Nimevamiwa na kunguni

Nimevamiwa na kunguni

Hiyo Diazon nimejaribu haifanyi kazi
Siafu,sisimizi,viroboto,mchwa,kunguni na mengineyo.

Kizibo cha hiyo chupa kimoja changanya na maji lita kumi,nyunyuzia.

Baada ya dk 30 unipe mrejesho

Twiga Gramma 20,,,,TSH 60,000.
JPEG_20221225_131506_3095367848266533160.jpg
JPEG_20221225_131745_5589804357073132916.jpg
 
Nimevamiwa na jeshi la kunguni, naomba msaada nimejaribu dawa mbalimbali za kunguni bila mafanikio. Tafadhali naomba msaada ili niweze kupambana na jeshi hilo!
Tengeneza dawa hii kisha spray watakufa...

1. Chukua OMO/Sabuni ya unga ya 500..
2. Mafuta ya taa hata litre 1 au chupa ya soda 1 ile ya mil 500.
3. Chumvi robo inatosha.

Fanya huu mchanganyiko kwenye chombo kisafi kisha weka kwa chupa kubwa toboa mfuniko kisha wapulizie, kunguni akipatwa na tone la hii kitu anakauka papo hapo, nmetumia sana hii kipindi 2017 baada ya kurudi mapumziko home kwenye geto langu niliachaga dogo wa A-Level alileta hao wageni na washkaji zake uzuri nilkua nishapata hii elimu so nikawapa haki yao waliishaga mpaka naondoka kwenda kutafuta maisha mengine sikuwahi kuwaona....

Pia kuna dawa nyingine ilishapigwa marufuku na serikali ni dawa ya mazao ile hasa walikua wanaitumia kwenye kahawa kama sijakosea ni hatari kwa afya ya binadamu ila inaua kunguni hatari sana hawatarudi tena ila ndo ivo kuipata tena naskia ni tizi sana..

Naona wadau wengi wanakushauri usafi tu hawajui kunguni ni mdudu mjanja sana na anajua namna ya kujificha hata uwe msafi vipi unaweza panda dala dala na shati lako umenyoosha vizuri tu kunguni akatokeza kwenye ukosi anakimbilia kwenye mgongo wa nyuma kushuka kwa suruali watu wa uliosimama nao wakabaki kucheka tu..

NB: Maji ya moto pia ni kiboko yao unaweza mwagia chumba, vitu vyote vya samani, nguo n.k unapohisi wapo wataisha.. Wageni wengi tunaokaribisha ndani kwenye masofa baadhi huja na mbegu/kunguni kisha wanawaacha hapo kinachofata sote tunakijua wanazaliana kwa speed ya sauti...
 
Ni Kweli mkuu, lakini tunawapata sehemu mbali mbali, kwenye madaladala, ukipumzika tu kwenye bench kariakoo unae, kwenye boat wapo kwenye mabasi ya mkoa wapo, hawa jamaa wapo very bright ataingia kwenye nguo bila kukuuma akitafuta sehemu salama ili akipata kiburudisho awe anapumzika katika security salama au angle safe kwake,infact ni kamdudu kenye akili lakini kepesi kukiua,
NI kamdudu ambako kanakuuma huku kakichukua taadhari ya kukimbia kwa haraka mambo yatakapoharibika kikomandoo.
Hahaaa bora umewaelezea.. Kunguni hawaletwi na uchafu, unaenda kumsalimia mwana getoni kwake unaondoka nae hapo utasema umeambukizwa uchafu au uchafu hapo unakujaje? mmoja tu anatosha kukuletea balaa kwako..

Watafiti pia niliskia wanasema hawa wadudu wanavutiwa sana na black colors, ila hawapendi rangi ya kijani na mwanga, pia kwakua ni wepesi kuuliwa ndo maana ni more sensitive wana mbio sana...
 
Pole sana,waliwahi kuingia kwenye chumba changu,nilifua nguo zote nikachemsha maji na kumwagia chumba na kitanda baada ya hapo nikapiga dawa hiyo hapo chini mpaka kwenye godoro. Kasoro ya hii dawa ni harufu aise ni hatari hasa usipoanika godoro kwa muda mrefu
1671970672627322850250.jpg
 
Timia hii dawa. Ni powder fulan hv mwisho wa matatizo. Inaua kabisa hao askari
Infinix X65734.JPG.jpg
 
Utakua umechanganya sio Kunguni hao mkuu wanaokufa...
Miaka mingi imepita mkuu, ila hii situation nimekutana nayo mara 3. Mara mbili sijui walienda wapi ila mara 1 walipotea na walikufa kiasi waliobaki, na mwishowe wakaisha kabisa.
 
Miaka mingi imepita mkuu, ila hii situation nimekutana nayo mara 3. Mara mbili sijui walienda wapi ila mara 1 walipotea na walikufa kiasi waliobaki, na mwishowe wakaisha kabisa.
OK inawezekana walivamia maeneo yasio rafiki kwao...
 
Safisha nyumba nzima ,deki na maji ya moto ,vitanda ,magodoro toa nje anika juani.
Kama hujajua chimbo lao hao wadudu na katika huo usafi wa nyumba nzima hujasafisha chimbo lao basi inakuwa kazi bure, unakuta umesafisha chumba kizima na kila kitu ila usiku ukilala wazee hao kumbe wanakaa kwenye dali ukiweka chandarua wanashuka kitandani wanakusumbua asubuhi wanarudi juu.
 
Hahaaa bora umewaelezea.. Kunguni hawaletwi na uchafu, unaenda kumsalimia mwana getoni kwake unaondoka nae hapo utasema umeambukizwa uchafu au uchafu hapo unakujaje? mmoja tu anatosha kukuletea balaa kwako..

Watafiti pia niliskia wanasema hawa wadudu wanavutiwa sana na black colors, ila hawapendi rangi ya kijani na mwanga, pia kwakua ni wepesi kuuliwa ndo maana ni more sensitive wana mbio sana...
Yani huyo unaweza ukamdaka kwa mkono ila ukimuangalia ghafla keshakupotea ni wepesi sana na wana mbio.
 
Dawa ya hao ni sisimizi
Paka asali kiasi kwenye mbao za kitanda, sisimizi watafuata watashambulia hao kunguni pamoja Na mayai yake, hawatorudi tena, mmi nilkuwa nao ndani kila aina ya dawa nilitumia lakin hawakuisha, komesha ya hao viumbe ni sisimizi
 
Back
Top Bottom