Nimepewa siku 7 niwe nimenunua mashine ya EFD

Nimepewa siku 7 niwe nimenunua mashine ya EFD

Tulipe tu kodi. Jamaa wamechachamaa hatariii... Nunua tu mashine, nenda kwa wakala, lipa hata nusu, wakala anakupa mashine,, na ukija kulipa kodi baadae, TRA wanapunguza kodi yako kwakua mashine ni bure!. soo kama ulikua ulipe kodi labda ya milion moja, utalipa laki mbili tu, maana laki nane ulishaitoa wakati unanunua mashine.

Fine ya kutokua na mashine ni 3 million,.. Fine ya kuuza bila kutoa risiti ya EFD ni 4.5 million...
Hii yakukatwa kwenye Return za mwezi sina hakika nayo kama nikweli hebu toa Shule hapa sote tujue inavyokuwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau habari zenu!

Leo nimefika kwenye biashara yangu nimekutana na barua wakinitaka kununua mashine ya efd na wamenipa siku 7 la sivyo watakuja kupiga makufuli, Je hii ni sawa maana nina mtaji wa kawaida tu hata mil 30 hazifiki!

Je kuna namna yeyote ya kuomba kuongezewa muda? Je ni kweli kwamba mashine ni laki 8? Je hakuna mashine zenye bei nafuu kuliko hiyo? Na ikiwa watafunga biashara faini yao ni kiasi gani?

Natanguliza shukrani!
Upo mkoa gani mkuu?
 
Hivi wakiweka makofuli yao na mimi nikaamua kuyakata na kutoa mali zangu kisha namrudishia land lord frame yake watanipata wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau habari zenu!

Leo nimefika kwenye biashara yangu nimekutana na barua wakinitaka kununua mashine ya efd na wamenipa siku 7 la sivyo watakuja kupiga makufuli, Je hii ni sawa maana nina mtaji wa kawaida tu hata mil 30 hazifiki!

Je kuna namna yeyote ya kuomba kuongezewa muda? Je ni kweli kwamba mashine ni laki 8? Je hakuna mashine zenye bei nafuu kuliko hiyo? Na ikiwa watafunga biashara faini yao ni kiasi gani?

Natanguliza shukrani!
Matumizi ya machine yatakusaidia kulipishwa kodi inayoendana sawa sawa na biashara yako tofauti na sasa ambapo wanakisia tuu hivyo kuleta mvutano kati yako na hao wakadiriaji.

Nunua tuu machine uwe huru. Mtaji wa million 30 kama unauzungusha vizuri ukiweka na mali za mikopo bado uko vizuri
 
Nunua,acha kulalamika.Sisi wengine tumezinunua kwa bei zaidi ya hiyo unayotaja.Kwa hali ilivyo,alternative nyingine ni kufunga biashara. Sidhani kama uko tayari kwa hilo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom