Nimezipenda solution za January Makamba kiukweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimezipenda solution za January Makamba kiukweli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by howard, Mar 2, 2011.

 1. howard

  howard Senior Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  KAMATI ya Nishati na Madini imeamuru kuwashwa mara moja kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya Dowans ili kupunguza tatizo la mgawo wa umeme.
  Hatua hiyo ni kati ya maazimio na mapendekezo 30 yaliyofikiwa na kamati hiyo na huku ikisisitiza kuwa iwapo serikali itayatekeleza kwa haraka itasaidia kuiondoa nchi katika athari za kiuchumi.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika kwa muda wa siku 12, Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba (CCM), alisema kutokana na mitambo hiyo kuwepo nchini ni muhimu serikali iiwashe mara moja ili kuepukana na matatizo ya kiuchumi.
  Alisema mapendekezo yaliyotolewa ni yale ya dharura, ya kati na ya muda mrefu ambapo katika moja ya mapendekezo ya dharura, kamati hiyo inataka kupunguzwe megawati 125 zinazotumika katika migodi 4 ya madini ili umeme huo uelekezwe kwa matumizi ya wananchi.
  Makamba alisema migodi hiyo haijawahi kuathiriwa na tatizo la umeme hivyo kwa sasa inatakiwa ipunguziwe megawatts 50 na kusisitiza kuwa hatua hiyo inaweza kufanyika hata sasa.
  “Katika migodi hiyo hawajawahi kujua wala kuonja makali ya mgawo hivyo serikali ikiamua kulitekeleza hilo linawezekana hata leo hili megawat hizo zikafidie maeneo yenye mapungufu,” alisema.
  Alisema mbali na hiyo pia serikali inatakiwa kuhakikisha inatoa mafuta ya kutosha katika mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL ambapo hadi sasa inazalisha kati ya megawat 10 hadi 50 huku ikiwa na uwezo wa kuzalisha megawat zaidi ya 80 hadi 90.
  Alieleza kuwa iwapo serikali itashindwa kutekeleza mapendekezo hayo kuna uwezekano wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kupoteza kiasi cha sh bilioni 840 iwapo mgawo huo utaendelea katika kipindi cha mwaka huu.
  Alisema mapato ya taifa yamepungua kwa asilimia tano ya pato la taifa ambayo ni sawa na dola bilioni 1.1.
  “Mapendekezo na maazimio tuliyotoa ni yale ya kati, dharura na ya muda mrefu na iwapo serikali itatekeleza mapendekezo hayo basi tatizo la umeme litaisha katika kipindi cha wiki moja,” alieleza.
  SOURCE:TANZANIA DAIMA
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hmmmmmm! solution indeed?
   
 3. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Big up January na kamati yako. Tunataka watu wanaokuja na solution siyo kila sike ahadi tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu. Sick & tired
   
 4. M

  Mutu JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wayosi mapendekezo,basi Nyie Tanesco washeni mitambo ya Dowans muone?

  Msikilizeni Jaji Mushi

  Huyo January ni mtego the issue is well calculated ...shit
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Jamani.. hakuna mtu au chombo kinachoweza kutangaza "dharura" nchini isipokuwa Rais. Kamati ya Bunge haina madaraka hayo na hili tulimkatalia Waziri Mkuu Lowassa alipoingilia kati suala hili hili kwa kudai "dharura". Mengine wanaweza kuyatoa mapendekezo lakini la kutuambia hatua ichukuliwe kwa sababu ni 'dharura' haina hoja. Haijawahi kutangazwa wakati wowote na Rais kuwa Tanzania iko katika dharura kiasi cha kulazimisha kupindisha sheria au kuchukua "extra ordinary" measures.
   
 6. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,526
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Ndicho wanachotaka kutuaminisha kuwa kuna dharura inayohitaji kushughulikiwa.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  dharura ya miaka sita ni dharura gani hiyo?
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,
  Umesahau Misri ilikuwa na utawala wa dharura kwa miaka 30?
   
 9. T

  T.K JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 345
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kazi ya kamati ya bunge ni kushauri au au kutoa kuamrisha serikali?
   
 10. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hivi kamati za bunge zina mamlaka makubwa namna hiyo....mbona kamati nyingine hatuzisikii au hazijapewa meno kama hii ambayo mwenyekiti wake anaonekana kuwa na sauti hata ya kumzidi waziri wa wizara husika. Au mwenyekiti wa kamati ya bunge yuko juu kimaamuzi zaidi ya waziri? Confusing!
   
 11. n

  niweze JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inaonyesha kweli nyie wachache humu JF na nchini kwetu hamjui "uchumi" wala kitu kinaitwa "solution" kamati wanakaa siku 12 kuzungumzia jinsi ya kupunguza megawatts za migodini na kuongeza uzalishaji IPTL kama solutions kwa depth ya tatizo la umeme nchini Tanzania. Kwani Tanesco hawajagundua migodi haiitaji hizo megawatts au kuongeza fedha za mafuta? Kazi ya mkurugenzi wa Tanesco ni nini? au Hii kazi kapewa January pia. Mpaka sasa tunaona wananchi wanaoipenda Tanzania wanapinga Dawans ndani ya Tanesco, they don't want to hear this word anymore. Ufahamu wako wa jambo la umeme katika nchi linaonekana ni finyu sana na mnadanganywa au hamjui la kufanya au ni just political claps. Unajua Tanzania tunahitaji megawatts ngapi kuendesha viwanda mkoa wa Moshi peke yake? Unafahamu megawatts ngapi zinahitajika kuendesha hospitali za mkoa wa Dar? Itakuwa vizuri sana kama hiyo kamati fake ya January wangekuwa wanakutana public ili dialog na wananchi wanaojua in deep solutions za umeme.

