Nimepata sababu ya kutoacha Pombe...

Hivi Asprin na Teamo hizi bear or something yenye kilevi haina madhara kwenye afya ya binadamu kama mimi???
Nadhani unamaanisha beer hapo. Hapa mama hatuzungumzii madhara, tunazungumzia dhambi! Hata nyama ina madhara kwa binadamu, kwa hiyo tuache kula?
 
Mbona mnajichanganya na vifungu vinajieleza wazi? Ni nani awezaye kutengua maneno ya biblia na kutengeneza yanayoendana na imani yake? Kwa ufupi "Son of God" alikuwa anapiga misosi na ulabu na hiyo ndiyo maana ya bold na red za Asprin. Kula na tax collectors na sinners si ndiyo hawa tunakutana nao bar wanagonga round na milupo pia inakuwepo maeneo hayo, kwani mimi na wewe siyo wadhambi? Suala ni je baada ya kunywa utachukua milupo? Utajifunza njia za kifisadi ili ujenge heshima bar nk. nk.

Mkuu Asprin thanks! Issue imekaa vizuri hasa siku kama hii ya ijumaa umenikumbusha kudu the needful responsibly
 
sasa mtu akiwa anakula chakula, anaitwa na watu mlafi, unafikiri alikuwa anakula hadi kuvimbiwa? na mtu kama alikuwa anakunywa divai, na watu wakasema mlevi, unafikiri alikuwa anakunywa pombe?...hivi kula ni ulafi? na kunywa ni ulevi?....cha maana ni kwamba, Neno la Mungu haliwezi kujipinga, Kuna maeneo mengi mno nitakuletea yanaongelea kuwa pombe ni haramu..na Biblia inasema Yesu hakutenda dhambi hata moja, hivyo kama pombe ni haramu, Yesu hakunywa, angekuwa amekunywa Yesu asingesemwa kuwa hakutenda dhambi...Unaliamini Neno la Mungu kuwa ni amina na kweli? au? hivi wewe ukichukua ule mvinyo mweusi uliotokana na kuchujwa kwa zabibu ukanywa ina maana unakuwa umekunywa pombe?

zaidi ya yote, unachotakiwa kujua ni kwamba, kipindi kile, hakukuwa na chai ama kahawa ama vitu vingine hivi...mtu akila mkate, alikuwa anashushia na divai (isiyolevya), divai ilikuwa kama chai ya sasa, haikuwa inanywewa ile ya kulevya. sasa, watu wote utakaowapotosha hapa kwa maneno yako, damu yao itadaiwa mikononi mwako siku ile ya mwisho...!
....Alaaa, umejuaje? hili nalo lipo kwenye bibilia, kwamba wakati ule kulikuwa hakuna vinywaji vingine isipokuwa juisi ambayo waliita divai?

(Tatizo ni akili za kushikiwa na mitume na maaskofu vihiyo)
 
Andiko lako haliendani kabisa na defence yako. Ningekuwa jaji nawe ni mshitakiwa ningekuhukumu vibao kwanza hapo hapo mahakamani. inaonekana umezoea kukariri maandiko tu. Hata kiingereza kidogo kama hicho unashindwa kuelewa? and you call yourself a great thinker??

Mwanzoni nilidhani unaquote andiko linalosema..."mpe maskini kilevi asahau shida zake" na hilo sikwambii liko wapi.

Ila kumbuka pombe huharibu fikra ikishatumiwa na kumfanya mtu kutenda mabaya mbele za watu na Mungu.

Ndio maana huwezi kuwa jaji kwa kuwa huna sifa hizo. Sijawahi kujiita great thinker na wala sipendi mtu aniite hivyo kwa kuwa kiukweli mimi siyo great thinker kama wewe. Inawezekana kweli kiingereza kidogo sikijui, after all siyo lugha ya mama yangu na wala kujua kiingereza siyo kigezo cha kuwa na maarifa. Lakini hebu nitafsirie "drunkard" ni nini kwa kiswahili?
 
Divai ilikuwa haileweshi? Kuna maandiko nimesahau vifungu (damn beer). Lutu (Sijui Nuhu?) alinyweshwa divai na mabinti zake akalewa mabinti zake wakalala naye.. Unaijua?

Sina nia ya kupotosha watu hapa mkuu. Nimetoa kifungu ambacho Yesu mwenyewe anasema watu walimwita mlevi, kwa maana alikuwa anakunywa. (Haikuelezwa kama alikuwa anakunywa divai isiyolewesha, sijui wewe ulijuaje) Isitoshe katika biblia pia kuna vifungu vinahalalisha watu kula ulabu; "Mpe maskini kileo, anywe alewe asahau shida zake" umeshawahi kuiona hii?

