Nimetapeliwa na mbeba mizigo

Nimetapeliwa na mbeba mizigo

Kwanza nikupe pole!

Pili, naomba nikupe pole tena...

Tatu, pole sana kaka!

Ni hayo tu!
 
Ilikuwaje hukuchukua risiti........?.......dah.......kweli mjini shule...........
 
Ndio maana watu wanamwagiwa tindikali hivi hivi.
 
kuna mdau kakushauri fresh. piga picha na ilete humu, pia kwenye post yako ungetaja jina la duka na location. pia hii inaweza kuwa stori nzuri kwenye magazeti ya udaku.
 
Baada ya kuzichanga kwa muda wa miezi mitatu hatimae nilifanikiwa kununua godolo langu la 6x6 chapa ya banko, kutokana na kuwa bize sana nilimtafuta mbeba kago nikamwelekeza nyumbani kisha nikaenda nae dukani na kumlipa muuza duka kiasi kilichosalia na kumuachia maagizo muuzaji akiwa tayari atampatia huyo mbeba kago mi nawahi mzigoni. Nafika nyumbani kama majira ya saa 2 nakuta hola nawauliza majirani hakuna mtu yoyote aliekuja hapo nyumbani. Nilimsalamba mpaka nikampata tukaenda polisi katika mahojiano akadai nitakuwa nimemfananisha tu kwani nae amenunua kama hilo hilo na jina na saini vinaonyesha ni lake nikamwendea mwenye duka akatoe maelezo ya kuthibisha kuwa lile godolo ni langu akagoma kunipa ushirikiano, sijui walikula njama pamoja.
Polisi wamesema hilo suala liko nje ya uwezo wao na hawawezi kumshurutisha mtu atoe wakati risiti inaonyesha huyo jamaa ndie mmiliki halali wa hilo godolo na hata wakiipeleka mahakamani uwezo wa kushinda haupo.

So inaniuma sana kudhulumiwa mali yangu huku naona na sijui nifanyeje? Japo nataka nijaribu kwa waganga wa jadi ingawaje sina uzoefu nao. Kwa hapa Dar nasikia wengi matapeli ila s/wanga inawezekana nikipiga mahesabu ya nauli, malazi na chakula ndo nachoka kabisa japo ni haki yangu. Mimi si islamic albadil inaweza saidia?
Wenye uzoefu na hayo makitu jamani naomba msaada wenu tafadhari

pole saana kaka,dunia tambala bovu
 
Chunguza kwa makini yawezekana Huyo mwenye DUKA na mbeba kago ni ukoo wa panya
 
Chunguza kwa makini yawezekana Huyo mwenye DUKA na mbeba kago ni ukoo wa panya

naisi hivyo mkubwa, sababu wakati nampelekea kidogo kidogo alinikisha jina, iweje ashindwe kunipa ushirikiano? Akidai its none of my biznès
 
Hii kzai ndogo.
Kama ni muunini na unataka kuwasaidia wenzio basi fanya hivi.
Kwanza Jua kama huo mchezo hautakuwa umeanzia kwako,inawezekana ni issue ya muda kwa wateja wao.

Nenda Kapige picha ya Duka hilo uilete humu.
Ili uwe umesaidia wengi,lakini kulalamika tu itakuwa haisaidii kitu na inaweza kuwa ni story Fake.

Tunasubiria Picha ya Duka husika

Kabisaaa, hana chake hapo na hamna cha kufanya kulipata godoro lake. Cha msingi sasa kufanya ni kuwaaibisha tu hao wezi. Ila asije vuka mstari sheria ikamkwida.
 
Mwenye duka hana kosa,mbeba kago ulimpeleka wewe sasa yeye mwenye duka afanyeje,ulitakiwa uchukue risiti na pia huyo mbeba kago ulitakuwa uchukue unayemfahamu au ungeenda nae!.Pole sana!
 
Sipati picha, mtu umetoka mihangaikoni na matumaini ya kulala usingizi mnono na wakati mwingine umeongozana na kisindikizio halafu unafika room fungua mlango, "kuko kama ulivyokuacha"
 
Si wabeba mizigo tu, binadamu wote siku hizi hawaaminiki. Kuwa makini, kama unaweza samehe, nunua godoro jingine maisha yaendelee.
majukumu ndugu yangu, ila nimeamin wabeba mizigo wengi ni wezi hiyo kazi ni kuzugia tu
 
Kama nitafute twende kwa mpemba mmoja hivi mtaalam- Jamaa atalileta godoro lako wakiambatana na huyo muuza duka wakikubembeleza ulichukue kwani ni mali yako.
 
Kwani we upo wapi nikusaidie mjukuu wangu mi ndo babu kutoka sumbawanga
Nichec inbox natibu mali iliyo potea ,mapenzi,nauza majini pamoja na vifaru ,siasa nguvu za kiume na n.k

babu mimi nisaidie ya mapenzi mjukuu wako mapenzi yananitesa
 
Back
Top Bottom