Nimeshangazwa na watu wanaokaribia 200.
Jee watu Hawa hawendi misikitini au makanisani?
Jee watu Hawa hawasomi mafundisho ya dini Yao?
Jee watu Hawa wanajua ila tamaa tuu ya maisha?
Jee watu Hawa hawajui na hawataki kujua?
Ni maajabu makubwa sana kwa binaadamu anaefikiria Ana akili timamu kisha kwa akili anayoifikiria akaweza kumshauri mwenye akili Kama zake, au ziko juu kuliko zake au zipo chini kuliko zake.
Hivi binadaamu anafikia kutokwa na tuu na IMAANI kwa binaadamu mwenzake!
Turudi kwa muokotaki
Umeokota peni na peni yenyewe kwa bahati nzuri imeandikwa jina la duka ambayo ndio inapotokea mwanzo.
Kama wewe ni muislam Sheria ya kiislam unapookota kitu unatakiwa ukitangazie kwa muda wa mwaka mmoja ubaki nacho kwa kufikiria huenda mwenyewe akatokea.
Sasa wewe unavyosema umeokota Jana Leo ushavunja na kutaka kujua nini kimo ndani, ukaja jamii forum kutaka ushauri,
Wewe huna akili wewe? Peni imeandikwa kwanini usifikirie ukarejeha kwa wenye duka au Kama unaogopa kurejesha mwenyewe Mbona unngetaka ushauri vipi peni ufike kwa mwenye duka?
Peni ikiwa ya kawaida au ya almasi , chochote unachookota usiingie na tamaa na kutokwa na imani na kukifanya chako. USITUMIE MSEMO WA WASEMAO CHA KUOKOTA SI CHA KUIBA
Usiwe na maamuzi ya haraka kabla ya kufikiria kufanya nini unafanya.
Kwa wachangiaji
Hivi wa TANZANIA wenzangu tunaposema tuna IMANI , Imani yetu ipo kwenye nini haswa?
Yaani fikiria hiyo peni ni yako tena ya "ALMAS" ikisha imekupotea na ni mwanaJF unakuta watu wametoa mchango Kama unavyoona ungejiskiaje?
Kwa hivyo Yale maumivu anayoyapata mwenzako fikiria kuna siku na wewe unaweza kupata Yale Yale .
Tunapochangia tufikirie nini tuna changia , tusiweke tamaa sana kupita kiasi.
Hiyo inawezekana ni kalamu tuu ya kawaida si lolote si chochote ni mtu kaidondosha basi wala hakujali Kama kaiangusha.
Akili sijui zimeruka na Imani zimwpotea kwa ajili ya kutofuata maamrisho ya dini au umaskini umetuzidia hatufikirii chochote.
Kwa kweli nimesoma mengi na kuona kuwa watu roho zao zimebadilika sana na ni mbaya sana.
Hebu turudini kwenye MAFUNZO ya dini kuziweka Imani ZETU sawa