Nimetukanwa na mke wa jirani yangu!!!

Hivi babu unajua dhana ya utii wa sheria bila shurti?


Hata hivyo, kwenye suala la kurudi nyumbani mapema mi halina mjadala. Na labda ndio maana nimeangukia kwa zombie simply because anarudi nyumbani mapema. Enzi zile yaani niko vacant, tabia ya kurudi mapema home likuwa moja ya kigezo, kwa nini? Kwa sababu najua ninakwazika sana na mtu kurudi sie tushakula. Maisha yenyewe ya kupikia mkaa sijui unaanza kuamka na kuchemsha ugali, utauchemshaje?

Siwezi kabisa, atanikuta nimekaukia kitandani kwa hasira.

That's my Kongosho in full swing....

Ila mama, hatuwezi kupata kila kitu tunachokitaka...ndiyo maana mwisho wa siku tunakubaliana na matokeo na kusonga mbele.....

Au wewe lazima Zombie atii mari zako 100%....?

Babu DC!!
 
mpuuzie kutokujiamini ndo kunamsumbua........ sasa mwanaume anawahi nyumbani ili afanye nini mwishowe aanze kukutuma maji ya kunywa loh.....! wakati we upo bussy na jiko mwanzo wakuanza kukerana hapo.....
Wanawake wengine hawajui kula na vipofu, anang'ang'ania awahi kurudi home, halafu akirudi anaanza kulalamika tena kuwa anamzonga, sasa sijui mtu afanyeje.
Mimi nawaasa wanawake wenzangu kuwa sisi wenyewe ndiyo tunapelekea kuitwa majina ya ajabu ajabu, kama vuvuzela, kamanda kova, mchiriku, na mangine mengi kutokana na mikelele yetu kwa waume zetu. Mpe mtu nafasi ili na yeye akupe nafasi, unambana kiasi ambacho anakosa view ya kutafuta pesa na ndipo anapoamua kulala na house girl , sasa sijui hapo utamlalamikia nani.
 
Wanawake wengine hawajui kula na vipofu, anang'ang'ania awahi kurudi home, halafu akirudi anaanza kulalamika tena kuwa anamzonga, sasa sijui mtu afanyeje.
Mimi nawaasa wanawake wenzangu kuwa sisi wenyewe ndiyo tunapelekea kuitwa majina ya ajabu ajabu, kama vuvuzela, kamanda kova, mchiriku, na mangine mengi kutokana na mikelele yetu kwa waume zetu. Mpe mtu nafasi ili na yeye akupe nafasi, unambana kiasi ambacho anakosa view ya kutafuta pesa na ndipo anapoamua kulala na house girl , sasa sijui hapo utamlalamikia nani.

hapo umenena dada !!!!!!!!!!!!
 
ha ha ha pole hizo ndio njia zake anatumia kukutongoza kuwa makini..huyo anakutaka
 
Kuna familia moja imejengea karibu kabisa na kwangu tokea wamehamia ni miezi minne na zaidi, Baba wa familia hii ni wa rika langu kabisa, siku chache baada ya kuhamia tulikutana kwenye Ibada ya Jumuia mtaa wa tatu, basi tukawa tunaongea kwa kutaniana akiniuliza wenyeji huwa mnanywea bia wapi? Mimi nikamshauri kwamba Wkend tutafutane akiwa anasikia hata mkewe.

From there onward inapotokea mmoja wetu amekaa sehemu anapata kinywaji tunashtuana na kama upo interested una-join au unapotezea na mara nyingi tumekuwa tukikutana baadhi ya Weekends au public holidays.

Majuzi nilikuwa na Business moja ya kumshirikisha, tukakubaliana tuonane Lunch time kwasababu wote tunafanya kazi mjini, Kutokana na mda wa Lunch kuwa tight kidogo tulishindwa kupata mda wa kuzungumza kwani kulikuwa na marafiki wengine ambao isingekuwa vema wasikie mambo yetu, hivyo tukakubaliana tukutane Jioni Bar moja ya karibu mtaani kwetu.

Mida ya saa moja na nusu usiku tukakutana na jamaa na tukaanza mazungumzo, tukiwa kati kati ya mazungumzo jamaa akawa busy sana na simu ya mkononi kwani alikuwa kila baada ya dakika chache ananyanyuka kwenda kuongea na simu alafu akirudi 'mudi' yake inabadirika, sikutaka kumuuliza maana niliamini ni mambo yake binafsi na ndomaana hakutaka nisikie anaongea nini.

Baadaye jamaa akazima simu yake, tukaendelea na mazungumzo huku tukipata Bia mbili tatu, ilipofika saa tatu na dakika kadhaa usiku nikapigiwa simu na namba ambayo sikuwa nimei-save, nikasikia sauti ya mdada lakini siku-notice ni nani, akajitambulisha kwamba yeye alikuwa ni mke wa Jamaa niliye naye Bar akaniuliza kama kweli nipo naye nikathibitisha hilo, Hapo ndipo alipoanza kunishambulia kwamba tokea nimefahamiana na mmewe, mmewe amekuwa akichelewa kurudi nyumbani, na ameanza tabia ya Umalaya, hivyo akaniasa niache kumfundisha mmewe Tabia zangu chafu za umalaya.