  Tanzania mpaka leo hii inahitaji at least 800megawatts kucover mahitaji ya wananchi na Taifa zima. Tangu hiki chama kinachojiita ccm waingie madarakani uzalishaji wa umeme umepungua kutoka karibu 300megawatt mpaka kiasi cha kusikitisha maybe 150megawatts. Ufisadi na wizi Tanesco ambako kulitakiwa kusimamia utunzaji wa mabwawa (dams) na kufanya estimates ya uzalishaji wa umeme kupitia mito. Badala yake tangu Nyerere alipojiuzuru na kumwachia Mwinyi, ufisadi ukaingia na Shirika la Umeme Tanzania, Tanesco likageuka kuwa mradi wa ccm na mafisadi wakati wa Mkapa na sasa msanii. Hakuna Mtanzania leo hii hajui haya. Tanesco pamoja na makumpuni mengi ya serikali yakafanyiwa miradi na kukaingizwa something called "contracts", "joint ventures" and "privatization" Huu ndio usingizi Watanzania wamekuwa wamelala na sasa wengi wameamka na taking responsibility kulinda raslimali za Taifa.

  Baada ya baba yake kumtafutia mtoto wake January kazi ili waendelee kuwatawala Watanzania, tunamwona mpotofu mwingine January akijifanya anafanya kazi wakati malengo ni kulinda deals za Rostam na mafisadi wengine ndani ya raslimali za Watanzania. Tangu January aingizwa na Makinda kwenye kamati ya nishati na madini tunaona wazi lengo kubwa ni kumlinda Rostam na deals zake na kuhakikisha kwamba Dowans inalipwa na zaidi kuendeleza kulinda siri za vyanzo vya kuharibika kwa Tanesco. Kwanini January asishirikiane na Chadema kuanzisha mjadala Richmond na Dowans ziliingiaje Tanesco na Tanzania? Kwanini January asichunguze hadharani nani mmiliki wa migodi ya Tanzania? This will be a good direction.

  Solutions za janga la Umeme Tanzania ni kama ifuatavyo. Kama kweli tunataka kutatua hili swala ni kuleta kwanza "Transparency" na kuvunja kabisa Tanesco na kuunda chombo chenye mwelekeo wa kutatua Matatizo ya umeme. Wananchi wenye professional za engeering na economy waangalie estimates and conducting researches on the real energy capabilities of our country. Vitu vingine ni jinsi ya kufanya energy investments kwa ajili ya long-term solution. Hizi solutions za January, Rostam na Kikwete ni majanga makubwa sio solutions, wanachokifanya ni kufungua milango ya kuibia Taifa letu hakuna jipya hapa.

  Sisi kama Watanzania tuangalie pembeni na kusonga mbele kubadilisha hii serikali ya Kikwete na ccm. Mapinduzi yameshaanza na tunamaliza kazi siku chache zimebaki kwa hiyo January na Kikwete jiandeani kuishi kwa mlo mmoja kama Watanzania mnao watesa.​
   
 12. S

  Selemani JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Acha kukurupuka. Kamati imetoa mapendekezo kibao. Na kama umesoma hiyo article kuna mapendekezo ya sasa, kati, na muda mrefu. ie long term plan. Article ya Tanzania Daima imeweka only one pendekezo which is a short term. Subiri hapa hapa, in one day or two, InshaAllah---u will read the whole kamati report then utoe dukuduku lako. And I guarantee you, those are solutions to fix umeme.

  Muulizeni Mnyika, yeye alikuwemo kwenye hivyo vikao.
   
 13. n

  niweze JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mnyika alikubaliana na hayo ma-upupu ya Kamati? What are Tanesco and management responsibilities? Do your researches and stop bow down to empty ideas. I didn't hear anything from your brain yet. My grand parents listen to people like you and you guys killed them.
   
 14. S

  Selemani JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  And u listen to Mbowe, Regia Mtema, Slaa, Sugu, Lema??

  Mnyika ni member wa kamati na kamati haiwezi kutoa recommendations without a consensus. Haya ni matakwa ya Kamati sio January Makamba. Maybe ya can't hear me because you are unwilling to listen and your idolatry to Chadema is probably plugging your masikio.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Kwanini huko nyuma makampuni ya madini hayajawahi kukatiwa umeme wakati wa Tanzania wamekuwa wakipata adha hii miaka nenda rudi?
   
 16. S

  Selemani JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  I wish I knew kaka
   
 17. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 521
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa mawazo yangu, hii itakuwa a good transition toward debt payment! Tanasco iwashe mitambo, hapo hapo isilipe hilo deni la bil.94shs. au wakatae kuinunua hiyo mitambo kwa bei atakayotaka muuzaji, itaingia akilini kweli??
   
 18. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,954
  Likes Received: 2,096
  Trophy Points: 280
  Crap!! Sasa wale wa migodi wakipunguziwa umeme ndio watazalisha zaidi? Na serikali itatoa wapi pesa ya kuongeza mafuta kwa IPTL? Hivi ni kweli wananchi wanaweza kuzalisha na kufikia kupata kuokoa TSH 840 bil. au ni mafisadi ambayo yana misamaha ya kodi lukuki?
   
 19. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa mara ya kwanza katika historia ya bunge letu, kamati hii ya Makamba ni ya utendaji. Wanatoa amri na kuingilia utendaji wa TANESCO na wizara halafu wanaonekana eti wako pragmatic. Mimi nakwambia mitambo ya Dowans ikishawashwa hutamsikia tena Makamba maana atakuwa amemaliza kazi aliyotumwa.
   
 20. Mr. Mwalu

  Mr. Mwalu JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 814
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
   
Loading...