Lutu ndiyo alinyweshwa pombe na binti zake nao wakalala naye...lakini haimaanishi kuwa Kunywa pombe kwake kipindi kile ilikuwa halali. ilikuwa ni dhambi vilevile ndo maana yote hayo yalimkuta. hata nuhu alikunywa pombe akalewa akaweka instrument zake wazi mtoto wake Hamu akaziona akacheka...hata mtoto wake hamu akalaaniwa badaye....ni kwasababu ya Pombe..haimaanishi kuwa pombe ilikuwa imehalalishwa kipindi hicho....ni dhambi, na si kwamba hao watu walikuwa malaika, walikuwa ni watu wa Mungu lakini walikuwa wanafanya makosa vilevile

unajua Bible inasema, zamani Mungu alijifanya mjinga na alikuwa anaachilia tu uovu kutendeka, lakini kwasasa Mungu anawaamuru watu wote watubu na kumfuata yeye, wasipofanya hivyo ameandaa siku atakayowahukumu wote. hivyo usiweke evidence za agano la kale ambalo Mungu alikuwa anajifanya mjinga na sasahivi baada ya kuleta wokovu kupitia mwanae mpendwa Yesu Kristo na Roho wake Mtakatifu kutuongoza...hakuna cha kujitetea kwasasa. zamani watu hawakuwa na Yesu, na hawakuwa na Roho kama sasa..hivyo Mungu alikuwa anachukuliana nao hivyohivyo. na enzi ile imebadilika kwa Kuja kwa Yesu kwaajili ya ukombozi wako mkuu wangu.
 
enzi zote pombe ni haram. kizazi cha kanaani kililaaniwa kwasababu ya pombe pale Nuhu babu yao alipolewa na Ham akauona uchi wa babake. unakumbuka Lutu alilewa binti zake wakalala naye na wakapatikana kizazi cha waamoni na wamoabu watu ambao kwasasa ni raia wa Jordan na maeneo ya syria and around that area. Biblia inasema kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu na kuwa waasherati, wazinzi na walevi hawataurithi ufalme wa Mungu. Pombe ni shetani, maeneo yote yanayouzwa pombe yana harufu kabisa ya shetani na vitu vyote vya kishetani vinapatikana pale, kuanzia kupapasapapasa wanawake/uzinzi,kuibiana kufanya kila kitu. JAMANI, NURU NA GIZA VIKO WAZI MNO, NI DHAHIRI HAVIHITAJI KUJIULIZA MASWALI...hili mbona liko wazi, pombe ni giza na siku zote wanywaji wa pombe wanaogopa mwanga...Neno la Mungu,,,hata kama hawatakwambia lakini roho zao huwa zinawasuta muda wote kwamba wanatenda dhambi. Mungu awasaidie.
Hapa unawasemea wanywaji wa biere au unatoa mtazamo wako ambao hakuna anayeweza kuuthibitisha isipokuwa Mungu?
 
Hivi wale jamaa wa Alshabab wa somalia - waasi wa serikali ya Somalia (kama ipo) nao wanakunywa sana pombe eehh!! au maasi unayongelea ni asprin kumuona Eliza mzuri baada ya bia ya saba na valuu mbili?

ha ha ha ha ha u made my day ...
 
Mbona mnajichanganya na vifungu vinajieleza wazi? Ni nani awezaye kutengua maneno ya biblia na kutengeneza yanayoendana na imani yake? Kwa ufupi "Son of God" alikuwa anapiga misosi na ulabu na hiyo ndiyo maana ya bold na red za Asprin. Kula na tax collectors na sinners si ndiyo hawa tunakutana nao bar wanagonga round na milupo pia inakuwepo maeneo hayo, kwani mimi na wewe siyo wadhambi? Suala ni je baada ya kunywa utachukua milupo? Utajifunza njia za kifisadi ili ujenge heshima bar nk. nk.

Mkuu Asprin thanks! Issue imekaa vizuri hasa siku kama hii ya ijumaa umenikumbusha kudu the needful responsibly
Mkuu nimekutendea haki kwenye hii yuziful posti. Ukipita maeneo ya Zero Pub utakuta mbili za baridi zinakusubiri..

....Alaaa, umejuaje? hili nalo lipo kwenye bibilia, kwamba wakati ule kulikuwa hakuna vinywaji vingine isipokuwa juisi ambayo waliita divai?

(Tatizo ni akili za kushikiwa na mitume na maaskofu vihiyo)
Hahahaha! ndio maana nimewapiga chini nikaamua kusoma biblia mwenyewe. Sidanganyiki!
 
