macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 28,208
- 56,811
Kupigana na kunguni inatakiwa ujue makazi na mazalio yao kwanza. Kunguni wanapenda kujificha kwenye kuta zenye nyufa/matundu/upenyo, Kona za kitanda na ndani ya godoro na sehemu zozote zenye cracks na pia nguo, matandiko na hata viti na sofa. Kwa kifupi unatakiwa utoe vitu vyote nje, unyunyizie dawa na ndani na hasa kwenye kona na nyufa. Ikiwezekana mwaga maji ya moto mkali kwenye hizo sehemu baadae ndiyo upige dawa. Vitu ulivyotoa nje pia inabidi uvi-treat kwa dawa na nguo uzichemshe kama supu.Nimevamiwa na Jeshi la kunguni naomba msaada nimejaribu dawa mbalimbali za kunguni bila mafanikio tafadhali naomba msaada ili niweze kupambana na jeshi hilo!!.

