Nimepata mgeni wa ajabu sana

Nimepata mgeni wa ajabu sana

Kuna kijana mtoto wa baba mkubwa kaja kunitembelea hapa nyumbani baada ya kumaliza form six wanasubilia selection za chuo ila huyu kafeli maana kapata four ya mwisho.Sasa nilichoudhika ni hili tukio nililolikuta home kwangu.Yaani nimekuta limekunywa Box zima la Heinken zangu na st.Anna za mke wangu ***** zake cha kushangaza sasa toto dogo nimekuta linakula sigara packet nzima tena sebuleni yaani hili toto lina siku moja limeanza kufanya hivi nimekuta sebuleni kumejaa moshi kama jamaika aisee.AISEE HILI TOTO NASIKIA BABA YAKE ALILEA KWA KULIDEKEZA NA KUNA TETESI HATA HUO MTIHANI WA FORM SIX HALIJAFANYA.WAKUBWA HEBU NISAIDIENI MBINU ZA KULITIMUA KWA SABABU NAHISI NIMETEMBELEWA NA PAMPULA NA SIO MGENI TENA.MBAYA ZAIDI HUYU DADA WA KAZI AISEE KANIHADITHIA VITIMBWI VILIVYOKUWA VINATENDWA NA HILI TOTO MPAKA MENGINE AIBU KUYAANDIKA.NIPENI MBINU WAKUU HAPA KWANGU ANA SIKU MBILI NATAKA NIMG'OE HAPA.

Sent using Jamii Forums mobile app
yaani unashindwa kufanya maamuzi mepesi kama hayo mpaka unakuja huku
Timua tu,kosa ni ulevi na kuvuta sigara
 
Mwambie ajiandae kesho mnaenda kwao, mkifika huko waambie matatizo yake then rudi kwako.
 
Kwan kwako kuna vyumba vingapi??
Kama havitoshi mwambie arudi kwao umepata mgeni mpya
Chumba cha wageni kipo na cha dada wa kazi kipo in short huyu dogo ni mfano wa mitoto iliyoelewa vibaya sijui kiburi kwao walikuwa wanazo ila baada ya jpm kuingia life imebadilika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilichogundua wewe jamaa ni mchoyo alafu mke wako ndio mwenye kauli ndani ya nyumba zaidi yako, sababu kubwa ya kumfukuza huyo dogo ni kunywa pombe zenu.. mama watoto akakuweka kitimoto umfukuze mdogo wako, chukua uamuzi wa kumfukuza maana nyumba ni yako ila kaa ukijua hiyo ni tabia na inazidi kuota mapembe.. kesho utamfukuza na baba ako kwasababu ya mke.
Malipo ni hapahapa duniani, na watoto wako watakuja kufukuzwa siku moja.
 
Kwanza wewe ni msanii kama Yule wa GPA ya 32,unasema amepata four ya mwisho afu unadai inasemekana mitihani hakufanya,kama hakufanya mitihani hyo four ya mwisho kaipataje?Unaandika inasemekana baba yake alimlea kwa kumdekeza,mtoto wa ba mdogo wako usiwe na uhakika alilelewa vipi? Any way Kama kaja kutembea mvumilie tu ataondoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari divison four niliambiwa na baba yake ila mimi nimejaribu kuserach matokeo yake hayapo na pia kuna dogo alisoma nae anasema hakufanya mtihani amemdanganya baba yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
establish ground rules
  • thou shall not smoke
  • thou shall not drink alcohol (it's for papa n' mama only)
  • thou shall not touch or disrespect the house maid (she is part of the family)
  • thou shall not come home after sunset
  • thou shall help the maid with daily activities like dish washing and mopping
  • if you can not follow the above rules, thou shall go back to your papa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom