Nimewapiga wachawi—kipigo cha mbwa koko!

Hii ni habari ya kweli kabisa. Uongo mimi nauchukia kama ukoma.

Kama huamini kuna wachawi, sikiliza vizuri: Hivi majuzi, walikuja usiku, muda mfupi baada ya mimi kujilaza kitandani. Wakaanza kunikandamiza kwa nguvu sana. Mgandamizo ulikuwa mzito, utafikiri mtu ameweka juu yangu mifuko mitano yenye saruji. Sio mzaha, nakwambia.

Sijawahi kuhisi uzito huo kamwe. Haraka sana nilitambua ni wachawi wanaotumiwa na mapepo kujaribu kunidhuru. Nikaanza kuwakemea kwa Jina la Yesu - kwa sauti ndogo, lakini yenye mamlaka watoke na kuniachia. Instantly, waliniacha na mgandamizo ule ukatoweka. Jina la Yesu lina nguvu sana. Ukilitamka, wachawi wanapigwa kipigo kikali sana na kukimbia. Hii ni mojawapo ya faida za kuokoka. Unatembea kifua mbele bila kuogopa wachawi.

Yakobo 4:7-10
"Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili. Huzunikeni, na muomboleze, na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni. Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua."

Umesema ulitambua kwamba ni wachawi na mapepo, lakini Biblia yako haikupi msingi wa kusema kila mgandamizo wa usiku ni wachawi. Ulichopitia ni tukio lako binafsi, si ushahidi wa kwamba wachawi walikuwa hapo.

Na Yakobo 4:7 haisemi kwamba ukilitaja tu “Jina la Yesu” wachawi watapigwa na kukimbia. Inasema wazi: “Mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia.” Muktadha wake ni kumtii Mungu na kujinyenyekeza kwake, si kuthibitisha kwamba tukio lolote la usiku limesababishwa na wachawi.

Pia Biblia inasema: “Usishuhudie uongo juu ya jirani yako” (Kutoka 20:16). Kwa hiyo, kama huna ushahidi kwamba walikuwa wachawi, usidai kwa uhakika kwamba walikuwa wachawi.

Lete aya ya Biblia inayosema kwamba mtu akihisi amebanwa au kukandamizwa akiwa amelala, basi lazima ni wachawi waliotumwa na mapepo. Hapo ndipo hoja yako ithibitike kwa Biblia, si kwa uzoefu wako binafsi.
 
Lakini kama hujaokoka ukiwakemea wachawi au mapepo, hayatoki, sana sana yatakudhuru. Soma Matendo 19:13-16
"Baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwapo wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile wakiwa uchi na kujeruhiwa."

Lakini Matendo 19:13–16 haithibitishi unachodai. Aya yenyewe inasema hao watu walikuwa “wapunga pepo” waliokuwa wakilitumia jina la Yesu kama maneno ya uchawi: “Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.” Ndiyo maana pepo aliwajibu: “Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani?”

Hivyo tukio hilo linaonyesha kwamba jina la Yesu si hirizi au formula ya kichawi ambayo mtu analitamka tu ili kupata nguvu. Lakini hakuna mstari hapo unaosema: “Mtu asiyeokoka akiwakemea wachawi au mapepo, lazima atadhurika.”

Zaidi ya hapo, wewe ulidai kwamba uliokandamiza usiku ulikuwa wachawi waliotumwa na mapepo. Matendo 19:13–16 haisemi chochote kuhusu mtu kulala, kuhisi mgandamizo, kisha kuhitimisha kwamba ni wachawi.

Lete aya ya Biblia inayosema wazi kwamba mgandamizo wa mtu akiwa amelala ni ushahidi wa wachawi. Matendo 19:13–16 haiwezi kuthibitisha jambo ambalo yenyewe haisemi.
 
Yuko sahihi. Shida yako unacopy na kupaste uliyoandikiwa bila kuyatafakari na kuhakikisha ukweli wake. Kwani wapunga pepo ni watu waliookoka? Waliopewa amri ya kukemea pepo ni watu waliookoka tu
 
Mwambie asome Marko 10:1 kama hajui waliopewa mamlaka ya kukemea pepo ni kina nani.
 
Hilo halijajibu hoja yangu. Mimi sikuuliza kama wapunga pepo walikuwa wameokoka; nilisema Matendo 19:13–16 haisemi kwamba mgandamizo wa mtu akiwa amelala ni ushahidi wa wachawi au mapepo.

Ndiyo, Yesu aliwapa wafuasi wake mamlaka juu ya pepo, lakini hilo halimaanishi kila mtu anayepata mgandamizo usingizini amevamiwa na wachawi.

Kwa hiyo, usibadili mada. Lete aya ya Biblia inayosema wazi kwamba mtu akihisi mgandamizo akiwa amelala, huo ni ushahidi kwamba wachawi au mapepo wamemvamia. Kama hakuna aya hiyo, Matendo 19:13–16 haiwezi kutumika kuthibitisha dai hilo.
 
Wachawi ni maajenti wa shetani. Kumbuka waliyoyafanya wachawi mbele ya Farao.
Sasa Maandiko yanasema:
“Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.” (Luka 10:19)
Unaelewaje hilo andiko "nguvu zote"?

Andiko jingine linasema:
“Zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuzima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.”
Unaelewaje mishale yenye moto ya yule mwovu?

