Nimetapeliwa pesa, naombeni ushauri

Nimetapeliwa pesa, naombeni ushauri

Imani imetoweka..

Huyo mfungulie kesi rasmi ..ongea na mkubwa kituoni hapo..utalipwa..
 
Kwanza shikamoo mzee mpili

Itikia salamu Kwanza nitakushonea baadae
 
Pole sanaa bro ila kifupi binafsi ""SIJAWAHI AMINI MTU KWENYE PESA""
linapokuja swala la pesa SINA NDUGU Wala RAFIKI ninae mwamini.

Ila pole, nadhani ni wakati wa kwenda mahakamani.

#YNWA
 
Mtumie picha ya mkungu wa ndizi zinazoanza kuiva, halafu mwambie upo kwa babu...
 
Wewe ulifungua kesi ya madai ndio maana mkaandikishana. Sasa nakushauri nenda tena polisi, wafungue jalada la wizi wa kuaminiwa. Hii ni jinai na atakamatwa kama mtenda jinai. Wakimuweka ndani atatafuta pesa zako akulipe ili yaishe
 
Kuelekea mwishoni mwa mwaka 2019 nilikuwa na kazi ya miezi mitano mkoani Kigoma. Nikiwa huko nilikutana na classmate na roommate wa chuo niliyesoma naye miaka ya nyuma DIT.

Tulipiga stori za hapa na pale, tukazoeana kiasi. Akajitambulisha kuwa anafanya kazi kwenye shirika la misaada, na pia anajishughulisha na kuagiza magari. Tulivyoendelea kukutana na kuzoeana tulizidi kufahamiana. Bahati mbaya nilijikuta nimefunguka kuwa nilikuwa ninapanga kununua gari.

Tulivyokuwa tunaendelea kuonana, jamaa alianza kunionyesha mawasiliano na kampuni za kuagiza magari, na kuniaminisha kuwa tunaweza ku-save hela kama ataagiza gari yeye, kisha gari likifika atanikabidhi.

Alinishawishi kuwa nimpatie kile kiasi cha kulipia nje huko, millioni 13. Kwa kumwamini, nilimwekea kwenye akaunti yake ya benki. Nikabaki na bank slip.

Ulipofika wakati wa gari kufika, jamaa alianza hadithi. Mwanzo alidai nimpe muda atoe gari, kisha atanipatia tumalizane. Zikapita zaidi ya wiki. Baadae akasema kuna mtu amelipenda, ananunua kwa bei nzuri, tuagize lingine. Akadai amesafiri, anarudi tutaonana.

Nilipoona anazunguka kinyume na makubaliano nikampeleka polisi. Afande niliyemkuta akampigia simu, jamaa akafika, akakubali kuwa ameuza gari ananirudishia pesa yangu na nyongeza. Tukaandikishana nikatulia.

Baada ya hapo, mpaka leo imekuwa ni mwendo wa kuzungushana kila mahali, na pesa sijapata. Kila akipigiwa simu anadai amepata majanga, mara vifo, nk.

Hajalipa pesa zangu.

Naombeni ushauri namna bora ya ku-deal na mtu wa aina hii.

Natanguliza shukrani za dhati.
Uko tayari kumfanya awe wa baridi kabisa?
 
Bora hiyo pesa yako ungepata mbususu mubashara hata ya kizungu,kiarabu angeikamua kiroho safi.
 
Fanya uchunguzi wa kina kujua mali anazomiliki.... Tafuta Askari 2 watata wapoze, ahidi hata 1mill wakifanikisha pesa kurudi ikibidi wape bonus ya pesa nusu za usumbufu kama watafanikisha hilo pia.....

Ingia kazini vaa roho ya fisi pita na chochote kilicho chake hata katikati ya mazishi
 
Hizo hela sijui huwa mnaziokota, yaani so simple unampa 13m,
Tena hukooo ingekuwa dar na wewe wangekuuza
 
Mkuu huyo jamaa deal naye TRADITIONALLY otherwise utapoteza muda wako tuu
 
Pole mkuu. Ni wazi huyo rafiki yako Ni tapeli na acha kusikiliza hizo excuse zake. Wewe Rudi polise chonga nao Kama vipi wapooze hao Askari, akamatwe atiwe ndani asitoke.

Usitake maelezo zaidi ya pesa, kama anamali aweke dhamana zipigwe Bei upate Chako.
Police wanadili na kesi za jinai na siyo madai aende akafungue kesi mahakamani moja kwa moja ili asipoteze pesa zaidi
 
Back
Top Bottom