Nimesoma na kuhitimu uhasibu kwa ngazi ya cheti

MC RAS PAROKO

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
623
595
Nitangulize shukrazi kwenu wadau wa JF..
Mimi ni kijana wa kiume ninayeishi kilimanjaro. Nina cheti cha uhasibu na haikuwa malengo yangu kuishia certificate bali ni kutokana na kwamba nilikuwa nalipiwa ada na ndugu zangu ila kwa sasa wamedai ada ya diploma ipo juu sana na ukizingatia na wao watoto wao wanahitaji msaada wao kwani wanamaliza kidato cha nne mwaka huu. Hivyo ninahitaji ajira ambayo naweza kuifanya ili nijiwekee hela zangu na baadae Mungu akipenda nijilipie mwenyewe.(nipo tayari kulipwa hata 100,000 kwa mwezi) Siangalii sana kwenye taaluma niliyonayo {kuchagua kazi} ila naweza hata kuuza duka,sheli,stationary, hata kuwa msambazaji wa bidhaa,kufundisha
0 level commerce & book-keeping.
Naombeni msaada wenu wana jf niweze kufikia malengo niliojiwekea..

AHSANTENI.!
 
Ni bora ungesoma ualimu wa primary sasa hivi ungekuwa na mshahara, wakati mwngne maisha mnayakosea wenyewe
 
soma mitandao sana na magazeti kwa ajili ya kupata nafasi za kazi. Pia muombe Mungu hata kwa kufunga utafanikiwa
 
Back
Top Bottom