Nimevunja ukimya lakini hola!

Nyakwaratony

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
573
140
Ni miaka minne (4) sasa tangu nimefahamiana na mkaka mmoja. Tulifahamiana wakati ninasoma course flani "c mnajua tena mambo ya kujiendeleza ukubwani" yeye alikuwa mwalimu wangu na ananizidi miaka minne (4). Wakati nasoma sikuwa na feelingsd naye kabisa cos nilumuheshimu kama mwalimu wangu pia nahisi na yeye alikuwa vivyo hivo. Basi sasa baada ya mimi kumaliza hiyo course nilihamia mkoani yeye akabaki Bongo hapo ndipo tulianza mawasiliano kwa muda mrefu na pia tukaanza kuoneshana feelings baina yetu ingawa yeye hakuwa wazi sana. Nilijikuwa nazidiwa ikabidi nimueleze juu ya hisia zangu ila kwa kweli alisita sana na kuwa na wasiwasi "oh yan mimi masikini sina kitu, nitapendwaje ma mtoto mrembo kama wewe" na vitu kama hivo yan hakuwa na uhakika kama ninampenda kiasi hiko.

Kiukwei mimi ninampenda saaaaaaaaana toka moyoni natamani hata angenitamkia kuwa njoo hata sasa hivi tulisukume gurudumu la maisha nisingesita cos ni mtulivu, mpole asiye na makuu. Nimekuwa nikipigia mara kwa mara kuliko yye anavonipigia, ninamtext sms nzrui za kimapenzi ila yeye anakuwa mzito sana. Hata zawadi nimekuwa nikimtumia wakati mwingine lakini yeye hola. hata vocha jamani. Ila kuoana kwetu ni mara moja au mbili kwa mwaka.

NOTE: Cjaahi kukutana naye kimapenzi. Sasas nimechoka cos naona naumiza roho yangu bure, nimeamua kuacha kuwasiliana naye mara kwa mara. Sasa hivi nina kama cku 5 cjawasiliana naye na yeye pia kakaa kimya.. Nimeamua uamuzi huo lakini naona nauma pia. Je wanajamvi niendelee kumsumbua, ama nitumie njia gani. Plz........ :shock:
 
Una uhakika kuwa hana mke wa watoto nyumbani?

Na kipindi hiki cha sikukuu huenda anaogopa utamdai full-tank, wakati anajua watoto wanataka nguo mpya, na januari ndo kuna ile sikukuu kubwa sana ya kulipia ada za shule!

Wanaume wengi muda kama huu wamewakaukia wale wachumba wao 30, wanajikita kwenye mambo ya familia, maana hayana option!
Msubiri huenda baada ya hizi sikuku ataonekana!
 
Hilo nalo neno PJ.
Mrembo, huyo jamaa ungekubali tu hali. Manake huko mbeleni atakuja kukutesa manake wewe sio chaguo lake. Dawa chungu pia inaponyesha. Get a life, keep busy na tafuta hobby mpya. Asikufungie baraka za mbinguni!
 
Usife moyo some things need time,kuwa mvumilivu japokuwa jamaa anaonekana hajiamini,endeleza mawasilino na mpe moyo na mtoe wasiwasi!
 
Umesha fanya la maana kupiga kimya. sasa endelea na maisha kama kawaida.
 
Ungekuwa karibu yangu ningekusaidia; hapa kuna kuku wengi si sehemu sahihi pa kumwaga mtama. Jaribu kunitafuta nitakushauri na utampata tu kama kweli wampenda. Kama ni kinyume tutaangalia la kufanya.
 
Miaka 4 bado tu asikate tamaa waendelee na chit_chat?! Kama ni mtoto angeshaanza na shule kabisaa!
Usife moyo some things need time,kuwa mvumilivu japokuwa jamaa anaonekana hajiamini,endeleza mawasilino na mpe moyo na mtoe wasiwasi!
 
Naam! Au kama hatumi vocha basi walau akulipie kodi ya pango, akununulie handbags, shoes, perfumes au basi walau ki-vekesheni bagamoyo kwa faida yake binafsi.
Hivi bongo mtu akikutumia vocha ndio anakupenda?Na asipokutumia hakupendi?
 
Kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa ana mahusiano na mtu mwingine na hataki kukuumiza roho..au hajakupenda kabisa,na angependa mbaki kuwa marafiki...Cha msingi mpendwa,kama mtaonana tena muelezee mkiwa uso kwa uso then utaona reaction yake...utajua kama muoga au hataki kabisa...Mapenzi sio ya kulazimisha kabisaaaaa,otherwise utajikuta unaangukia pua..
 
Kashindwa voda fasta ya 300, ije handbag?

Naam! Au kama hatumi vocha basi walau akulipie kodi ya pango, akununulie handbags, shoes, perfumes au basi walau ki-vekesheni bagamoyo kwa faida yake binafsi.
 
Back
Top Bottom