Mbona mnajichanganya na vifungu vinajieleza wazi? Ni nani awezaye kutengua maneno ya biblia na kutengeneza yanayoendana na imani yake? Kwa ufupi "Son of God" alikuwa anapiga misosi na ulabu na hiyo ndiyo maana ya bold na red za Asprin. Kula na tax collectors na sinners si ndiyo hawa tunakutana nao bar wanagonga round na milupo pia inakuwepo maeneo hayo, kwani mimi na wewe siyo wadhambi? Suala ni je baada ya kunywa utachukua milupo? Utajifunza njia za kifisadi ili ujenge heshima bar nk. nk.

Mkuu Asprin thanks! Issue imekaa vizuri hasa siku kama hii ya ijumaa umenikumbusha kudu the needful responsibly

watu mmedata si kidogo
 
sasa wandugu pombe zenyewe inategemea ni POMBE GANI.....................

adhawaisi kuna ile mambo ya mwasiti SIO KISA POMBE.......!
 
enzi zote pombe ni haram. kizazi cha kanaani kililaaniwa kwasababu ya pombe pale Nuhu babu yao alipolewa na Ham akauona uchi wa babake. unakumbuka Lutu alilewa binti zake wakalala naye na wakapatikana kizazi cha waamoni na wamoabu watu ambao kwasasa ni raia wa Jordan na maeneo ya syria and around that area. Biblia inasema kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu na kuwa waasherati, wazinzi na walevi hawataurithi ufalme wa Mungu. Pombe ni shetani, maeneo yote yanayouzwa pombe yana harufu kabisa ya shetani na vitu vyote vya kishetani vinapatikana pale, kuanzia kupapasapapasa wanawake/uzinzi,kuibiana kufanya kila kitu. JAMANI, NURU NA GIZA VIKO WAZI MNO, NI DHAHIRI HAVIHITAJI KUJIULIZA MASWALI...hili mbona liko wazi, pombe ni giza na siku zote wanywaji wa pombe wanaogopa mwanga...Neno la Mungu,,,hata kama hawatakwambia lakini roho zao huwa zinawasuta muda wote kwamba wanatenda dhambi. Mungu awasaidie.

Kabla ya kuondoa kibanzi.........ondoa boliti........ (siendelei). "Siyo kila asimaye bwana bwana atauona ufalme wa Mungu". Ni nani huyu awezaye kuhukumu? Mbona Yesu mwenyewe alikutana na wadhambi kibao lakini hakuwahukumu? mbona mafundisho yote ya Yesu sijaona ukali huu na hukumu hizi za kibinadamu?
 
Si umeona? Same applies to ulabu. Kama nimepiga bia zangu mbili nikajirudia zangu home kucheza na watoto kuna ubaya wowote hapo na Mungu?
...Niliwahi kumuuliza mtu mmoja aliyejifanya kuwa ni mwokovu...nikienda bar nikigonga serengeti zangu 4 then huyooo na-drive kwenda nyumbani sijatukana mtu, sijatongoza eliza wala elizabetty, nikiwa home nakula raha na kuendelea na life kama kawaida kuna dhambi gani ya kutumia pombe hapo?? Tatizo wengi wao wanakariri tu kuwa pombe ni dhambi lakini hawana justification yoyote ya maana.
 
Lutu ndiyo alinyweshwa pombe na binti zake nao wakalala naye...lakini haimaanishi kuwa Kunywa pombe kwake kipindi kile ilikuwa halali. ilikuwa ni dhambi vilevile ndo maana yote hayo yalimkuta. hata nuhu alikunywa pombe akalewa akaweka instrument zake wazi mtoto wake Hamu akaziona akacheka...hata mtoto wake hamu akalaaniwa badaye....ni kwasababu ya Pombe..haimaanishi kuwa pombe ilikuwa imehalalishwa kipindi hicho....ni dhambi, na si kwamba hao watu walikuwa malaika, walikuwa ni watu wa Mungu lakini walikuwa wanafanya makosa vilevile

unajua Bible inasema, zamani Mungu alijifanya mjinga na alikuwa anaachilia tu uovu kutendeka, lakini kwasasa Mungu anawaamuru watu wote watubu na kumfuata yeye, wasipofanya hivyo ameandaa siku atakayowahukumu wote. hivyo usiweke evidence za agano la kale ambalo Mungu alikuwa anajifanya mjinga na sasahivi baada ya kuleta wokovu kupitia mwanae mpendwa Yesu Kristo na Roho wake Mtakatifu kutuongoza...hakuna cha kujitetea kwasasa. zamani watu hawakuwa na Yesu, na hawakuwa na Roho kama sasa..hivyo Mungu alikuwa anachukuliana nao hivyohivyo. na enzi ile imebadilika kwa Kuja kwa Yesu kwaajili ya ukombozi wako mkuu wangu.

