Nimepigwa mzinga wa maana leo

Nimepigwa mzinga wa maana leo

Ulivo mzembe Mwanaume mwenzio ungemkaushia au hata kujibu vibaya
Mkuu mim huwa najawa n.a. huruma sana. Hata leo pale makumbusho nilivyoshusha mzigo sehemu fulani ivi pindi narudi kudaka usafiri nielekee ofisini kwangu, Nikakutana na special need mmoja akaniomba chochote (Kilema wa mguu) nikamtoa buku
 
wamesambaa hao jumamosi nilikutana nao wanaomba nauli buku mbili Ila niliwacheki nikaona hawa wanatafuta pesa ya kula barabarani nikawatosa ukiwaona hawafanani kbx
 
Kipindi wife niliyemuoa baada ya kumuacha mke wangu wa ndoa hajanipiga limbwata madem kama hao walikuwa hawakatizi.
 
Hello wana wanabody habari za jioni

Niende moja kwa moja kwenye mada.
Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu. Leo nilikuwa n.a. safari kwenda shule fulani maeneo ya mtoni mtongani (kwaazizially) kwa lengo la kuchukua order ya vifaa vya stationeries....!! Mimi ni supplier wa vifaa ivyo.
Wakati natoka hapo shuleni nikasema let me go to posta now. Nilipotaka kuvuka upande wa pili, ili nikapate usafiri kuelekea posta nikawaona wadada 2 warembo kweli kweli...nisiwe mnafiki hapa kwa kweli walikuwa wazuri siyo reception wala Tigo. Hakika waliumbwa wakaumbika.

Nikasema ngoja nivute faster niwasalimu kidogo. Nilipo wakaribia kumbe na wao walikuwa wananifanyia tyming. Na maongezi yetu yakawa ivi....!!!

Mimi: Mambo zenu watoto wazuri.....?
Wao: Nzuri
Moja kati yao akaniambia.....!!
Yeye: Kaka samahani. Naomba utusaidie elfu mbili ya nauli.
mimi: Nikamuuliza, mnaenda wapi?
Yeye: Tunaenda Kigamboni.
Mimi: mnatoka wapi....?
Yeye: Kwa Dada, anaishi Mtoni mtongani.
Mimi: Sawa. Though nikawa nawaza n.a. kutafakari iweje hawa wadada wazuri ivi wakose nauli tena elfu 1 na si elfu 2. Au ndiyo januari imekaza na kuvaa bukta nyeusi nini...? Manake from mtoni adi kigamboni ni elfu 1 kwa wawili. Baada ya kutafakari kwa kina nikatoa elfu 2. Nikawapatia kiroho safi tena bila kinyongo. Tukaagana n.a. kila mmoja akawa busy kusubiri usafiri wake.

Muda mfupi nikawaona wanashuka kituo kinachofata pembeni nikamuona yule Dada mwingine aliyekuwa nyuma pindi namwoji mwenzake...amemfesi kaka mmoja anamuomba nauli kwenda posta.
Nikashangaa n.a. kupigwa n.a. butwaa nikajisemea kimoyo moyo tayari nimeisha pigwa MZINGA tena asubuhi asubuhi...!!!.kwa kweli nilitamani kuwakimbiza wale wadada lakini nikasita na kujishauri wasije wakanigeukia hapa nikapata aibu ya mwaka. Kwani mjini mpango. Ingawa roho inaniuma.
Hivyo ndivyo nilivyopigwa mzinga siku ya Leo.
Ahsanteni naomba kuwasilisha
Hahaha! Mjini shule jamani. Na vyuma vilivyokaza hv, mjini sio shule tena bali ni CHUO! Hahaha akina dada mnatia huruma aisee!....na bado mtapiga mizinga sana mwaka huu.
 
Ungewapiga cha ten na kubeba namba mda huu badala ya kukesha JF ungekua unajigongea
It is not such easy. Kama ingekuwa hivyo, hata wao wasingekuwa wanashinda mitaani kusaka pesa kwa mizinga bali wangezama Jolly Club wapige pesa ndefu.
 
Ulikuwa unawashangaa mno mpaka wakakusoma,
 
Ndo maana ulipigwa limbwata
Ila limbwata lako halisaidii kiivyo kwani saizi nimla mtoto wake wa kumzaa ninamaanisha nakula kuku na yai lake. Me ndo mkurugenzi bwana, wengine wa kuchonga tu.
 
Back
Top Bottom