Nimetapeliwa na mbeba mizigo

Nimetapeliwa na mbeba mizigo

yutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2013
Posts
1,778
Reaction score
1,222
Baada ya kuzichanga kwa muda wa miezi mitatu hatimae nilifanikiwa kununua godolo langu la 6x6 chapa ya banko, kutokana na kuwa bize sana nilimtafuta mbeba kago nikamwelekeza nyumbani kisha nikaenda nae dukani na kumlipa muuza duka kiasi kilichosalia na kumuachia maagizo muuzaji akiwa tayari atampatia huyo mbeba kago mi nawahi mzigoni. Nafika nyumbani kama majira ya saa 2 nakuta hola nawauliza majirani hakuna mtu yoyote aliekuja hapo nyumbani. Nilimsalamba mpaka nikampata tukaenda polisi katika mahojiano akadai nitakuwa nimemfananisha tu kwani nae amenunua kama hilo hilo na jina na saini vinaonyesha ni lake nikamwendea mwenye duka akatoe maelezo ya kuthibisha kuwa lile godolo ni langu akagoma kunipa ushirikiano, sijui walikula njama pamoja.
Polisi wamesema hilo suala liko nje ya uwezo wao na hawawezi kumshurutisha mtu atoe wakati risiti inaonyesha huyo jamaa ndie mmiliki halali wa hilo godolo na hata wakiipeleka mahakamani uwezo wa kushinda haupo.

So inaniuma sana kudhulumiwa mali yangu huku naona na sijui nifanyeje? Japo nataka nijaribu kwa waganga wa jadi ingawaje sina uzoefu nao. Kwa hapa Dar nasikia wengi matapeli ila s/wanga inawezekana nikipiga mahesabu ya nauli, malazi na chakula ndo nachoka kabisa japo ni haki yangu. Mimi si islamic albadil inaweza saidia?
Wenye uzoefu na hayo makitu jamani naomba msaada wenu tafadhari
 
Pole saana ila Ubosi umekuponza. Ulishindwa nini kufuatana nao.
 
Kwani we upo wapi nikusaidie mjukuu wangu mi ndo babu kutoka sumbawanga
Nichec inbox natibu mali iliyo potea ,mapenzi,nauza majini pamoja na vifaru ,siasa nguvu za kiume na n.k
 
achana nae ndugu hayo mambo yapo tu kikubwA binadamu wana pande mbili usiwaamini sana
 
Aliyekutapeli ni muuzaji siyo mbebaji!

Komaa naye mwanzo mwisho
 
Chukuwa kijiko chimba kashimo kwa kutumia kijiko chukuwa kitambaa cheusi fukia chini kanyanga utasikia mshindo utakuwa umemaliza kazi yake huku unanuwia
 
Cunauhakika hy pesa umepata kiuhalali kama hujapta kiuhalali utaondoka wewe
 
Hii kzai ndogo.
Kama ni muunini na unataka kuwasaidia wenzio basi fanya hivi.
Kwanza Jua kama huo mchezo hautakuwa umeanzia kwako,inawezekana ni issue ya muda kwa wateja wao.

Nenda Kapige picha ya Duka hilo uilete humu.
Ili uwe umesaidia wengi,lakini kulalamika tu itakuwa haisaidii kitu na inaweza kuwa ni story Fake.

Tunasubiria Picha ya Duka husika
 
Mazingira ya kutapeliwa uliyajenga mwenyewe na hilo litakuwa funzo kwako daima...

Btw pole sana...
 
Na hasira na SITA mamaaaakeza...nipishe nipite.
Mkuu usije ukatuua bure!! Sasa Li-Sitta tutalifanyaje limeshatuumiza!! Bora tu umpe ushauri huyu mdau maana kashusha mahesabu ya kwenda S/wanga, gharama yake inanunua godoro moja na nusu! Sasa si bora asamehe tu ili ajichange upya??
 
Pole saana ila Ubosi umekuponza. Ulishindwa nini kufuatana nao.

majukumu ndugu yangu, ila nimeamin wabeba mizigo wengi ni wezi hiyo kazi ni kuzugia tu
 
Kwani we upo wapi nikusaidie mjukuu wangu mi ndo babu kutoka sumbawanga
Nichec inbox natibu mali iliyo potea ,mapenzi,nauza majini pamoja na vifaru ,siasa nguvu za kiume na n.k

mh! Kwani mnatoa huduma hata kwa njia mtandao? Au na wewe ndo wale wale akina manyaunyau?
 
Kwani we upo wapi nikusaidie mjukuu wangu mi ndo babu kutoka sumbawanga
Nichec inbox natibu mali iliyo potea ,mapenzi,nauza majini pamoja na vifaru ,siasa nguvu za kiume na n.k

JINI unauza bei gani babu?
 
Back
Top Bottom