Nimepigwa na house girl

moesy

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2012
Messages
3,237
Points
2,000

moesy

JF-Expert Member
Joined Oct 30, 2012
3,237 2,000
Nipo kwenye machungu yasiyo na kifani baada ya kupigwa tsh 700,000 na house girl. Ilikuwa hivi jana nimechukua hiyo fedha toka ATM ili nikalipe mafundi wanaonifanyia kazi moja ya ujenzi.

Fedha zote zote hizo nikaziweka kwa mfuko wa nyuma ,basi jana jioni kufika nyumbani nikavua hiyo suruali nikaitundika kwenye mlango nikaingia kulala.

Kuamka asubuhi kwa mbwembwe zote nikakusanya nguo zote pamoja na ile suruali iliyokuwa na laki saba kwenye mfuko wa nyuma nikamkabidhi house girl kwa ajili ya kufua.

Basi nikaseme ngoja nipate supu hapa mtaani halafu nielekee site kukutana na mafundi,ile namaliza kupata supu ndipo nakumbuka fedha za kwenda kuwalipa mafundi nimezisahau kwenye suruali niliyovaa jana.

Yaani nilirudi nyumbani kwa kasi ya duma, nafika nakuta baadhi ya nguo zipo apo chini na zingine bado azijafanyiwa ufuaji,halafu mhusika(house girl) haonekani.

Duh nikajua tayari nimeshapigwa halafu kazima na simu,kumbe kabeba laki saba katokomea zake. Yaani nimechoka kwa kweli ,housegirl kanifanya mtaji, ila kitaelweka tu nitamtafuta kila kona kuanzia nchi kavu,angani adi majini , kwa sababu maumivu aliyoniachia ni zaidi ya mwanaume kupigwa kwenye testicle.

Uzuri baadhi ya ndugu zake nawafahamu, usiombe upigwe laki saba kipindi hiki.
 

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Messages
11,620
Points
2,000

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2016
11,620 2,000
Nipo kwenye machungu yasiyo na kifani baada ya kupigwa tsh 700,000 na house girl. Ilikuwa hivi jana nimechukua iyo fedha toka ATM ili nikalipe mafundi wanaonifanyia kazi moja ya ujenzi. Fedha zote zote hizo nikaziweka kwa mfuko wa nyuma ,basi jana jioni kufika nyumbani nikavua hiyo suruali nikaitundika kwenye suruali nakaingia kulala. Kuamka asubuhi kwa bwebwe zote nikakusanya nguo zote pamoja na ile suruali iliyokuwa na laki saba kwenye mfuko wa nyuma nikamkabidhi house girl kwa ajili ya kufua. Basi nikaseme ngoja nipate supu apa mtaani alafu nielekee site kukutana na mafundi,ile namaliza kupata supu ndipo nakumbuka fedha za kwenda kuwalipa mafundi nimezisahau kwenye suruali niliyovaa jana.
yaani nilirudi nyumbani kwa kasi ya duma, nafika nakuta baadhi ya nguo zipo apo chini na zingine bado azijafanyiwa ufuaji,alafu mhusika(house girl) haonekani. Duh nikajua tayari nimeshapigwa alafu kazima na simu,kumbe kabeba laki saba katokomea zake. Yaani nimechoka kwa kweli ,housegirl kanifanya mtaji, ila kitaelweka tu nitamtafuta kila kona kuanzia nchi kavu,angani adi majini , kwa sababu maumivu aliyoniachia ni zaidi ya mwanaume kupigwa kwenye testicle.Uzuri baadhi ya ndugu zaka nawafahamu, usiombwe upigwe laki saba kipindi hiki.
Huwezi kusahau laki saba kwenye mfuko wa suruali kama maisha yako njaa njaa kama wewe? Hapo utakuwa umeongeza sifuri sifuri mbele itakuwa elfu 7 ya supu baada ya kubanwa na mama ntilie ukaona ukimbilie nyumbani kusave nayo ukaona hola ndio unamsingizia dada wa watu kusave soo au kuja kuchangamsha genge humu.


Laki saba tena ya ujenzi usahau kwenye mfuko wa suruali kwa usawa huu wa magu njoo na bandiko jingine mkuu.
 

moesy

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2012
Messages
3,237
Points
2,000

moesy

JF-Expert Member
Joined Oct 30, 2012
3,237 2,000
Huwezi kusahau laki saba kwenye mfuko wa suruali kama maisha yako njaa njaa kama wewe? Hapo utakuwa umeongeza sifuri sifuri mbele itakuwa elfu 7 ya supu baada ya kubanwa na mama ntilie ukaona ukimbilie nyumbani kusave nayo ukaona hola ndio unamsingizia dada wa watu kusave soo au kuja kuchangamsha genge humu.


Laki saba tena ya ujenzi usahau kwenye mfuko wa suruali kwa usawa huu wa magu njoo na bandiko jingine mkuu.
nalo neno
 

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Messages
11,620
Points
2,000

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2016
11,620 2,000
poleee sana mkuuuu
kwelii inaumaaa sanaa umejinyimaa lkn Mungu anajua namna ya kukulipaaaa mkuuu
nakushauri wala usihangaikee buree kumtafutaaa maana utapoteza gharama nyingine mkuuuuu
Unampa pole ya bure tu huyu mkuu wewe kweli unaweza kusahau laki saba kwenye mfuko wa suruali kwa usawa huu wa magu?

Hiyo hela ata ukilala na mke usiku unashituka kuitazama kama ipo kweli.
 

Khaligraph Jordan

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2017
Messages
6,425
Points
2,000

Khaligraph Jordan

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2017
6,425 2,000
nikavua hiyo suruali nikaitundika kwenye suruali, Kuamka asubuhi kwa bwebwe zote
😂😂😂😂😂😂😂😂 uachege ujinga.


Back in mada, ipigie kampuni ya simu aliyokuwa akiitumia waeleze watai trace hiyo simu kwani kwa akili yake ni lazima kaitupa laini ila simu ni ileile ataendelea kutumia utampata kirahisi
 

Forum statistics

Threads 1,389,938
Members 528,059
Posts 34,039,154
Top