Nimepigwa na house girl

Pole,ila ningetegemea kusikia walau mama watoto akitajwa.hiyo familia INA house girl bila mama??au huyohuyo ndo wife???

Anyway Sikh nyingine MPE mkeo atunze
 
Haina mama,,ni story ndefu adi kuamua kuishi hivyo kwa muda
 
Mkuu umewaza nje ya box. Kuna uwezekano alitumwa kwenda kusimamia site sasa pesa kala anajaribu kuona ikiwa uongo anaotunga utakubalika hapa JF kisha apeleke kwa mhusika.
Hiyo ni akili ya ukilaza uliopitiliza
 
Kwa ujumla haupo serious na mambo yako. Kabla ya kutafuta huyo HG anza kwanza kutafuta uzembe uliopo kichwani kwako. Ukiupata safisha.

Unawezaje kuanza safar ya site bila kitendea kazi yaani laki 7.
Huo uzembe nimeshautafuta na nimefanikiwa kuupata
 
Yaani wewe baba unampa house girl nguo afue? Line of command haipo sawa hapo kwako.

Pia huyo house girl ulikuwa unamlipa sh ngapi? Kama unamlipa elfu 30, laki saba ni mshahara wa miaka 2 kwanini asitokomee nazo?
Ata benk, watumishi wanashika mamilion,ila siyo rahisi kutokomea,cha muhimu uaminifu tu.
 
Kama uwongo umezidi, hii pesa yetu ilivyo haina thamani laki moja tu imejaza mfuko na umetuna sasa laki7 mfuko unakuaje kama sio unatuongopea unatoa suruali ushindwe hata kusikia kibulunguti kina nepanepa, na usawa huu wa magu nani anaisahau elfu kumi kaweka wapi ije hiyo laki7, kweli hii chai
 
Potezea Fanya umetoa sadaka hata ukimkamata umpati hata na mia,ajawahi pata laki hela hizo zitamlevya
Nipo kwenye machungu yasiyo na kifani baada ya kupigwa tsh 700,000 na house girl. Ilikuwa hivi jana nimechukua hiyo fedha toka ATM ili nikalipe mafundi wanaonifanyia kazi moja ya ujenzi.

Fedha zote zote hizo nikaziweka kwa mfuko wa nyuma ,basi jana jioni kufika nyumbani nikavua hiyo suruali nikaitundika kwenye mlango nikaingia kulala.

Kuamka asubuhi kwa mbwembwe zote nikakusanya nguo zote pamoja na ile suruali iliyokuwa na laki saba kwenye mfuko wa nyuma nikamkabidhi house girl kwa ajili ya kufua.

Basi nikaseme ngoja nipate supu hapa mtaani halafu nielekee site kukutana na mafundi,ile namaliza kupata supu ndipo nakumbuka fedha za kwenda kuwalipa mafundi nimezisahau kwenye suruali niliyovaa jana.

Yaani nilirudi nyumbani kwa kasi ya duma, nafika nakuta baadhi ya nguo zipo apo chini na zingine bado azijafanyiwa ufuaji,halafu mhusika(house girl) haonekani.

Duh nikajua tayari nimeshapigwa halafu kazima na simu,kumbe kabeba laki saba katokomea zake. Yaani nimechoka kwa kweli ,housegirl kanifanya mtaji, ila kitaelweka tu nitamtafuta kila kona kuanzia nchi kavu,angani adi majini , kwa sababu maumivu aliyoniachia ni zaidi ya mwanaume kupigwa kwenye testicle.

Uzuri baadhi ya ndugu zake nawafahamu, usiombe upigwe laki saba kipindi hiki.
 
mkuu sio sahihi kumwachia housegirl afue nguo zako......
 
Huwezi kusahau laki saba kwenye mfuko wa suruali kama maisha yako njaa njaa kama wewe? Hapo utakuwa umeongeza sifuri sifuri mbele itakuwa elfu 7 ya supu baada ya kubanwa na mama ntilie ukaona ukimbilie nyumbani kusave nayo ukaona hola ndio unamsingizia dada wa watu kusave soo au kuja kuchangamsha genge humu.

Laki saba tena ya ujenzi usahau kwenye mfuko wa suruali kwa usawa huu wa magu njoo na bandiko jingine mkuu.
hahahaaaa alitaka tujue kwamba anajenga!.......
 
Unampa pole ya bure tu huyu mkuu wewe kweli unaweza kusahau laki saba kwenye mfuko wa suruali kwa usawa huu wa magu?

Hiyo hela ata ukilala na mke usiku unashituka kuitazama kama ipo kweli.

Kusahau kupo mkuu, hawa wafanyakazi wa ndani sio wa kuwaamini...hata nyumba yangu nikitoka huwa nafunga kabisa..
 
Kama uwongo umezidi, hii pesa yetu ilivyo haina thamani laki moja tu imejaza mfuko na umetuna sasa laki7 mfuko unakuaje kama sio unatuongopea unatoa suruali ushindwe hata kusikia kibulunguti kina nepanepa, na usawa huu wa magu nani anaisahau elfu kumi kaweka wapi ije hiyo laki7, kweli hii chai
Ebu jaribu kunisoma tena polepole
 
Tatizo unamlipa 20K/month.
Unadhani anggetakiwa awe kijakazi wako kwa muda apate kibunda ndefu namuna huo?
 
Back
Top Bottom