Nimepoteza mwendo au mzunguko wa siku zangu za mwezi

Wavizangila

Member
Jun 3, 2011
33
2
Watanzania wote na nchi zote nawasalimia naomba mnishauri / mnipatie dawamimi nina umri wa miaka 40 sieleweki na tatizo langu lina kama mwaka sasa nilikuwa natumia dawa za uzazi wa mpango toka nimeacha ndo yananitokea haya na maziwa yangu huwa kama mtu mjamzito nikikaribia siku zangu nimeenda hospitali wakahisi labda nina vivimbe lakini hawakuviona naomba msaada ndugu zangu
 

Riwa

JF-Expert Member
Oct 11, 2007
2,598
3,018
Mzunguko wa mwanamke huwa unatawaliwa na hormones ambazo kiasi chake kwenye damu kinatofauti kufuatana na siku za mzunguko, na hivyo mwili unarespond tofauti. Si kitu cha ajabu matiti kujaa na/au kuuma kidogo ukikaribia hedhi!

Kuna dawa za uzazi wa mpango ukitumia unakuwa hupati hedhi (sindano ya Depo-Provera) kwa angalau miezi mi3, ndiyo ulikuwa unatumia? Ila ukiacha baada ya miezi mi3 hivi unaendelea kupata hedhi.

Umri wa miaka 40 unaanza 'menopause' ambapo mwanamke anakoma kupata siku zake. Mara nyingi huwa haikomi ghafla, kunakuwa na mabadiliko ya mwezi mara unapata mara unakosa, baada ya muda hedhi inakoma kabisa...ni kawaida (soma kuhusu menopause au kukoma hedhi).

Daktari uliyemuona kama ni wa magonjwa ya wanawake alikuwa anatosha kukupa maelezo kuhusu menopause na uzazi wa mpango. Unaweza ukawa na vivimbe yes, lakini mara nyingi vivimbe (fibroids) huongeza damu kutoka wakati wa hedhi, na sio kukausha (except labda ukiwa umeshakoma hedhi). Tafuta daktari wa magonjwa ya wanawake kwa uchunguzi na ushauri zaidi.
 

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
7,288
Daktari uliyemuona kama ni wa magonjwa ya wanawake alikuwa anatosha kukupa maelezo kuhusu menopause na uzazi wa mpango. Unaweza ukawa na vivimbe yes, lakini mara nyingi vivimbe (fibroids) huongeza damu kutoka wakati wa hedhi, na sio kukausha (except labda ukiwa umeshakoma hedhi). Tafuta daktari wa magonjwa ya wanawake kwa uchunguzi na ushauri zaidi.

Mkuu naomba kama unaweza kunijulisha vitu vinavyosababisha hizi fibroids, madhara yake, na dalili zake zaidi ya kuongezeka damu ya hedhi...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom