Nimeomba huduma Tanesco na hili ndio jibu nililopewa

Watu wasiojulikana watawakamatia humu..

Tanesco wangeweka utaratibu wa kupokea malalamiko kama ambavyo baadhi ya benki hufanya.

Watuwekee platform ya kuwaeleza kero zetu.

Ila kwa mikoani hawa TANESCO wanajitahidi sana,kuanzia huduma,fast response hata lugha zao wanajitahidi kwa hakika. Sio kama miaka kadhaa nyuma.

Endeleeni kuliboresha shirika letu. Maana siku sio nyingi mtaongezewa umeme wa nyerere HP.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kweli aisee umetoa angalizo zuri mno unaombwa details na unatoa kizembeee kabisaàa bila kukimbuka kuwa ulishacomment na kutoa threads za kuponda juhudi za awamu
 
Watu wasiojulikana watawakamatia humu..

Tanesco wangeweka utaratibu wa kupokea malalamiko kama ambavyo baadhi ya benki hufanya.

Watuwekee platform ya kuwaeleza kero zetu.

Ila kwa mikoani hawa TANESCO wanajitahidi sana,kuanzia huduma,fast response hata lugha zao wanajitahidi kwa hakika. Sio kama miaka kadhaa nyuma.

Endeleeni kuliboresha shirika letu. Maana siku sio nyingi mtaongezewa umeme wa nyerere HP.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mfumo wa kupokea malalamiko upo tena wa kielctronic na hivi karibuni tutawaletea kingine kipya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo 20/02/2020 nimemtuma kijana WANGU nikiwa nimempatia photocopy ya kitambulisho changu na passport size moja. Pamoja na no yangu ya simu .

Aende ofisi za Tanesco Darlive akanichukulie fomu kwa ajili ya kuomba kupatiwa umeme kwenye nyumba yangu iliyoko Mkokozi - Mkuranga.

Alipofika kwenye ofisi za Tanesco Darlive Mbagala akajibiwa hawatoi fomu nje ya Wilaya ya Temeke, aliponijulisha nikaiga simu na kuongea nao na wakanishauri niende Mkuranga ama Kurasini.

Nikamtumia kijana WANGU fedha na kumtaka aende Mkuranga, alipofika Mkuranga na kuulizwa nyumba ziko wapi? alipojibu akaambiwa mwambie mwenyewe aje.

Akanijulisha na mm nikapiga simu na kuulizia vp, jibu nililopewa ni fupi, NDO HIVYO njoo ww mwenyewe, nikamjibu Niko mbali , akajibu siku ukipata muda na nafasi njoo.

Nikamwambia bwanamdogo aondoke, nikaingia humu jamii forum ukurasa wa Tanesco na kupata no za simu Pwani.

Nilipopiga ikapokelewa Kibaha nikajieleza mkasa mzima ,kwa kweli mtumishi aliyenijibu akashangaa kwann kijana amekataliwa kupewa fomu.

Nikaomba ushauri nn nifanye akanipatia no ya afisa uhusiano nilipopiga simu ikawa haipatikani.

Nimeomba ruhusa kazini kesho inshallah ntafika katika ofisi za Tanesco Mkuranga kuchukua fomu.

Kama wanavyotaka baadhi ya watumishi wao kinyume na taràtibu zilivyowekwa na ofisi.
 
Moja ya jambo linalokera nihili la kuambiwa njoo mwenyewe.

Yani huwezi kumtuma hata mkeo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa Wala hakuwa na shida stress zake zilikuwa zinamsumbua, akidhani Ni ile tanesco yazamani
Tanesco ni ile ile hujasikia juzi huko Daslam nguzo zimekaa mtaani miaka miwili wananchi hawajasambaziwa umeme? Kule Zingiziwa chanika wamerundika nguzo tu wala hazisimikwi toka mwaka jana mwishoni nadhani wanasubir kampeni zikaribie ndio wataweka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moja ya jambo linalokera nihili la kuambiwa njoo mwenyewe.

Yani huwezi kumtuma hata mkeo

Sent using Jamii Forums mobile app
Leo nimetekeleza Amri yao. Nimefika na kuhudumiwa vzr Sana. Ila sikuona umuhimu wowote wa mm mwenyewe kuwepo kwa ajili ya kuchukua fomu hiyo.

Maana nimeombwa kitambulisho na passport size Kisha nikarejeshewa kitambulisho pamoja na fomu.

Maswali yaliyoulizwa nyumba ziko wapi, Karibu na nn? Alama muhimu ni ipi? ( Vitu ambavyo kijana angejibu au ningetoa maelekezo kupitia simu).

Lkn yote kwa yote ilinilazimu pia kwenda huko na fundi WANGU wa umeme ili kupunguza gharama ya nenda Rudi hivyo nimekamilisha Kila hatua .

Nimepewa wiki 3 za kusubiria.
 
Tanesco hivi kwetu kisesa mwahuli ndo mmetusahau kabisa? Kila siku ahadi za kuja kusimika nguzo na kutuunganishia umeme. Kama haiwezekani si tupewe majibu tu ya kueleweka tujiongeze ata kwa kununua viji solar kwa ajili ya kuchaji simu zetu
 
Back
Top Bottom