Unaingia Baa na laki ili utumie buku ten ajabu unarudi asubuhi na buku ten tu

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
14,304
29,837
Maisha yapo hivo sio lazima tufanane, wewe jenga nyumba mm nanunua gari, wewe save mimi natumia. Kuna mda unatoka kwenye hustle Nzito unasema Leo nimepiga penyewe ngoja niingie kwenye Viti virefu kwenye hii laki niliyonayo nitumie elfu kumi tu ili saa Tatu usiku nipumzike afu tisin ni save

Mchawi yupo kwenye bia ya pili baada ya hapo Kuna kitu kinasema pesa Zipo tu kesho siku unaanza kuagiza Za mafungu, zikikolea unamove kutoka kwenye serengeti kwenda kwenye Windhoek, unaona hapa kisuma pakichoko unaenda tip-top unakutana na warembo suruali inasimama unaweka mmoja kwenye siti unamwagizia serengeti lite huku unamshika matako, hajakaa Sawa unamwagizia chipsi kuku na wewe unapiga mishikika,

Mda huooo saa nane usiku unaangalia salio ipo forty, unaona hapa ngoma imeondoka unaona usiku umalizie tu, bia zimekolea unaona Dunia yote yako, asubuhi kunakucha umebaki na buku ten tu unajishangaa upo ambiance mkaka anafanya usafi wa kuokota machupa wengine wa mama wanaandaa supu huku barabarani wanafunz wanaenda shule

Unahangaika hiace upo full confidence unafika geto unalala unaamka saa saba mchana unaanza kushtuka hangover unapotezea unaona muda unaenda njaa inakukamata mara kichwa kinauma Kwa mbali ushuzi unanuka hatari, unaenda Kwa mama bonge unaagiza ugali dagaa unakula kidogo tu ngoma yote inabaki, siku inaisha kesho unaingia tena kwenye mapambano kutafuta faranga
 
Back
Top Bottom