Isitoshe, shetani na maajenti wake(wachawi) wanafananishwa na wezi, ambao kazi yao ni kuiba uhai wetu, kuchinja na kuharibu. Ukigandamizwa kwa uzito ule unafikiri matokeo yake ni nini, kama sio kuchinjwa na kufa.
Yohana 10:10
Mwizi huja ili aibe, aue na aangamize.

Kama unatafuta aya au kifungu specific "kugandamizwa" utaendelea kuonewa na Ibilisi.

Mimi nimemaliza sina maelezo zaidi ya hayo
 
Hapo umeunganisha aya ambazo hazisemi unachodai.

Luka 10:19 inasema Yesu aliwapa wanafunzi mamlaka juu ya “nguvu zote za adui,” lakini haisemi kwamba kila hali ya kugandamizwa usingizini ni shambulio la wachawi.

Waefeso 6:16 inaposema “mishale yenye moto ya yule mwovu,” inatumia lugha ya mfano kuhusu mashambulizi ya kiroho; haisemi kwamba kila uzito unaohisiwa wakati wa usingizi ni mshale wa Shetani.

Na Yohana 10:10 inasema mwizi huja kuiba, kuchinja na kuangamiza, lakini Yesu hapo hamtaji mchawi wala hasemi kwamba kugandamizwa usingizini ni kuchinjwa na Shetani.

Kwa hiyo hoja yangu bado iko pale pale: Lete aya inayosema wazi kwamba mtu akigandamizwa akiwa amelala, basi ni mchawi au pepo anayemshambulia. Aya zinazozungumzia nguvu za Shetani hazithibitishi moja kwa moja kwamba kila tukio la kugandamizwa usingizini linasababishwa na wachawi.

Usichanganye “Biblia inafundisha kuwepo kwa Shetani na nguvu za uovu” na “kila tukio fulani la usingizini limesababishwa na Shetani.” Hayo ni madai mawili tofauti.
 
Luka 10:19 inasema Yesu aliwapa wanafunzi mamlaka juu ya “nguvu zote za adui,” lakini haisemi kwamba kila hali ya kugandamizwa usingizini ni shambulio la wachawi.
Usinilishe maneno, sijasema kila hali ya kugandamizwa usingizini ni shambulio la wachawi.
Nilichosema ni kwamba katika tukio hilo kugandamizwa kulikoma instantly baada ya kukemea kwa Jina la Yesu. Hiyo inasupport moja kwa moja Andiko la "Mpingeni shetani naye atakimbia"(Yakobo 4:7)

Kama unaamini haikuwa uchawi basi toa maelezo mbadala huo mgandamizo chanzo chake ni nini na kwa nini mgandamizo ulikoma papo hapo baada ya kukemewa.

NB: Unapotumia chatGPT kutafuta majibu, uwe unahoji kwanini imekupa majibu hayo, sio unacopy na kupaste tu kila unachoambiwa. Chini kwenye user interface imeandikwa: ChatGPT can make mistakes. Check important info.
 
Kukoma baada ya kukemea kwa jina la Yesu hakuthibitishi kwamba chanzo kilikuwa Shetani au uchawi. Hilo ni hitimisho lako tu. Yakobo 4:7 haisemi kwamba kila mgandamizo wa usingizi unatokana na Shetani. Lete andiko linalosema wazi hivyo, si tafsiri yako ya tukio.
 
Mwambie asome Marko 10:1 kama hajui waliopewa mamlaka ya kukemea pepo ni kina nani.

Marko 10:1 haisemi chochote kuhusu mamlaka ya kukemea pepo. Inazungumzia Yesu kwenda Yudea na watu kumfuata. Soma aya yenyewe kwanza kabla ya kuitumia kama ushahidi.
 
Uchawi haupo mkuu, ni imani yako na manifestation ya negative energy kumkichwa tu ndo inaleta yote hayo.
 
Marko 10:1 haisemi chochote kuhusu mamlaka ya kukemea pepo. Inazungumzia Yesu kwenda Yudea na watu kumfuata. Soma aya yenyewe kwanza kabla ya kuitumia kama ushahidi.
Typo.
Mathayo 10:1
Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa uwezo wa kuwafukuza pepo wachafu na kuponya magonjwa na maradhi yote.
 
Kukoma baada ya kukemea kwa jina la Yesu hakuthibitishi kwamba chanzo kilikuwa Shetani au uchawi. Hilo ni hitimisho lako tu. Yakobo 4:7 haisemi kwamba kila mgandamizo wa usingizi unatokana na Shetani. Lete andiko linalosema wazi hivyo, si tafsiri yako ya tukio.
Nimekwambia elezea mgandamizo ule ulisababishwa na nini na kwanini ulitoweka ghafla baada ya kuukemea, umeshindwa.
Ndio shida ya kutegemea chatGPT. Za kuambiwa changanya na zako. Bahati mbaya huwezi kuchanganya na zako kwakuwa huna ufahamu wa kisayansi kuhusu jambo hilo na wala huna ufahamu wa kiroho kuhusu nguvu za giza. Umebakia kupinga tu. Nakuombea, Mungu aondoe upofu uliofunika akili zako, nuru ya Kristo ikuangazie.
2 Wakorintho 4:4
Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu.
 
Ndo maana nikasema huyo Mungu ha exist physically ila spiritually na hatuwezi kusema ni physical kama Bible inavyosema
Soma vizuri Mathayo ujue kwanini Yesu aliitwa Mungu pamoja nasi (Mathayo 1:23)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom