Mtaji wa laki 2 ( 200,000) Fanya biashara hizi

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,736
Reaction score
39,284
Nataka niwatie moyo vijana wanaohangaika na mitaji mikubwa, basi tumieni hicho kidogo ulicho nacho

Hakuna pesa isiyofanya biashara, pesa yoyote ina uweZo wa kufanya biashara na kuzaa nyingine
Hapa nitashare na wadau biashara ya kufanya ukiwa na mtaji kiduchu

1. Nunua WiFi 3 Kwa 70,000 funga sehemu za masoko.
Wifi 1 ina uweZo wa kuhudumia watu 20,
Gharama za bando la internet ni kubwa na watu wengi hawamdu hizo gharama za mitandao ya simu.

Sasa wewe tafuta angalau watu 10 tu wakupe 500 Kwa siku ambapo hapo utakuwa na uhakika wa kupata 15,000 Kwa siku Kwa WiFi zako 3 ukiwa umekaa bila kumwaga jasho

2. Biashara ya mkaa
Mtaji wa 200,000 una uhakika wa kupata gunia zaidi ya mbili
Watu wengi wa uswahilini hawana uweZo wa kutumia gasi au umeme

3. Biashara ya matunda
Nunua madeli mazuri katakata matunda tembeza huko 10,000 ya faida Kwa siku

4. Chuma chakavu
Mtaji wa 200,000 unakutosha kusota na kupambania mavyuma na kwenda kupima Kwa na agent wakubwa, hakika hutakosa faida mpambanaji

5. Biashara ya kuuza uji
Kama mwanamke hii inakufaa zaidi amka alfajiri au jioni uza zako uji mtaani tena kama kipindi hiki cha mfungo utapata pesa nyingi

6. Biashara ya viungo vya vyakula.
Hii biashara inalipa mno na ina mtaji mdogo mno, tunaenda kwenye kipindi cha sikukuu za Eid na pasaka ndo kipindi cha kupiga pesa
Tafuta hizo binzari, vitunguu swaumu, pilau masala, cocoa, karufu, iriki, mdarasani n.k
Uza Kwa watu wa maduka, au tembeza majumbani

Pambania ulipo
 
1. Nunua WiFi 3 Kwa 70,000 funga sehemu za masoko.
Wifi 1 ina uweZo wa kuhudumia watu 20,
Sasa wewe tafuta angalau watu 10 tu wakupe 500 Kwa siku ambapo hapo utakuwa na uhakika wa kupata 15,000 Kwa siku Kwa WiFi zako 3 ukiwa umekaa bila kumwaga jasho
Hapo mkeka unasoma 210,000 na kulipia kila mwezi ni 210,000 emu anza tena utajiri wa PDF ni mtamu sana
 
5. Biashara ya kuuza uji
Kama mwanamke hii inakufaa zaidi amka alfajiri au jioni uza zako uji mtaani tena kama kipindi hiki cha mfungo utapata pesa nyingi
Hii biashara ni nzuri ila inahitaji Ubunifu na haiitaji mtu MCHOYO wanachokosea wengi wanaofanya hii biashara ni wana namna fulani ya UCHOYO, onjosha fanya km wale wanaouza karanga au ubuyu onjesha uji nusu kikombe wengine watanunua baada ya kuonja
 
Uji kama mtu ananunua ananunua tu hamna haja ya kuonja.
Yaani uonje uji ndo ununue kikombe cha 500
 
Ila we jamaa unajiita ngara23 nuksi Sana! Juzi tu hapa ulitoa gazeti reeefu ukiwakandia vijana wapambanaji na hapa nanukuu
[IMG alt="ngara23"]https://www-jamiiforums-com.cdn.ampproject.org/ii/AW/s/www.jamiiforums.com/data/avatars/m/565/565550.jpg?1749207170[/IMG]

ngara23

JF-Expert Member​

Tuambizane ukweli ambao watu wengi huwa hatuambiani, Huwa tunafarijiana tu
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aliwambia vijana huwezi kutoboa maisha Kwa kuuza uduvi, watu wakamwijia juu

Huo uvivu wa kukataa kumwaga jasho na kuumiza akili ndo hivo tunauwa vijana wanakosa ubunifu na kuishia kuwa masikini wa kutupwa

Kijana ukiwa na nguvu Fanya kazi au biashara Kwa bidii na tengeneza kesho yako

Kijana uliyekamilika usifanye biashara au shughuli zifuatazo

1. Kuuza genge
Kijana wa miaka 20/ 22/23, unajisifu kumiliki genge, yaani nguvu zako zote na akili unashinda unakata kabichi na kuuza kitunguu 100, lini utashika million 100, lini utaenda China au Dubai, lini utakaa baa ule mtungi wa laki 5
Kwanini usikimbie Kariakoo ukachukua mzigo wa nguo au cover A simu ukimbize chap upige faida ya maana

2 Kushona viatu
Kijana mwenye nguvu upo kibarazani unashona na kungarisha viatu.
Binafsi laZima ni kudharau nikikuta unafanya hii shughuli Dar es salaam

3. Kuchoma vitumbua
Kijana mwenye nguvu unaibuka na idea ya kuchoma vitumbua, utatoboa lini, fikiria biashara ya kukutoa mapema

4 Kuuza miguu ya kuku
Hii biashara inatakiwa wafanye wabibi, kijana mdogo unauzaje biashara ya mabibi kama hii
Amka acha uvivu Katie jasho upate pesa

5. Kuchemsha mayai
Kijana mjinga unatembea na trey ya mayai mtaani ati upo mjini unapambana, we ni jinga na pumbavu kwanini usije huku tukalime maharage na mahindi

6. Kuuza kahawa, tangawizi na kashata
Hapa kijana unajimaliza kifikira, jinga sana wewe Tanzania kubwa hivi, amani yote hii, unapata wazo la kutembeza kahawa kwenye birika.
Kwanini usifate kuku Morogoro,

7 kuchoma mahindi

8. Kuuza vipande vya matikiti kwenye deli
Yaani ununue Tikitiki ukate vipande kadhaa na eti ukawe tajiri

9 Kuuza supu ya utumbo na makongoro

10 kuuza dawa za mbu na sumu ya panya

Hizi ni baadhi ya biashara za kijinga ambazo kijana hupaswi kuzifanya
 
kuna uzi nilikutag kuna mtu alikua anatafuta fundi ujenzi je uliuona?
 
Back
Top Bottom