Nimeolewa na golikipa nifanyeje?

Nimeolewa na golikipa nifanyeje?

Suala la mapenzi hasa kumwacha au kuendelea kuwa naye siyo la kushauriwa, "you should listen to your heart when it comes to matters of love"

One more thing, wakati mnaoana alikuwa anashughulika na nini?
 
Mimi nina degree moja ila nimeolewa na mtu ambaye ana elimu ya msingi na hana shughuli yoyoye anayojishughulisha hata nimuelimishe vipi kuhusu biashara au kuhusu kwenda kujiendeleza hataki yeye anachotaka nimhudumie vyoote. Na mtu mwenyewe hata mapenzi hana ila anachotaka ni kuheshimiwa kama anapita Obama. Je? Nimuache au niendelee kumvumilia labda Mungu atambadilisha siku za usoni? Nisaidieni wenzangu

wakati mnaanzana alikudanganya kwa maneno gani mpaka ukakubali kuoelewa na primary school graduate?
 
Kwani ulikurupushwa kuolewa naye, na je leo ndo umegundua kuwa elimu yake ni ya msingi?
 
Mie ndio najisemeaga 'mtu anapanda bangi, anataka kuvuna mchicha' How?

Ndio maana yake: Nitambadilisha tu, mwingine alisema, bibi yake alimwambia hadi anioe ndio anafanikiwa.

Mwingine, kasema nikimwacha anajiua

lakini kwanini sasa hivi? si aliolewa nae akijua ni golikipa sasa kimetokea nini, au ndio tunarudi pale pale "nitambadilisha"?
 
Kaa naye chini mueleweshe maisha yalivyo kama una mtindo wa kumpa pesa punguza hiyo tabia...tafuta siku nzuri sana tokeni out umueleze kinagaubaga na mtishe kabsa umepewa notice ofisin utatimuliwa kazi miezi miwili ijayo so lazma mjiimarishe inabidi jifunze kula na kipofu kama akili yake ya kijinga mpeleke kijinga kijinga mfanyishe biashara kwa kumtisha akishaona faida yake akili itakaa sawa...ukishindwa kaone washauri wenu labda wazazi mshenga kanisani....

Ila swali linanitatza tabia zake kabla ya ndoa zilikuaje??? Je ulikua unajua ni std 7 ?? Ulikutana naye vipi??? Je umejuaje hakupendi??? Na kama hakupendi unaomba ushauri wa nini??? Mwisho je wewe unampenda na kumjali.....

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Jamani, wapo wanamme wa aina hi kabisa, anapewa mtaji anaunywea pombe wote.
Afu mke unamsikia 'nina degree'
Wananiudhi hadi basi, nina mfano wa karibu sana.
Kimsingi kosa ni mwanamk maana kama ni kweli inaonesha msichana alikosa options ndo maana akakubali kuolewa na huyo mwanaume..!!!
 
love is blind

Then marriage is an eye opener

sio mateja. nimeona stori kadhaa hapa MMU, dada kaolewa na mume lofa baadae mume suddenly kapata very high paying job na kumnunulia mkewe gari/nyumba la mamilioni. stori ikaitwa ''true love''
Ha ha ha, mtu asipokuwa na pesa akipatya inakuwa true love?!:smile-big:
 
Degree yako haijakusaidia.
Ila mumeo kaelimika pamoja na darasa lake la saba, akajua achague mke wa aina gani ili ale bata tu.

Abadilike amekuwa kinyonga?

Nina hasira na wewe maana rafiki yangu kaolewa na golikipa, anamtesa kama nini lakini kang'ang'ania tu, mnaudhi kama nini halafu na ushauri hamsikilizi, kazi kulalamika tu kwa matatizo yakujitakia.

Tena, bora aanze kutaka kubebwa mgongoni badala ya kutembea.

Hahahahahaaaaaaaaa ............ Umemaliza yoote!
 
........tamaa yako itakuwa juu ya mumeo naye atakutawala!!! umesahau hayo maneno nini? kama ni golikipa mzuri mpeleke Arsenal, wanatafuta golikipa saivi!!

hahahahahahha haki ya nani watu mna vituko jamani, jamani mtatufanya tushindwe kuleta matatizo yetu humu na mie nina langu halitofautiani sana na hili mwehh:tongue: bwana we umenivunja mbavu kabisaaaaa
 
Ulilazimishwa kuolewa na wazazi au uliamua wewe mwenyewe? Vicheche ndo walivyo hapo ujue umeshapata kidume kingine sasa unatafuta mapungufu ya mwenzio. Kwa mfano kwamba yeye la saba umejua leo??

