Nimepewa siku 7 niwe nimenunua mashine ya EFD

Nimepewa siku 7 niwe nimenunua mashine ya EFD

Pole mkuu lakini hapa Same traffic police wanatoza madereva fine bila kuwapa EFD risiti. hizi za kuandika kwa mkono ni halali? wahusika watusaidie. Raisi amesema.tudai risit nadhani zile za EFD. wachunguzwe. wana gari T353 BAJ
 
Nipo sahihi
Maxcom wanayo tenda ya efd na ktk series ya mashine zao zipo zinazounganishwa na kuwa na huduma ya efd pia (Max95FT)

Fuatilia maxcom watakupa majibu
Hii naona imekaa poa...nimewaona maxcom kwenye list ya supplier wao! Kama inawezekana kuintergrate na huduma nyingine ni bora zaidi!
 
Una heri wewe uliepewa siku 7 za kujipanga,wengine chupu chupu on the spot tuliambiwa ndani ya 48hrs tuwe na EFD machine laa penalty Tsh2,500,000/=tutakapozitoa tutajua wenyewe,ni shida sana hii kitu ukizembea wanakufilisi.mashine zipo zinauzwa 700,000/= ukiwa na cash but unaweza kuilipia kwa awamu ndani ya mwezi mmoja ila hii inaongezeka 50,000/=.kama upo Dar nenda mtaa wa Lumumba na Kipata zilipo office za TRA kitengo cha kodi mkabala napo pana jengo kwa chini kuna bank ya access wapo 2th floor.ukihitaji mawasiliano yao sema nitakutumia Pm mkuu.

sent from my Infinix S2 Pro using JamiiForums mobile app
 
Tulipe tu kodi. Jamaa wamechachamaa hatariii... Nunua tu mashine, nenda kwa wakala, lipa hata nusu, wakala anakupa mashine,, na ukija kulipa kodi baadae, TRA wanapunguza kodi yako kwakua mashine ni bure!. soo kama ulikua ulipe kodi labda ya milion moja, utalipa laki mbili tu, maana laki nane ulishaitoa wakati unanunua mashine.

Fine ya kutokua na mashine ni 3 million,.. Fine ya kuuza bila kutoa risiti ya EFD ni 4.5 million...
 
Asante mkuu..angalau mmenipa mwanga!
 
Pole mkuu lakini hapa Same traffic police wanatoza madereva fine bila kuwapa EFD risiti. hizi za kuandika kwa mkono ni halali? wahusika watusaidie. Raisi amesema.tudai risit nadhani zile za EFD. wachunguzwe. wana gari T333 BAJ
Ni nani wa kuwakamata polisi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu na inakuwaje Kwa biashara ambayo ni ya siku nyiingi kwenye documents lakini haijawahi kukadiriwa kodi na TRA halafu ukainunua machine na kuipeleka kusajiri tra ili makadirio ya kodi yafuate badaye, je kuna vikwazo vyovyote?
 
Mimi ninayo mashine ya maximalipo yenye uwezo wa kuunganisha efd ninauza mwenye pesa aje pm tuzungumze
Napatikana kagera

Mashine ikisha sajiliwa kwa jina la biashara yako na TIN namba yako huwezi kubadilisha majina kwenye hiyo mashine tena.
 
Wakuu na inakuwaje Kwa biashara ambayo ni ya siku nyiingi kwenye documents lakini haijawahi kukadiriwa kodi na TRA halafu ukainunua machine na kuipeleka kusajiri tra ili makadirio ya kodi yafuate badaye, je kuna vikwazo vyovyote?
Unafanyaje biashara bila kulipa kodi?
 
Wadau habari zenu!

Leo nimefika kwenye biashara yangu nimekutana na barua wakinitaka kununua mashine ya efd na wamenipa siku 7 la sivyo watakuja kupiga makufuli, Je hii ni sawa maana nina mtaji wa kawaida tu hata mil 30 hazifiki!

Je kuna namna yeyote ya kuomba kuongezewa muda? Je ni kweli kwamba mashine ni laki 8? Je hakuna mashine zenye bei nafuu kuliko hiyo? Na ikiwa watafunga biashara faini yao ni kiasi gani?

Natanguliza shukrani!
njoo na laki m7na 50 na kopi ya tin nikupe mashine
 
Tra si wa kuchezea. Yawezekana wakati wenzio wanafuatilia mashine kipindi kile wewe ulipuuzia. Tra watakufilisi na ukicheza uraweza hata kujinyonga. Najua mauzo ya wiki yanatosha kabisa kununua hiyo mashine
 
Back
Top Bottom