Nimepewa siku 7 niwe nimenunua mashine ya EFD

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
16,456
Reaction score
38,236
Wadau habari zenu!

Leo nimefika kwenye biashara yangu nimekutana na barua wakinitaka kununua mashine ya efd na wamenipa siku 7 la sivyo watakuja kupiga makufuli, Je hii ni sawa maana nina mtaji wa kawaida tu hata mil 30 hazifiki!

Je kuna namna yeyote ya kuomba kuongezewa muda? Je ni kweli kwamba mashine ni laki 8? Je hakuna mashine zenye bei nafuu kuliko hiyo? Na ikiwa watafunga biashara faini yao ni kiasi gani?

Natanguliza shukrani!
 
simu saba sio salama kabisa utazitumia zote

ila siku saba ni salama nenda kanunue mkuu usibashane na uma EFD 800,000 ila ukiendelea kubishana na hawa jamaa utajikuta unapoteza mamilioni
 
Sawa mkuu..kuna uwezekano wa kuomba kuongezewa muda siku 7 ni chache sana kwangu!
 
Faini mil 3 mbona hatari duh
hiyo fine inazungumzika nunua mashine kisha kaonane nao lipa fine kiasi hata laki 5 hizo zingine wata wave, wewe Biashara iendelee Ukibishana nao kaka utauwa watoto na njaa
 
Wadau habari zenu!
...
Je kuna namna yeyote ya kuomba kuongezewa muda? Je ni kweli kwamba mashine ni laki 8? Je hakuna mashine zenye bei nafuu kuliko hiyo? Na ikiwa watafunga biashara faini yao ni kiasi gani?

Natanguliza shukrani!
Ghali laki 8 au milioni moja kwa kuendelea na biashara inayokuingizia fedha na kullipa kodi ya kuiwezesha Serikali kupata pato kwa ajili ya maendeleo ya nchi!

Hapo ulipo una simu ya bei mbaya na matumizi ya muda wa hewani na 'bundle' kila siku! Jiulize!
 
hiyo fine inazungumzika nunua mashine kisha kaonane nao lipa fine kiasi hata laki 5 hizo zingine wata wave, wewe Biashara iendelee Ukibishana nao kaka utauwa watoto na njaa
Shukrani mkuu
 
Wadau habari zenu!

Leo nimefika kwenye biashara yangu nimekutana na barua wakinitaka kununua mashine ya efd na wamenipa siku 7 la sivyo watakuja kupiga makufuli, Je hii ni sawa maana nina mtaji wa kawaida tu hata mil 30 hazifiki!

Je kuna namna yeyote ya kuomba kuongezewa muda? Je ni kweli kwamba mashine ni laki 8? Je hakuna mashine zenye bei nafuu kuliko hiyo? Na ikiwa watafunga biashara faini yao ni kiasi gani?

Natanguliza shukrani!
Hi waliniletea kwenye kwenye kabiashara kangu
 
Back
Top Bottom