Nimeshtuka sana baada ya kuona wanachama kindakindaki wa ACT na CHADEMA wakijiunga na CCM. Hongera Dkt. Samia kwa kuwarejesha kundini kondoo

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,201
1,839
Mimi binafsi ni mdau mkubwa sana na muumini mzuri wa siasa za CCM na mara nyingi napenda sana kutembea kwenye matawi ya CCM kujua yanayoendelea.

Katika kipindi cha wiki moja tangu lile zuio la kutofanya mikutano ya hadhara ya kisiasa kutenguliwa nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu kujua mtazamo wa wanachama wa upinzani, je wamechukuliaje?

Nilichokiona kimenistaajabisha sana. Makundi kwa makundi wanarejesha kadi za vyama vyao na kuchukua kadi za CCM na wengi wakipongeza uamuzi wa Samia na kusifu mabadiliko ambayo CCM imenuia kuyaleta.

Karibu wote nilioona wanarejesha kadi ili kuchukua za CCM ni wale wakereketwa wa upinzani. Ni wale wa 'nitafia upinzani', nimewajua kutokana na juhudi walizoonesha kipindi fulani kuupambania upinzani.

Binafsi nampongeza sana Rais Samia kwa uamuzi wake mgumu kwa kukirudisha CCM katika enzi yake, Ile enzi ambayo imebaki kovu kwa upinzani mpaka leo.

Uamuzi wa Rais Samia ni muafaka kwa mustakabali za siasa za hoja.

Upinzani najua wanaamini sasa ni wakati wao lakini wangejua kinachoendelea huku chini namna gani watu wanavyopagawa na maamuzi ya Chifu Hangaya basi wangetumia majukwaa yao kumpongeza badala ya kumponda na kuwakasirisha Wananchi.
 
Mimi binafsi ni mdau mkubwa sana na muumini mzuri wa siasa za CCM na mara nyingi napenda sana kutembea kwenye matawi ya CCM kujua yanayoendelea..
Hv bado mna zile sinema zetu za kuwakusanya wana ccm na kuwavalidha sare za chadema na kusema wamerejea ccm?

Tupia picha zao hapa wakirudisha kadi za kidigital za chadema, la sivyo utakuwa umtunga tu story ili upewe bk 7 hapo Lumumba
 
Nasema
Hv bado mna zile sinema zetu za kuwakusanya wana ccm na kuwavalidha sare za chadema na kusema wamerejea ccm??? Tupia picha zao hapa wakirudisha kadi za kidigital za chadema, la sivyo utakuwa umtunga tu story ili upewe bk 7 hapo Lumumba
Nimesema nilichokiona
 
Umekiona ww , na mm naeleza usanii wa ccm kuwavalisha wanachama wake sare za chadema na kusema wamerejea ccm kumbe ni ulongo mtupu ... ukitaka tuamini, bc tupia picha zao hapa wakirudisha kadi za kidigital na siyo yale mabox ya zamani
CCM haina sababu yoyote ya kufanya hayo unayosema. Jaribu kufanya tathmini uone ukweli wake
 
Watu kama huyu mleta mada ndio alikuwa anawasema Trump
20230111_225952.jpg

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Mimi binafsi ni mdau mkubwa sana na muumini mzuri wa siasa za CCM na mara nyingi napenda sana kutembea kwenye matawi ya CCM kujua yanayoendelea...
Mkuu mbona hili la kawaida tu?!! subiri CHADEMA waanze mikutano..wote watarudi... mbona toto kenda Azam kisha karudi?
 
Mimi binafsi ni mdau mkubwa sana na muumini mzuri wa siasa za CCM na mara nyingi napenda sana kutembea kwenye matawi ya CCM kujua yanayoendelea.

Katika kipindi cha wiki moja tangu lile zuio la kutofanya mikutano ya hadhara ya kisiasa kutenguliwa nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu kujua mtazamo wa wanachama wa upinzani, je wamechukuliaje?

Nilichokiona kimenistaajabisha sana. Makundi kwa makundi wanarejesha kadi za vyama vyao na kuchukua kadi za CCM na wengi wakipongeza uamuzi wa Samia na kusifu mabadiliko ambayo CCM imenuia kuyaleta.

Karibu wote nilioona wanarejesha kadi ili kuchukua za CCM ni wale wakereketwa wa upinzani. Ni wale wa 'nitafia upinzani', nimewajua kutokana na juhudi walizoonesha kipindi fulani kuupambania upinzani.

Binafsi nampongeza sana Rais Samia kwa uamuzi wake mgumu kwa kukirudisha CCM katika enzi yake, Ile enzi ambayo imebaki kovu kwa upinzani mpaka leo.

Uamuzi wa Rais Samia ni muafaka kwa mustakabali za siasa za hoja.

Upinzani najua wanaamini sasa ni wakati wao lakini wangejua kinachoendelea huku chini namna gani watu wanavyopagawa na maamuzi ya Chifu Hangaya basi wangetumia majukwaa yao kumpongeza badala ya kumponda na kuwakasirisha Wananchi.
Ukilala na njaa lazima uote ndoto za kijinga kijinga tu
 
Hv bado mna zile sinema zetu za kuwakusanya wana ccm na kuwavalidha sare za chadema na kusema wamerejea ccm?

Tupia picha zao hapa wakirudisha kadi za kidigital za chadema, la sivyo utakuwa umtunga tu story ili upewe bk 7 hapo Lumumba
Bado upo kwenye usingizi wa pono
 
Back
Top Bottom