin unaweza kufanya jambo kubwa. Anza biashara ya kuku, tafuta kijiwe , anza hata na kuku watano (25, 000) wa Dar hawaachi kitu, kuanzia utumbo mpaka miguu ya kuku wewe uza.
kweli kabisa
 
Fanya kama huna hiyo hela,ifiche mahali usi ione kbsa kisha anza kusaka ajira kibarua yani Teseka lala njaa jitose kwenye maisha na wala usiikumbuke ile 70 kule ulipoificha,nina uhakika utapata tena hela.

ukipata tena kaifiche kule ulipoficha ile 70 ya mwanzo,ingia tena tafuta kbarua,saka pesa,saka kazi teseka hasa usichague kazi,utapata tena najua,chukua hyo amount kaongezee kule kwenye zile za mwanzo.

nenda na mwendo huo huo hadi utakapoona sasa nimechoka nahitaji kufanya biashara yangu nipumzike kidogo,katoe zile hela ulipokua unazificha angalia una kiasi gani kisha kwenye hiyo hela fungua biashara inayohtaji mtaji wa ile 70k ya mwanzo kbsa,yani fanya kama una 70k tafuta biashara ya mtaji huo fanya hela zingine ziache zikulinde na kuipa backup biashara yako itakapoyumba.
Moja ya wazo bora na la kimkakati zaidi
 
Fungua genge tu uza mboga mboga nyanya nk
 
Back
Top Bottom