Je, ni kweli Bongo maisha yamekuwa magumu kwa sasa? Nimepigwa mzinga na wahitimu watatu ndani ya siku moja. Kiwango wanachoomba ndiyo kimenishangaza!

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
11,537
18,002
Toka Mwezi wa tisa nimekuwa nikipigwa mara KWA mara simu na watu ninao wafahamu wakiomba kukopeshwa hela.

Wanasema maisha yamekuwa magumu sana hela hawaioni.


Leo nimepigwa simu na watu watatu graduates ambao ninafahamiana nao.

KILA mmoja kanipigia KWA wakati wake.

HAWA ni graduate ambao nilimaliza nao chuo mwaka mmoja..( mind u nime graduate mwaka 2011)


Kilicho ni shangaza zaidi ni kiwango cha hela wanacho omba.

Sh elfu ishirini. Elfu kumi..
Mmoja nilimuazima elfu hamsini alinishukuru hadi aibu nikaona mimi.


Huyu ni mtu ambae miaka minne iliyo pita alikuwa anajimudu vizuri ila now mambo yamekuwa magumu.


Last week nikiwa mitaa ya kariakoo nilikutana na jamaa huyu yeye alisoma sheria so alivyo maliza 2011 aliunganisha LST akaapishwa uwakili mwaka 2013.

Na yeye mambo yake hayakuwa mabaya. Alikuwa anaweza kuyamudu maisha yake.

Juzi nimekutana nae kariakoo nikiwa naelekea pale Al Uruba hotel ( mgahawa wa wasomali) kupata makange ya samaki na ndizi bukoba za kupika.

Baada ya salamu story mbili tatu jamaa anapiga mzinga wa boku mbili ya nauli anasema mambo magumu sana.

Nilijisikia vibaya sana nikampa jamaa huku ten. ( Am.a Geminine. We are generally generously)


So jamani naomba kuuliza ndugu zangu ni kweli sasa hivi maisha ni magumu ama?

N.B: mimi ambacho kimenisaidia na ambacho kinafanya ni si feel huo ugumu wa hela ni vitu vingi lakini leo nitataja vitu vitatu.


1. Nimejifunza kutoka kwa Wana wa ISACHAR sio ISACK ni ISACHAR. HAWA walikuwa wanaishi kulingana na nyakati zilizopo. Mungu alipendezwa nao kwa sababu walifanya mambo yao kulingana na nyakati zilizo kuwepo. Hawakushindwa na jambo lolote lile KWA sababu walikuwa vizuri sana kwenye intelligence gathering and analysis.

So hata mimi nimekuwa nikiishi kulingana na nyakati zilizopo. Nimekuwa nikifanya biashara na shughuli zangu kulingana na nyakati zilizopo.

2. Nimejifunza kutoka kwa uumbaji wa Mungu..Mungu aliumba Tembo/Nyangumi lakini huyo huyo aliumba sisimizi. Nimejifunza nini kwenye hilo? more especially kwenye perspective ya biashara? Kwamba natakiwa kuinvest kwenye biashara kubwa kubwa bila kusahau biashara ndogo ndogo.

Kama nita invest kwenye biashara ambayo ninauza bidhaa au huduma kwa Mamilioni ya shilingi BASI natakiwa pia nisiache ku invest kwenye biashara ndogo ndogo ambayo ina uza bidhaa za sh mia, mia mbili, mia tano, elfu moja etc. ( There is no business like small business)

Bahkresa anafanya hivi. Ndio maana ana uza ving'amuzi/anatoa huduma ya usafiri wa boti lakini at the same time anauza hadi maandazi ya sh mia mia.


3. Nimejifunza kwenye nature. Nilifanya utafiti kujua ni kitu GANI huwa kina survive kwenye mazingira magumu. Vipo vingi ila kimoja wapo ni mti wa mtende. Nikajiuliza hivi mti wa mtende unaweza vipi kusurvive jangwani. Moja Kati ya sababu ni kuwa na mizizi imara. So nifanye nini kuileta attribute ya mtende kwenye maisha yangu ya kibiashara.

Jibu ni kuwa na mizizi imara kwenye biashara na shughuli zangu.

Siwezi kukosa hela .

Siwezi kuwa masikini maisha yangu yote.

Jay Z aliwahi kusema.kwenye wimbo " I love the dough" alioshirikishwa na Biggie Smalls " Being broke is childish and I am quite grown"
 

Notorious thug

JF-Expert Member
Dec 29, 2021
2,094
7,320
Pole sana... Ulikuwa na umri gani wakati huo? Je, kulikuwa na watu waliosimama pamoja nawe wakati huo wa shida? Ulikuwa na mpenzi wakati huo au wote uliotongoza walikukwepa?
Nilikua na miaka 19 sikua na mtu wa kuni-push nilikua na kademu flan kakachukuliwa na jamaa flan alikua muuza nguo.
 
13 Reactions
Reply
Top Bottom