Nimepanga nisome open university degree ya ICT, Lakini malalamiko ya watu humu ni Mengi je ni uhalisia?

Nimepanga nisome open university degree ya ICT, Lakini malalamiko ya watu humu ni Mengi je ni uhalisia?

opondo

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2017
Posts
545
Reaction score
1,346
Mimi ni mtumishi, Nilipata ruhusa ya kwenda masomoni lakini sikwenda kwasababu ya ukiritimba uliopo halmashauri kwamba ukienda masomoni basi uwezi kupanda daraja, na Mimi napanda daraja Mwakani, nimetimiza miaka mitatu ya ajira Sasa, naona nikasome kitu kingine, passion yangu ni Mambo ya computer, nimechungulia open university nimeona degree ya Information and Communication Technology nimeangalia zile course outline zote zinasomeka tu, sikuhuzi platform za kujifunza ni nyingi, Nimeomba open university na Masomo yanaanza Mwezi wa nne, nimejaribu kufatilia nimeona Malalamiko mengi sana kuhusu hiki chuo Cha open university,

Lengo langu ni kumaliza baada ya miaka 3, lakini nimeona watu kulalamika kwamba, ni ngumu kumaliza Kwa miaka mitatu, lecture ni wasumbufu, mtihani inapotea, wakufunzi wanaomba hela ya ziada na malalamiko Mengi zaidi.

Swali langu ni moja je hayo mambo yana uhalisia? Nifanyeje ili nimalize Kwa wakati, au niachane nayo niende tu mwakani nikasome kampasi?.….
 
nimejaribu kufatilia nimeona Malalamiko mengi sana kuhusu hiki chuo Cha open university,

lakini nimeona watu kulalamika kwamba, ni ngumu kumaliza Kwa miaka mitatu,

Haya umeuliza pia waliosoma chuoni If ni asilimia kubwa tatizo?

Kitu gani kimekuvutia haswa kutaka kusoma hiyo ICT miaka hiyo? Malengo uweje mbeleni? nime elewa ni degree ambapo umesoma kitu ingine kabla..

Majibu ya kuhusu chuo.. sikijui kipoje.
 
Kashfa ya hicho chuo ni kuoffer "cheap and easy to access degree". Ni chuo ambacho kina reputation ya kusaidia wanafunzi kuhitimu na kupata vyeti but kuhusu ubora wa elimu na stadi za uhakika thats questionable na ngumu kuwapa benefit of the doubt.

Kwanini usitafute chuo kama mzumbe, at least CBE,IFM, UDSM, etc. why usitafute chuo chenye reputation nzuri usome na kama kazini wanataka kukupandisha daraja subiria kwanza upande daraja then utaendelea na maswala ya masomo baadae.
 
Kwa
Haya umeuliza pia waliosoma chuoni If ni asilimia kubwa tatizo?

Kitu gani kimekuvutia haswa kutaka kusoma hiyo ICT miaka hiyo? Malengo uweje mbeleni? nime elewa ni degree ambapo umesoma kitu ingine kabla..

Majibu ya kuhusu chuo.. sikijui kipoje.
Upande wangu nilitamani nisome degree ambayo ninaweza kujiajiri, pia chances ni kubwa kutoka kwenye ualimu kwenda nafasi nyingine, mfano hii halmashauri/mkoani/ taasisi zinazonizunguka ninaona Kuna uhaba pia wa watu wa tehama, ilo ndilo likilonosukuma kusoma, natamani sana niwe developer nadhani nikiwa vizuri kwenye angle hiyo inaweza kunifikisha sehemu, Asante.
 
Sema nini janja kama tayari wewe ni mtumishi unaweza kusoma OUT kwa sababu Tanzania wanachoangalia kwa watumishi waliojiendeleza ni makaratasi na sio kilicho kichwani

Kuna jamaa alisoma OUT lakini akiwa tayari mwajiriwa wa BoT na cheo kimepanda baada ya kugraduate

Ila hicho chuo simshauri mtu akasome ili akimaliza akapambane kutafuta ajira
 
Back
Top Bottom