Nimetukanwa na mke wa jirani yangu!!!

Nimetukanwa na mke wa jirani yangu!!!

Analinda masilahi yake.... Haki yake kujikinga kabla ya maovu/mabaya kutokea !!
 
Kwa nini huyo mwanamke asiongee na mumewe aje kukufuata wewe?

Kama wake wenyewe ndio hawa, one can't even have a beer with buddies, marriage is overrated.

Sasa kama kamshindwa mume wake, anakulaumu wewe, wewe ukakata contact akaja rafiki mwingine napo atataka huyo mwingine asinywe bia na mumewe? Kama anataka mumewe asiwe na marafiki kwa nini asimwambie hivyo mumewe?

Unaweza kuivika dunia nzima zulia ili mguu wako ukikanyage ardhi, au unaweza kuvaa viatu tu.

Matatizo ya ndoa ni ya ndani, utatuzi uanzie ndani.

Tutasepa tu.

Karibia kila ndoa ina migongano flani kinachotofautiana ni aina ya migongano, lakini siyo busara kabisa migongano hiyo kumuhusisha mtu wa tatu
 
Kuna familia moja imejengea karibu kabisa na kwangu tokea wamehamia ni miezi minne na zaidi, Baba wa familia hii ni wa rika langu kabisa, siku chache baada ya kuhamia tulikutana kwenye Ibada ya Jumuia mtaa wa tatu, basi tukawa tunaongea kwa kutaniana akiniuliza wenyeji huwa mnanywea bia wapi? Mimi nikamshauri kwamba Wkend tutafutane akiwa anasikia hata mkewe.

From there onward inapotokea mmoja wetu amekaa sehemu anapata kinywaji tunashtuana na kama upo interested una-join au unapotezea na mara nyingi tumekuwa tukikutana baadhi ya Weekends au public holidays.

Majuzi nilikuwa na Business moja ya kumshirikisha, tukakubaliana tuonane Lunch time kwasababu wote tunafanya kazi mjini, Kutokana na mda wa Lunch kuwa tight kidogo tulishindwa kupata mda wa kuzungumza kwani kulikuwa na marafiki wengine ambao isingekuwa vema wasikie mambo yetu, hivyo tukakubaliana tukutane Jioni Bar moja ya karibu mtaani kwetu.

Mida ya saa moja na nusu usiku tukakutana na jamaa na tukaanza mazungumzo, tukiwa kati kati ya mazungumzo jamaa akawa busy sana na simu ya mkononi kwani alikuwa kila baada ya dakika chache ananyanyuka kwenda kuongea na simu alafu akirudi 'mudi' yake inabadirika, sikutaka kumuuliza maana niliamini ni mambo yake binafsi na ndomaana hakutaka nisikie anaongea nini.

Baadaye jamaa akazima simu yake, tukaendelea na mazungumzo huku tukipata Bia mbili tatu, ilipofika saa tatu na dakika kadhaa usiku nikapigiwa simu na namba ambayo sikuwa nimei-save, nikasikia sauti ya mdada lakini siku-notice ni nani, akajitambulisha kwamba yeye alikuwa ni mke wa Jamaa niliye naye Bar akaniuliza kama kweli nipo naye nikathibitisha hilo, Hapo ndipo alipoanza kunishambulia kwamba tokea nimefahamiana na mmewe, mmewe amekuwa akichelewa kurudi nyumbani, na ameanza tabia ya Umalaya, hivyo akaniasa niache kumfundisha mmewe Tabia zangu chafu za umalaya.

Nimeumia sana kwasababu hata siku moja huwezi ukamfundisha tabia mbaya mtu mzima mwenzako, labda na yeye awe tayari anatabia hizo, huo umalaya wangu sijui kaufahamia wapi kwasababu hatujawahi kufahamiana kabla ya wao kuhamia mtaani, japokuwa wife kasafiri mda mrefu nimejitahidi sana kujizuia na haya mambo, na mbaya zaidi wife akirudi akikuta sipo katika mahusiano mazuri na Mke wa jirani ata-draw picture gani? Nifanye nini ili tuendelee kuheshimiana na huu dada? Napata taabu kwasababu nikimueleza mmewe kwamba aangalie cha kufanya ili mkewe afute imani mbaya aliyo nayo juu yangu lakini jama ananiambia nimpuuze tu mkewe.

Mpotezee huyo mshamba, hajiamini huyo na jamaa yake.
 
achana naye huyo, ukijibizana yatakuwa mengine na utajuta kukaa mtaa huo.

Alafu sijawahi kubadirishana naye namba za simu sijui kazifuma wapi namba zangu
 
nadhani hapo cha kwanza kufanya ni kumshirikisha mkeo kilichotokea ili yatakapojiri ya kujiri awe muelewa,pili mpuuzie huyo wife wa jamaa na jamaa jaribu kuwa naye mbali kidogo au mpe kitu live bila chenga then mind mambo yako km wewe kwani b4 ulikuwa na wakina nani?? but pole sana unajua siri ya nyumba iko kwa ukuta wa master bed room

Kweli kuta zinaficha mambo mengi sana
 
Mvaa Tai, block namba ya huyo mama. Usimjibu chochote na kama ni mimi nongemuelezea mke wangu kabisa. Hana nidhamu kabisa, anawezaje kumconfront mume wa mwanamke mwenzie?

Sijui alipata wapi ujasiri, huwezi amini mda woote aliokuwa ananitukana nilishikwa na butwaa tu
 
Alafu sijawahi kubadirishana naye namba za simu sijui kazifuma wapi namba zangu

atakuwa alikuwa anakufuatilia muda mrefu tangu umefahamiana na mumewe, huenda aliichukua kutoka simu ya mumewe.
 
Kuna familia moja imejengea karibu kabisa na kwangu tokea wamehamia ni miezi minne na zaidi, Baba wa familia hii ni wa rika langu kabisa, siku chache baada ya kuhamia tulikutana kwenye Ibada ya Jumuia mtaa wa tatu, basi tukawa tunaongea kwa kutaniana akiniuliza wenyeji huwa mnanywea bia wapi? Mimi nikamshauri kwamba Wkend tutafutane akiwa anasikia hata mkewe.

From there onward inapotokea mmoja wetu amekaa sehemu anapata kinywaji tunashtuana na kama upo interested una-join au unapotezea na mara nyingi tumekuwa tukikutana baadhi ya Weekends au public holidays.

Majuzi nilikuwa na Business moja ya kumshirikisha, tukakubaliana tuonane Lunch time kwasababu wote tunafanya kazi mjini, Kutokana na mda wa Lunch kuwa tight kidogo tulishindwa kupata mda wa kuzungumza kwani kulikuwa na marafiki wengine ambao isingekuwa vema wasikie mambo yetu, hivyo tukakubaliana tukutane Jioni Bar moja ya karibu mtaani kwetu.

Mida ya saa moja na nusu usiku tukakutana na jamaa na tukaanza mazungumzo, tukiwa kati kati ya mazungumzo jamaa akawa busy sana na simu ya mkononi kwani alikuwa kila baada ya dakika chache ananyanyuka kwenda kuongea na simu alafu akirudi 'mudi' yake inabadirika, sikutaka kumuuliza maana niliamini ni mambo yake binafsi na ndomaana hakutaka nisikie anaongea nini.

Baadaye jamaa akazima simu yake, tukaendelea na mazungumzo huku tukipata Bia mbili tatu, ilipofika saa tatu na dakika kadhaa usiku nikapigiwa simu na namba ambayo sikuwa nimei-save, nikasikia sauti ya mdada lakini siku-notice ni nani, akajitambulisha kwamba yeye alikuwa ni mke wa Jamaa niliye naye Bar akaniuliza kama kweli nipo naye nikathibitisha hilo, Hapo ndipo alipoanza kunishambulia kwamba tokea nimefahamiana na mmewe, mmewe amekuwa akichelewa kurudi nyumbani, na ameanza tabia ya Umalaya, hivyo akaniasa niache kumfundisha mmewe Tabia zangu chafu za umalaya.