Mkuu nilikuwa nataka nikuweke sawa manake ulisema divai ilikuwa haileweshi. Sasa ilikuwaje Lutu na Nuhu walilewa kwa kunywa divai?
 
...Niliwahi kumuuliza mtu mmoja aliyejifanya kuwa ni mwokovu...nikienda bar nikigonga serengeti zangu 4 then huyooo na-drive kwenda nyumbani sijatukana mtu, sijatongoza eliza wala elizabetty, nikiwa home nakula raha na kuendelea na life kama kawaida kuna dhambi gani ya kutumia pombe hapo?? Tatizo wengi wao wanakariri tu kuwa pombe ni dhambi lakini hawana justification yoyote ya maana.
Hili huwa hawalisemi kabisa. Watakuambia ukinywa moja lazima uongeze nyingine...
 
Ndio maana huwezi kuwa jaji kwa kuwa huna sifa hizo. Sijawahi kujiita great thinker na wala sipendi mtu aniite hivyo kwa kuwa kiukweli mimi siyo great thinker kama wewe. Inawezekana kweli kiingereza kidogo sikijui, after all siyo lugha ya mama yangu na wala kujua kiingereza siyo kigezo cha kuwa na maarifa. Lakini hebu nitafsirie "drunkard" ni nini kwa kiswahili?

Thanks Mkuu... ni vizuri kuendelea kuchambua hoja kuliko hao wanaokuja na hukumu tayari mikobani in the name of great thinking

hebu ngoja nielewe mada kwanza
 
Ndio maana huwezi kuwa jaji kwa kuwa huna sifa hizo. Sijawahi kujiita great thinker na wala sipendi mtu aniite hivyo kwa kuwa kiukweli mimi siyo great thinker kama wewe. Inawezekana kweli kiingereza kidogo sikijui, after all siyo lugha ya mama yangu na wala kujua kiingereza siyo kigezo cha kuwa na maarifa. Lakini hebu nitafsirie "drunkard" ni nini kwa kiswahili?
Kile kibatani cha kukagua kimegoma.
SENKI YUU!! uwezo wako nimeukubali katika post hii!
 
Hapo awali msimamo wangu ulikuwa kwamba nitaacha pombe endapo tu:
1. Nimeshauriwa na daktari kwa manufaa ya afya yangu.
2: Nimeishiwa kiasi kwamba kununua bia unakuwa mzigo mkubwa

Nilishawishiwa na baadhi ya watumishi wa Mungu kuwa niache pombe, kwa kuwa eti pombe ni dhambi (imagine, eti bia ni dhambi?). Aisee walikaribia kufanikiwa mpaka nilipokutana na Neno Hili Takatifu toka katika kitabu Kitakatifu Cha Mungu. Hapa aliandika Mtakatifu Matayo katika Sura ya 11 ya Injili yake:

.16"To what can I compare this generation? They are like children sitting in the marketplaces and calling out to others: 17" 'We played the flute for you, and you did not dance; we sang a dirge and you did not mourn.' 18For John came neither eating nor drinking, and they say, 'He has a demon.' 19The Son of Man came eating and drinking, and they say, 'Here is a glutton and a drunkard, a friend of tax collectors and "sinners." ' But wisdom is proved right by her actions."

HILO NDILO NENO LA MUNGU!

Leo ntakunywa bia kwa raha sana.

Ahsanteni na wikiendi njema!!!!

Hii kitu imekuja saa ngapi hapa??

Watu wengine wanajitahidi sana kuhalalisha dhambi...

Ngoja mi nikaandae misa ya asubuhi, naweza nikawa nabishana na watu ambao tayari walishaanza kuone maluweluwe hapa...
 
Nadhani unamaanisha beer hapo. Hapa mama hatuzungumzii madhara, tunazungumzia dhambi! Hata nyama ina madhara kwa binadamu, kwa hiyo tuache kula?

sawa kabisa kwa sababu Topic ni ya beer namaanisha hivyo mheshimiwa ..
 
Hii kitu imekuja saa ngapi hapa??

Watu wengine wanajitahidi sana kuhalalisha dhambi...

Ngoja mi nikaandae misa ya asubuhi, naweza nikawa nabishana na watu ambao tayari walishaanza kuone maluweluwe hapa...
Ya nini malumbano?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom