Nimeolewa ila nimefall kwa jamaa

Nimeolewa ila nimefall kwa jamaa

If you want to ruin your life just go ahead,tou have two kids you have good life there is no way ukajiambia umefall kwa huyo mtu kirusi,kama unataka kwenda just declare to your husband kwamba hukuwahi kumpenda Mumeo,Hakika nakwambia utajiaharibia sana na usifikiri utafanikiwa kufanya siri,itajulikana tuu hata kama sio leo ni kesho,kwanini ukubali mwanaume mwingine alufunue uchi wako???shame on you lady for that fall.piga magoti mwombe Mungu akuondolee hiyo kitu nafsini mwako,huyo ni shetani mkamilifu anakua mshiriki ushetani pamoja.stay away from that kaa mwaminifu kwa mumeo,mshirikishe mumeo tamaa yako ili usumbufu uishe maana maandiko yanasema tamaa ya Mumeo itakua juu yako sasa watch out utaumia sana kwenye ndoa yako na ukishajulikana no body will see what excellent things you have done previous,utadharaulika na zaidi hakuna rafiki atakaye kuungana mkono.Rafiki yako ni Mungu na mumeo na wanao tuu don't be close to that Man.
 
Wakuu nahitaji mawazo yenu kwa kipindi hiki cha majaribu nachopitia.
Mi nimeolewa nna miaka kama 9 kwenye ndoa na kwa kipindi hiki chote nimepitia mazuri na changamoto pia ila sikuwahi kujutia ndoa.Jamaa aliyenioa ni msomi na anajua kuitafuta hela.Kiufupi tuna maisha mazuri nina kila kitu nachokihitaji km nyumba,usafiri wa maana na two beautiful kids.

Ktk kipindi cha ndoa nimepitia changamoto kwa huyu mume wangu.Kiufupi anapenda starehe pombe kwa sana na company za washikaji.Me sio mnywaji wala sitoki kiivo nikitoka job ni home kuangalia watoto na nyumba.Kiufupi ni mke mwema flan!!yes najiamini kwa hilo.Jamaa nishafumania msg za wanawake mara kibao ila naishia kusamehe na sikuwahi kuwaza kulipiza.Huwa nasali sana nikipitia hizi changamoto na Mungu ananivusha salama.

Sasa basi kilichonifanya nilete huu uzi jamvini ni situation niliyonayo now.Kiufupi miezi km 6 iliyopita nimekutana na jamaa ktk kazi flani.Jamaa ana mvuto na alikua ananipa attention flan ivi throughout..Tuliclick haraka sana tukawa close.Ilitokea tu sijui kwa nn..Nilinotice jamaa ananicare vby sana. Mwanzo nilichukulia poa ila siku zilivoendelea kwenda nikaanza kumfeel taratibu.

The eye contact was awkward btn us na imefika mahali najiona nashindwa kuresist.Nikiwa nae under one room nashindwa kabisa napoteza uchangamfu naishiwa pozi kbs.Jamaa anaonyesha interest za wazi ila najikaza knowing kwamba am married ataniona a cheap woman.

Huwa tunaongea mambo mengi na ananieleza issues zake kibao.Kuna siku alinifungukia ila nikavunga nikamwambia its better tuwe mbalimbali coz me ni mke wa mtu na siwezi cheat on my husband.Baada ya hapo akanikaushia km wiki.Aisee nilikonda kwa mawazo.Baadae tukaanza kuwasiliana upya na jamaa anaomba kidate na mm anataka tuspend tym wawili.Kashanialika kwake mara kibao nachomoa.Imefika mahali najiona ntashindwa huko tunakoelekea siko.
Kiufupi kinachonitatiza ni haya yafuatayo:

1.jamaa anajua me ni mke wa mtu so its obvious anataka game tu hakuna mapenzi.

2.Since ni coworker baada ya game ntamwangaliaje ofcn?

3.Naogopa reputation yangu among my workmates wakijua nimetoka na jamaa since wanaume hawana siri.Aisee mi ni mdada nayejiheshimu na wananiona nina bonge la mume.

4.Namfeel mno jamaa na siimagine kupotezea hizi feeling.Ni mtu anayenifanya niwe happy muda wote,confident about myself na I feel lyk a woman again.

Wakuu nisaidieni namna nitakavyohandle hii situation maana naumia kiukweli natamani niuridhishe moyo wangu ila nawaza consequence,kumpotezea jamaa nashindwa naumia at the same time sitaki kuharibu maisha yangu.
Duh... Kam ni kwel ulichokieleza, epuka n ucje thubutu ukaja kukukuta ule msemo unaosema "JIFUNZE KUTOKANA NA MAKOSA" ktk hili swala lako lakin n co mengine... Ni utakuja kujutia mpk unaingia "karibuni" ... Hakika nakwambia, uyo mwana ni tamaa tu uckute,

ila ndo ingekua mm ni uyo jamaa wallaaaah ucngechomoka, ila siri ningekutunzia tu..
 
sifa ya moyo tamaa...moyo kazi yake kutamanii..tamaa ya moyo inaweza kukuweka matatizoni...una mtamani jamaa kazini..nyumbani kuna jamaa ambaye ni mume wako....chunga tamaa mbaya
 