Nimeumia sana kwasababu hata siku moja huwezi ukamfundisha tabia mbaya mtu mzima mwenzako, labda na yeye awe tayari anatabia hizo, huo umalaya wangu sijui kaufahamia wapi kwasababu hatujawahi kufahamiana kabla ya wao kuhamia mtaani, japokuwa wife kasafiri mda mrefu nimejitahidi sana kujizuia na haya mambo, na mbaya zaidi wife akirudi akikuta sipo katika mahusiano mazuri na Mke wa jirani ata-draw picture gani? Nifanye nini ili tuendelee kuheshimiana na huu dada? Napata taabu kwasababu nikimueleza mmewe kwamba aangalie cha kufanya ili mkewe afute imani mbaya aliyo nayo juu yangu lakini jama ananiambia nimpuuze tu mkewe.

Ni miezi minne tu. Huo ni muda mfupi sana kuwa concerned, na kutaka kuendelea kuheshimiana wakati hujaonyesha kama mnafahamiana vizuri kiasi gani?, baki ya kuhesimiana wote wawili hasa mwanamke. Halafu, umri kufanana siyo kufanana values. Jiulize mume wake alimpaje namba yako bila ridhaa yako.be careful, either mwanamme ana problems zake anataka kutokea kwako, au wanampango mmoja. Kwa nini akuambie umpuuze mke wake na ni yeye alimpa kontakti zako?
 
Katika maisha kuna mistari mtu hutakiwi kuvuka, huyo kavuka mstari usiomhusu, sana sana amejiaibisha tu..

Je angekuwa na mume kama dizaini za hawa wa kwetu anarudi home saa 8 za usiku angefanyaje? si angegombana na mtaa mzima na baa zote anazonywea huyo mume wangemkoma?

mmh mwanamke kama huyu hakawii kukutokelezea ofisini akamwambia boss mume wangu jana kachelewa kurudi home ...
 
Sijui alipata wapi ujasiri, huwezi amini mda woote aliokuwa ananitukana nilishikwa na butwaa tu

you can imagine huyo mume wake anaishi katika mazingira gani kama wewe tu mgeni asiyekujua anaweza kukutukana hivo!!!!! wanawake wengine bana tunajiharibia ndoa zetu wenyewe halafu mwisho wa siku tunamtafuta mchawi

huyo hana heshima wala adabu, yaani HAJAFUNZWA KWAO

hata kama ingekuwa ni kweli hayo anayosema kwa nini akupigie simu si angekuja kwako mkaongea vizuri ilikuwa na shida gani..
 
Kinachouma huyu ataendelea kuwa jirani yangu permanently, mbona maisha ya huku kununiana yatakuwa magumu sana?

halafu sasa cha kushangaza, atamnunia zaidi mke pindi atakaporudi nje ya nchi kama unavyosema, siku akija tu lazima amnunie..utafikiri yeye ndio kakutuma.. ndio ujue sisi wanawake wakati mwingine vichwa vyetu viko mbele dakika 3
 
yap kwanini uwai home? unaenda kupika au kufanya nini? why usijichanganye na wenzako mtaani kujua hata dunia inaendaje? kuna muda wa marafiki kuna muda wa home! kwani ukishaoa unacancel maisha mengine au na wengine kaka?

hahahah Smile hizi nasaha zako hizi...we haya tu....uliusoma uzi wa lara 1 kwanza kuhusu wanaume wa watu kurudi home majogoo?
 
Last edited by a moderator:
yap kwanini uwai home? unaenda kupika au kufanya nini? why usijichanganye na wenzako mtaani kujua hata dunia inaendaje? kuna muda wa marafiki kuna muda wa home! kwani ukishaoa unacancel maisha mengine au na wengine kaka?

hapo sasa ndo umefafanua vizuri mamii maana ujue kuna watoto wengne wenye watoto kama sisi unatamani uwe na muda na watoto wako ambao pengine uliondoka home bado wamelala sasa ni muhimu uwahi kujua maendeleo yao kwangu mimi ni bora kuliko kwenda bar!
 
Back
Top Bottom