Nimeota ndoto saa kumi alfajiri nimeshinda Stories of Change!

Habari zenu wadau!

Alfajiri ya leo Jumamosi mnamo saa 10:30 hivi nimeota kama nimeletewa mifuko mitatu mizuri sana. Katika mifuko yote kuna nguo. Naomba nielezee!

1. Mfuko huu una nguo nzuri sana imeandikwa mshindi namba moja wa stories of change, ila pale sikumbuki jina lake. Ukishika huu mfuko unaona kabisa ni nguo ambayo ina hadhi sana tangu nizaliwe sijawahi kuiona nguo ya namna hiyo nikasema hongera zake.

2. Nikaona mfuko wa pili, imeandikwa mshindi wa pili, una nguo nzuri sana pia, inavutia mno nikatoa pongezi huku nikijiuliza sasa mimi naletewa yote mitatu kwa nini na ya washindi Hawa hata siwajui, anyway!

3. Nikaona mfuko wa tatu, huu una tisheti (T-shirt) nzuri sana ni rangi ya dark blue. Nikaona hii tisheti imeandikwa jina langu PS BONIFACE, chini yake nikaona yameandikwa majina ya watu wengine wanne ndani ya tisheti moja. Nikaanza kujiuliza sasa hii ni yangu au mmoja wa hawa wanne chini yangu.

Huko huko ndotoni likaja wazo kuwa mimi ni mmoja wa washindi wa JF Stories of change kwa andiko langu ila ushindi wangu ni namba 3 na kuendelea ndiyo maana ya hizi zawadi nionavyo.

Nilipoamka ilikuwa saa 10:57 alfajiri, ghafla nikaingia JF telegram naona matokeo ya mshindi wa tano hadi wa kwanza. Akili yangu ikapata bumbuwazi huku nikijiuliza sasa nini maana ya ile ndoto? Mbona mimi sijioni kabisa hapa.

Nilichojijibu mwenyewe: Ni kwamba majaji walipata tabu sana kuamua nani awe mshindi hasa kuanzia mshindi wa tatu na kuendelea. Ni wazi kuwa ndoto hutoka kwa Mungu kama ilivyoandikwa katika (Ayubu 33:14-15). Itakuwa Mungu kwa kuwa ni Jaji Mkuu alichonionesha ameamua kunifariji kuwa kihaki ulitakiwa uwepo kuanzia 3 hadi 7 ila waliokuwa ni majaji wa hilo wamepitiwa tu tena ilikuwa jukumu zito kwao.

Jamani kumtegemea Mungu raha sana. Unajua hii ndoto umenipa raha sana. Nimepata kujiamini kuwa nimejitajidi maana tangu nizaliwe sijawahi shiriki mashindano ya kuandika isipokuwa mwaka huu hili limekuwa shindano la pili. Nimepata faraja kuona angalau mbingu zimenipa kujua siko mbali sana kati ya washiriki 1509. Inawezekana kabisa majaji mmepata tabu sana kuamua washindi nawapongeza kwa kazi njema.

Pongezi za dhati kwa washindi waliotuwakilisha katika hili shindano kwa awamu hii. Mungu awabariki sana.

Mwisho: Nawapongeza sana washindi waliotangazwa nimepita maandiko yote matano ukweli nimejifunza kikubwa kwenu, kuanzia ubunifu wa kuandika, mawazo chanya, na mtiririko wa mawazo mazuri. Nilichofurahia sana kwamba majaji wakiangalia vigezo kitaaluma bila kuangalia kura za watu wengi, hii safi sana.

Note: Nimeona niitunze hapa hii ndoto kabla sijaamka iwe kumbukumbu kwangu.

Unaweza soma nilichokuwa nimechangia kwenye shindano Usitafute ajira, tengeneza ajira
Abriana karoboa mkuu
 
Abriana karoboa mkuu
Washiriki
IMG_20211016_091529_964.jpg
 
Back
Top Bottom