Nimetoka kumuona Msela jela

Nimetoka kumuona Msela jela

Dumelang

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
3,273
Reaction score
5,926
Wimbo maarufu ulioimbwa na Mwanamziki Bushoke Jr.

"Nimetoka kumuona msela jela amenipa ukweli wa kesi yake, kaongea kwa uchungu huku analia watu wanaamini kesi yake".

Wengi tunaamini wimbo huu ulimuhusu Papii Kocha ambae inasemekana alikuwa Rafiki mkubwa sana wa Bushoke.

Jana magazeti kadhaa yaliandika sana kuhusu kesi hii na wafungwa hawa babu seya "Nguza Viking" na mwanae Papii Kocha au "Papii Nguza" ambapo wameendelea kutafuta haki zao kwa kuamini hawana hatia. Gazeti moja limeandika kuwa katika Maombi yao ya sasa wanalalama kuwa kesi ilikuwa ya kutunga.

Mimi napata wakati mugumu sana, maana huku uraiani watu tumegawanyika makundi mawili, wapo wanao amini hawa wafungwa wameonewa na tuhuma zao si za kweli wapo wanao amini wana hatia na hawafai kuwa uraiani.

Hata hapa JF ili linatokea kila mara linapokuja suala hili. Hisia hizi za mgawanyiko pia zilidhihirika siku CHADEMA wanazindua kampeni zao pale jangwani.

Wakati mgombea wa CHADEMA alipoahidi atamaliza kesi za mashekh wa Zanzibar mara atakapopewa Ridhaa ya kuwa Rais wa JMT, Umma ilipaza sauti na kumwambia "na Babu seya"..

Lowassa alijibu kwa Ufupi "nimewasikia".

Hoja yangu ni hii, kama Kweli P alimwambia ukweli rafiki yake Bushoke ukweli, na katika madai yao yaliotoka jana pia wanadai ni kesi ya kupakaziwa, kwanini wasiuambie na Umma ukweli huo?

Ukweli ambao utawaweka huru, kwanini sasa wasiuseme? Kwa miaka kumi waliomba huruma za Kikwete mara kadhaa, bila mafanikio, Kikwete kaondoka sasa wameona hali ni mbaya wenda, sasa wameamua kwenda tena kwingine kutafuta haki. Swali kwanini kwa mara nyingine tena?

Kwanini Papii na baba yake hawajawai kukubaliana na maamuzi ya mahakama yaliokwishafanywa mara tatu? Kwanini wamelilia sana huruma za Rais? Kwanini wameendelea kuamini walisingiziwa na kutafuta haki kila mara wakiamini wataipata?

Jamii imegawanyika, mahakama imebaki moja lakn ikiporomoa hukumu zake mara kadhaa.

'P', UKWELI ULIOMWAMBIA BUSHOKE UAMBIE NA UMMA SASA, LA SIVYO...ENDELEENI KUKAA NDANI.

Naomba kutoa hoja.....

NOTE:
Nami nakanganywa sana na ukweli wa kesi hii.
Nipo 50/50..
 
Hii kesi ukiangalia kiundani ina mizizi ya vigogo kuhusika
 
huwa nimeshindwa kuufahamu ukweli

hivi yule mama mwalimu aliyekuwa anawaunganisha wanafunzi na babu seya kama inavyosemekana alifungwa na yeye?
 
Hivi kwa katiba hii kuna ukomo wa kukata rufaa?Ahadi kama hizi zinatekelezeka hata ukishindwa urais kama kweli unadhamira.Hivi Edo aliahidi kuwatoa sababu ya umaarufu wao tu au sababu anaamini walibambikiwa kesi?
 
Kwani wale watoto miaka yote hii baadaye wanaweza kukumbuka hakuna hata mmoja au anayewafahamu humu JF na mwalimu yule kama ameshastaafu kwa sasa atakuwa anaabudu mahali fulani wanaweza kusema. Wanalalamika sana hao wakisema ukweli wa Mungu tutaona kama waongesewe adhabu wanyongwe kabisa au watoke na walipwe fidia
 
Hivi kwa katiba hii kuna ukomo wa kukata rufaa?Ahadi kama hizi zinatekelezeka hata ukishindwa urais kama kweli unadhamira.Hivi Edo aliahidi kuwatoa sababu ya umaarufu wao tu au sababu anaamini walibambikiwa kesi?

Lowasa hakusema atawatoa, lowasa aliujibu umma ulipopiga kelele "na babu seya" alijibu nimewasikia.

Jibu la lowasa pia linaacha udadisi.

Lakin swali la msingi kama walikutwa na kosa la kubaka, mwalimu aliepeleka watoto kubakwa kwanini aachiwe, naomba mnaokumbuka hii kesi mje mtuambie hapa nini kilitokea?
 
Kila mtu atasema lake lakini ukweli anaujua mwenyezi mungu na wahusika,ila kama wameonewa basi waliowaonea hawatotia kichwa kaburini bila kuonja adhabu kwakutendea wenzao mabaya.....
 
Hii tabia ya kutongoza tongoza ndio tujifunze tuache....starehe ya boss wako we ndio (malizia)
 
Hii tabia ya kutongoza tongoza ndio tujifunze tuache....starehe ya boss wako we ndio (malizia)

Kumbe mwenzetu we unajua chanzo chake hebu mwagika. Ikiwezekana kwa kuwa jamaa wanakata rufaa hebu fanya msaada wa USHAHIDI
 
huwa nimeshindwa kuufahamu ukweli

hivi yule mama mwalimu aliyekuwa anawaunganisha wanafunzi na babu seya kama inavyosemekana alifungwa na yeye?

Alikuwa anawaunganisha kwa minajiri ipi??yaani analipwa pesa au kivpi...sijaielewa
Hali ya kawaida mmama tena mwalimu awaunganishe vitoto vya 6yrs_8yrs kubakwa....
Nielekeze my dia ...
 
Back
Top Bottom