ongeeni na mtoe bla bla zote kama watakuwa wamevunja kanuni za nchi kwa kuingilia madaraka ya tanesco au wizara watanzania hatutaki kujua tunachohitaji umeme. kama makampuni ya madini yatapunguziwa umeme ili sisi tuweze kuishi kama zamani kwetu ni neema hatutaki kujua kama makamba na kamati yake wameingilia madaraka ya raisi au ya waziri mkuuu tunachohitaji ni umeme procedure baadae period.
Howard si vyema ku-generalize issue. Ni kweli kwamba watanzania tunahitaji umeme iwe tumeshaunganishwa Tanesco au tunataraji kuunganishwa, lakini kusema kwamba hatujali huo umeme unakujaje hilo si kweli. Sio mara zote kwamba
the end justifies the means.
Ndani ya Tanesco kuna wazalendo wenye majibu ya matatizo ya umeme Tanzania tatizo hawapewi microphone na wanachoandika kutokana na tafiti mbalimbali kimejaa vumbi ndani ya makabati.
Kama mnakumbuka waziri Ngeleja alikuja bungeni na proposals (short, medium and long term). Sasa watuambie proposal za Makamba zimetokana na wataalam gani na zile za Ngeleja zilitokana na wataalam gani.
Tanesco limekuwa shamba la bibi kila mtu achuma anavyotaka.
January alipata kusema "tutaishauri serikali lakini ikikataa tutaishinikiza", yaweza kuwa ni kauli ya kizalendo lakini kwa kung'ang'ania Dowans kwa nini nisiamini M/Kiti wa kamati kabeba masilahi ya kundi la wabaka uchumi??
Hizi zote mie naziona ni sarakasi za kisiasa, sioni dhamira ya kweli ndani ya chama tawala na serikali kushughulikia tatizo la umeme. Tumekuwa taifa dhaifu lenye watu na viongozi dhaifu, ni waoga wa worst cases ndo maana tunatishwa tusipowasha mitambo ya dowans TRA watapoteza 840b lakini hawajawahi kusema TRA inapoteza bilioni ngapi kwa misamaha, rushwa, wizi n.k
Tunatishwa mahospitali yatakosa dawa wakati hatujui ni lini walisema yana dawa, na kama hali ni mbaya mbona wabunge wanapewa milioni 90 za kununua gari, mbona jet yetu inaruka kila leo mara uswisi, mauritania, congo, sasa iko paris.
Kama hali ni mbaya tuiche iwe mbaya to the very last point ili kila mwananchi ajue nani katufikisha hapa, maralia haitibiwi kwa panado hata siku moja. Proposal za kamati ni panado tu, huwezi mkajifungia ndani siku 12 mkaja na majibu ya umeme 2030 bila hata ya utafiti.
Dowans wakifanikiwa ama kuwasha mitambo yao ama kuiuza kwa serikali itakuwa ni ushindi kwa wabaka uchumi na fedheha kwa wazalendo. Binafsi niko tayari kusubiri majibu sahihi kuliko kupata raha ya kitambo huku utu wa mtanzania ukiendelea kufedeheshwa.
Cha msingi nunua tochi/taa za kichina ili kupunguza hatari ya mishumaa nyumbani kwako!