Nasisi tulio na wanawake ambao hawajasoma tuwaache?, nadhani ili jamii ikutambue kuwa wewe ni msomi mojawapo ni kuishi kutegemea na mazingira yaliyokuzunguka, kwa maelezo yako basi we si msomi hata kidogo, hata waliokufundisha umewadhalilisha....na kama ningejua chuo ulichosoma basi ningeshauri kwa kusema kozi yako haina walimu wa kutosha hivyo serikari uwafutie usajiri na iwafungie kabisa. zaidi nadhani kama umeajiliwa, kampuni ulipo inapoteza mapato au umebebwa ......hufahi kabisa wewe. inabidi ufutiwe hata usajiri wa jamiiforum.je umeisharudisha mkopo uliokusomesha "bodi ya mkopo"?, au umepelekwa na baba yako fisadi....unajiona msomi. hufahi kabisa.
 
Degree yako haijakusaidia.
Ila mumeo kaelimika pamoja na darasa lake la saba, akajua achague mke wa aina gani ili ale bata tu.

Abadilike amekuwa kinyonga?

Nina hasira na wewe maana rafiki yangu kaolewa na golikipa, anamtesa kama nini lakini kang'ang'ania tu, mnaudhi kama nini halafu na ushauri hamsikilizi, kazi kulalamika tu kwa matatizo yakujitakia.

Tena, bora aanze kutaka kubebwa mgongoni badala ya kutembea.

Kongosho kwani huyo rafiki yako kaolewa na goalkeeper wa timu gani? Magolkeepers wana lipwa vzr mbona!
 
wakati mnapendana ilikuwaje,usije tegemea hata siku mmoja kuwa huyu atabadilika akisha ingia kwenye ndoa
 
Mimi nina degree moja ila nimeolewa na mtu ambaye ana elimu ya msingi na hana shughuli yoyoye anayojishughulisha hata nimuelimishe vipi kuhusu biashara au kuhusu kwenda kujiendeleza hataki yeye anachotaka nimhudumie vyoote. Na mtu mwenyewe hata mapenzi hana ila anachotaka ni kuheshimiwa kama anapita Obama. Je? Nimuache au niendelee kumvumilia labda Mungu atambadilisha siku za usoni? Nisaidieni wenzangu

Umeolewa au bado ni kijure? Ebu endelea kushikilia kile kilichokufanya kumpenda na kuolewa nae, hayo mengine ya darasa la saba yasikusumbue, ni mapito tu yataisha. Lazima umuheshimu, huyo ndiyo OBAMA wako. Soma biblia WAEFESO YOTE. Utapata neno la kukubariki na kukupa moyo.
 
umwache ili iweje wakati mnafungishwa ndoa mliambiwaje kifo ndo kita watenganisha, ukimwacha ndo mwanzo wa kisirani ktka maisha yako huo ni msalaba wako na kila mtu ata ubeba msalaba wake , labda cha kukusaidia muelimishe taratbu ikisindkana fungua biashara aisimamie
 
Mimi nina degree moja ila nimeolewa na mtu ambaye ana elimu ya msingi na hana shughuli yoyoye anayojishughulisha hata nimuelimishe vipi kuhusu biashara au kuhusu kwenda kujiendeleza hataki yeye anachotaka nimhudumie vyoote. Na mtu mwenyewe hata mapenzi hana ila anachotaka ni kuheshimiwa kama anapita Obama. Je? Nimuache au niendelee kumvumilia labda Mungu atambadilisha siku za usoni? Nisaidieni wenzangu

Nimekusoma hivi, wewe ulimpenda kijana kwa kuangalia maisha na uwezo wa wazazi wake hukuangalia yeye anafanya nini kuendeleza maisha yake. Ni jambo la kawaida wasichana wengi hushindwa kutofautisha uwezo wa wazazi wa "boy friend" na uwezo wa kiuchumi wa "boy friend" wakishaolewa ndiposa wanakutana na mama wakwe wale wakorofi kabisa wasiotaka mtu achezee jasho lake......utakumbuka watoto wa maskini uliowapiga chini ukakimbizana na mtoto wa tajiri asiyejua hata elfu kumi inapatikanaje
 
Mie ndio najisemeaga 'mtu anapanda bangi, anataka kuvuna mchicha' How?

Ndio maana yake: Nitambadilisha tu, mwingine alisema, bibi yake alimwambia hadi anioe ndio anafanikiwa.

Mwingine, kasema nikimwacha anajiu
a

hahahahah bibi aliona kuna "kismati" aisee! wengine tunashaurigi mpaka tunaonekana kama ndoa zinatushinda, kumbe wenzao tunakuwa na maamuzi magumu kwa hawa wenzetu, hizi habari za kusubiria kuoteana nani anataka, mbona na ndoa zetu zinasonga mbele tupo mpaka sasa, mmoja aliniambia "akimfanyia/muhoji hivyo mume wake ataulizwa amepatia wapi hicho kiburi na mambo ndio yataharibika kabisa" huyo nilimwambie kaendee kufunga na maombi dada Mungu wetu ni mwema sana sana atakujibu/atambadilisha.
 
hahahahahahahahahaha atabadilika tu, hata Asprin alikuwaga golokipa na nilimvumilia tu mume wangu mpaka alivyopata ya kuwa michuzi wa jf!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom