Nimepigwa na house girl

Nipo kwenye machungu yasiyo na kifani baada ya kupigwa tsh 700,000 na house girl. Ilikuwa hivi jana nimechukua hiyo fedha toka ATM ili nikalipe mafundi wanaonifanyia kazi moja ya ujenzi.

Fedha zote zote hizo nikaziweka kwa mfuko wa nyuma ,basi jana jioni kufika nyumbani nikavua hiyo suruali nikaitundika kwenye mlango nikaingia kulala.

Kuamka asubuhi kwa mbwembwe zote nikakusanya nguo zote pamoja na ile suruali iliyokuwa na laki saba kwenye mfuko wa nyuma nikamkabidhi house girl kwa ajili ya kufua.

Basi nikaseme ngoja nipate supu hapa mtaani halafu nielekee site kukutana na mafundi,ile namaliza kupata supu ndipo nakumbuka fedha za kwenda kuwalipa mafundi nimezisahau kwenye suruali niliyovaa jana.

Yaani nilirudi nyumbani kwa kasi ya duma, nafika nakuta baadhi ya nguo zipo apo chini na zingine bado azijafanyiwa ufuaji,halafu mhusika(house girl) haonekani.

Duh nikajua tayari nimeshapigwa halafu kazima na simu,kumbe kabeba laki saba katokomea zake. Yaani nimechoka kwa kweli ,housegirl kanifanya mtaji, ila kitaelweka tu nitamtafuta kila kona kuanzia nchi kavu,angani adi majini , kwa sababu maumivu aliyoniachia ni zaidi ya mwanaume kupigwa kwenye testicle.

Uzuri baadhi ya ndugu zaka nawafahamu, usiombe upigwe laki saba kipindi hiki.[/QUOTE.
Pole sn nina amini utaipata
 
Yaani wewe baba unampa house girl nguo afue? Line of command haipo sawa hapo kwako.

Pia huyo house girl ulikuwa unamlipa sh ngapi? Kama unamlipa elfu 30, laki saba ni mshahara wa miaka 2 kwanini asitokomee nazo?
 
Pole sana, lakini nikulaumu kitu kimoja. Utampaje nguo zako HG wakati una mke? Amin Amin nakuambia, nguo zangu haziwezi kufuliwa na HG. Period.
 
Nipo kwenye machungu yasiyo na kifani baada ya kupigwa tsh 700,000 na house girl. Ilikuwa hivi jana nimechukua hiyo fedha toka ATM ili nikalipe mafundi wanaonifanyia kazi moja ya ujenzi.

Fedha zote zote hizo nikaziweka kwa mfuko wa nyuma ,basi jana jioni kufika nyumbani nikavua hiyo suruali nikaitundika kwenye mlango nikaingia kulala.

Kuamka asubuhi kwa mbwembwe zote nikakusanya nguo zote pamoja na ile suruali iliyokuwa na laki saba kwenye mfuko wa nyuma nikamkabidhi house girl kwa ajili ya kufua.

Basi nikaseme ngoja nipate supu hapa mtaani halafu nielekee site kukutana na mafundi,ile namaliza kupata supu ndipo nakumbuka fedha za kwenda kuwalipa mafundi nimezisahau kwenye suruali niliyovaa jana.

Yaani nilirudi nyumbani kwa kasi ya duma, nafika nakuta baadhi ya nguo zipo apo chini na zingine bado azijafanyiwa ufuaji,halafu mhusika(house girl) haonekani.

Duh nikajua tayari nimeshapigwa halafu kazima na simu,kumbe kabeba laki saba katokomea zake. Yaani nimechoka kwa kweli ,housegirl kanifanya mtaji, ila kitaelweka tu nitamtafuta kila kona kuanzia nchi kavu,angani adi majini , kwa sababu maumivu aliyoniachia ni zaidi ya mwanaume kupigwa kwenye testicle.

Uzuri baadhi ya ndugu zaka nawafahamu, usiombe upigwe laki saba kipindi hiki.
Kwa ujumla haupo serious na mambo yako. Kabla ya kutafuta huyo HG anza kwanza kutafuta uzembe uliopo kichwani kwako. Ukiupata safisha.

Unawezaje kuanza safar ya site bila kitendea kazi yaani laki 7.
 
Kwa ujumla haupo serious na mambo. Kabla ya kutafuta huyo HG anza kwanza kutafuta uzembe uliopo kichwani kwako. Ukiupata safisha.

Unawezaje kuanza safar ya site bila kitendea kazi yaani laki 7.
conditional reflex
 
Laki saba umezitoa bank, ukazisahau! Ukaenda kupata supu kwenye banda......!!!!!

Napata wasiwasi kuamini kama hizo pesa zilikua zako
Mkuu umewaza nje ya box. Kuna uwezekano alitumwa kwenda kusimamia site sasa pesa kala anajaribu kuona ikiwa uongo anaotunga utakubalika hapa JF kisha apeleke kwa mhusika.
 
Mna house girl kwa ajili ya kufua tu? sawa mkeo hayupo ww ukampa mdada nguo, ksha waenda kwe supu ina maana hampk hamna watoto? akiamka cha kwanza kufua hahhhaa, hii chai kwa kwel
 
Back
Top Bottom