Nimeumia sana kwasababu hata siku moja huwezi ukamfundisha tabia mbaya mtu mzima mwenzako, labda na yeye awe tayari anatabia hizo, huo umalaya wangu sijui kaufahamia wapi kwasababu hatujawahi kufahamiana kabla ya wao kuhamia mtaani, japokuwa wife kasafiri mda mrefu nimejitahidi sana kujizuia na haya mambo, na mbaya zaidi wife akirudi akikuta sipo katika mahusiano mazuri na Mke wa jirani ata-draw picture gani? Nifanye nini ili tuendelee kuheshimiana na huu dada? Napata taabu kwasababu nikimueleza mmewe kwamba aangalie cha kufanya ili mkewe afute imani mbaya aliyo nayo juu yangu lakini jama ananiambia nimpuuze tu mkewe.

mpotezee kwakuwa hufanyi kweli hayo we muangalie tu ipo siku mwenyewe atapata jibu na kama ni mstaarabu atarudi kukuomba msamaha
 
Mkuu shughuri unayo, kwani hakuna kitu kibaya kama
kuishi na jirani mbaya,ulikumbuka kuweka loud speker
ili mumewe aweze kusikia?
 

kweli kajidhalilisha bureeee !!
mwny uamuzi wa kuwah nyumbani ni
mume wake,labda amfunge kamba huyo mume!!
 
Jinsi ulivyonitukana mimi kwenye pm leo hii, bila sababu yoyote, hunijuwi sikujuwi. Sioni ajabu ikiwa utatukanwa na jirani zako. Inaonesha u mtu wa aina gani.

Kanitukana hanijui simjui wala sijawahi ku pm nae wala kujibizana nae kwenye posts. Mimi mwenyewe nimeshangaa. Mara nakuta humu katukanwa na jirani yake. Sasa sijui hasira zake za kutukanwa akaona aje kuntolea mie? Majanga, kutukanwa atukanwe na mwingine matusi aje nilamba mimi.


Mambo yenu ya kutongozana kwa PMs msiyalete public si mnajua taratibu haziruhusu mambo ya PMs kuletwa Public?????
 
Mambo yenu ya kutongozana kwa PMs msiyalete public si mnajua taratibu haziruhusu mambo ya PMs kuletwa Public?????

Nimeandika mtu kanitukana wewe unasema "kutongozana", kichwa chako kipo sawa? wanaotongozana wanalalamika?

Hujui kuwa sifa ya mwanamke ni kutongozwa? au huna mama, dada wala mke/mume wewe nyumbani? kama unao, walishakuja kukulamikia hata siku moja kuwa wanatongozwa?

Au wewe ushalalamika unapotongozana?

Unashangaza!
 
Hata kama hupendi pika, mme akiwepo lazima utataka kumpikia tu.

Unaenda jikoni unapika pika, mara unakuja unamchungulia kuku wako mwenyewe tena kwa kunyata nyata. Hapo unapalilia apetaiti ya usiku, flirting ndogo ndogo. Asikwambie mtu, hata uhongwe Bombay hutakaa ufikirie kuchit.

Sijui hapo bado ni jioni jioni, mara umempitishia ka supu kepesi kepesi tu kumchangamsha, kama ni mpenzi kwa kahawa, unaiunga kahawa kwa nyanya. Kama ni mpenzi wa bia, kabia unakaleta hadi kanatoa jasho umekaunga na giligilani, poa tu hata aje na marafiki zake 100, wapige kelele za kushangilia mpira hamna shida. Tena hata nisivyowapenda Man U, kama ni timu yake nitaishangilia tu hata kama inacheza na Chelsea.

Mapenzi ni mchezo wa wakubwa, na raha wa kucheza naye anapokuwepo mcheze wote. Sasa unataka kucheza afu wa kucheza naye hataki ama hayupo, lazima utaenda kucheza kwa jirani tu.

cc Kaizer Asprin Babu Dark City
Sijafurahia jinsi unavyotoa siri za ndani. Nimehamia Liverpool kwa hasira. Shenzy zako na nusu Kongosho. Marahaba sana, na shikamoo nyingi.
 
Hivi babu unajua dhana ya utii wa sheria bila shurti?


Hata hivyo, kwenye suala la kurudi nyumbani mapema mi halina mjadala. Na labda ndio maana nimeangukia kwa zombie simply because anarudi nyumbani mapema. Enzi zile yaani niko vacant, tabia ya kurudi mapema home likuwa moja ya kigezo, kwa nini? Kwa sababu najua ninakwazika sana na mtu kurudi sie tushakula. Maisha yenyewe ya kupikia mkaa sijui unaanza kuamka na kuchemsha ugali, utauchemshaje?

Siwezi kabisa, atanikuta nimekaukia kitandani kwa hasira.
Ndio maana niliopt kukufanya nyumba ndogo badala ya kukufanya mke wa ndoa.... Yaaani, khaaaaaa!!
 
YAANI we unatukanwa na mwanamke halafu unaliweka moyoni hadi linakusumbua? potezea endelea na maisha yako hao ni viumbe dhaifu ukiwafuatilia kwa kila wanachokifanya au kukufanyia utaishia kuwa na wewe mdhaifu. msamehe bure.
 
Back
Top Bottom