Mpende mmeo, mmeo ni mchangamfu kuliko Hugo jamaa unajielewa acha hizo mambo akikuchunia kuwa karibu zaidi na mmeo utamsahau Hugo jamaa vinginevyo utaharibu penzi kikohozi Dada shauri yako
 
pole sana, kesi yako juu ya matendo ya mumeo sio ya kwanza. Natoa lawama kubwa kwa wanaume wenzangu kwa matendo mabaya tunayowatendea wake zetu. Kuna rafiki zangu wa kike well educated with very high profile jobs lakini wanashida na wanaume zao kama zako kupelekea kuchanganyikiwa na wengine ninavyoongea wameshavunja mahusiano ya ndoa. Wanawake wengi mmekua waadilifu na wengi wanaobadilika tabia katika ndoa husababishwa na waume zao. Waume hasa generation hii, huendeleza tabia zao za kabla ya kuoa ikiwepo kujali zaidi na kuthamini marafiki na kutumia muda mwingi na marafiki kuliko rafiki zao, kurudi nyumbani usiku wa manane kila siku, kutoka out zaidi na marafiki kuliko wake zao. Kunywa pombe kipita kiasi kupelekea low sperm count na kushindwa ku perform home. Kudharau wake na kufanya ngono sana nje na kushindwa kuwaridhisha wake zao. Mbaya zaidi hawatunzi familia kabisa hususani pale wake zao wanapokuwa na kazi za maana huwa ni mzigo mkubwa kwa wanawake. Imefikia mahali mwanamke hasa msomi economically independent anauma kuwa na maisha mapya. Mjini hapo, wale wasioweza kutoka kwenye ndoa wanatunza ndoazao kwakuwa na relathionships nje ya ndoa ambazo huwa zinawariwadha sana na kuwafanya wajione wanawake kama unavyojisikiawewe. Inafika mahali mwanaume hawala ndio anamshughulikia mke wa mtu kwa kila kitu hata kumpeleka kliniki mwanamke anapokuwa mjamzito. Kwakweli, sisi wanaume wa sasa ni shida tumebaki kudai haki zetu na heshima wakati hatutimizi wajibu wetu. Wanaume tunapaswa kuelewa kuwa it is our primary responsibility ku take care of our family for one hundred percent regardless of wife's financial muscles, mwanamke akiwa na mali ni added advantage lakini tunapaswa kumlisha, kumvisha, malazi, matibabu, elimukwa watoto, tujifunze kutokuwa tegemezi au kusaidiwa wajibu wetu na wake zetu.
Sasa wewe dadangu kwa kesi yako sikulaumu kwakuwa mumeo ndiye aliyekusababishia hivyo and believe me mumeo hawizi kubadilika wako wengi wa aina hiyo. Huyo jamaa yako uliyefall ni mtihani sana kwako kwakuwa mnafanyakazi pamoja. Nimeona na nina marafiki wengi wa kike ambao ndo zao hazifai kabisa wanaishi maisha ya kuwa na boyfriends ila hawafanyikazi pamoja. Sikushauri uwe nae huyo jamaa kwakuwa lazima itafahamika tu na utapoteza integrity yako na heshimu ebu jitahidi kujizua ingawa ni ngumu. Pole sana
Nashukuru sana kwa mawazo yako na pia kutonihukumu km wengine.Najua hii sio sawa na wala sitakiwi kufanya moyo unachonisukuma.Ningeamua kufanya ningefanya wala nisingekuja kujianika hapa jamvini.Ila nimejifunza kwamba ujasiri wangu wa kuomba ushauri hapa umenisaidia.Najisikia mwepesi km nimetua mzigo mzito.Na nimepata ujasiri wa kukabiliana na hili.Only because nimeshare.Walionitukana siwalaumu kwani ni mawazo yao pia.
 
Asanteni wote mmekuwa msaada mkubwa sana kwangu.Wanaonijudge wafahamu nimefanya kazi na wanaume kibao ila sijawahi kupitia hii hali nikiwa kwenye ndoa.Kwanza mjue mi nilikuwa nawashangaa mno wanaocheat kwenye ndoa.Nimekuwa muumini mzuri wa kuheshimu mume na kuithamini ndoa.Ugumu ni namna ya kumpotezea jamaa.Ni km kuna kitu nakikosa.Ila now nimekuwa stronger than ever.Thanx to u all
 
Pole sana Joblee, najua haya yanakukuta kwa sababu ya uaminifu wako nakuomba usidiliki kutembea na mtu huyo, fanya yafuatayo
1.Jitahidi usiwe na huyo jamaa sehemu private
2.Mwambie mumeo unavyoikosa kampani yake na unavyojisikia ukiikosa
3.Endelea kumuomba Mungu akusaidie maana unajaribiwa katika hili kwa sababu ndiko ulikokamilika
 
Ama kweli kitabu cha wanawake sisi ni kimoja na changamoto zetu ni zile zile.
 
Kumnyima mwenzio ulichopewa bure na mungu walahi ni dhambi ya mauti!
 
Unaonekana kweli unajiheshimu ila umeanza kuidororesha heshima yako hapa ukumbini kwa kueleza kile ulichodhamiria.
Ulishawahi kujiuliza hivi siku familia yako ukiiparanganyisha itakuwaje? Watoto wako wazuri watakuwaje ktk maisha yao?
Unaonekana unataka kulipiza coz umeshafumania sms kibao ktk simu ya mumeo.
Unahiyari kubomoa au kuendelea kuilinda na kuijenga familia yako kwa mikono yako mwenyewe.
Muonja hasali haonji mara moja, huo utakuwa mwanzo mbaya wa safari ya misukosuko ktk familia yako.
Huyo mwanaume angekuwa kweli anakujali na kukupenda angeiheshimu ndoa yako, huyo anakiu yake ya tamaa ya ngono na akishakugonga utakuwa huna thamani yoyote mbele yake, atakuchukulia kama wale wanaouza mzigo barabarani.
Roho imeniuma sana kwa unachotaka kufanya.
 
Kwahiyo jamaa ndio kashakosa mzigo kisa ni JF daaaah, ingekuwa hakuna mitandao ya kijamii angetunukiwa tayari daaah
 
Back
Top Bottom