Hujawahi kuingia mikononi mwa polisi wewe. Polisi wengi ni wa HOVYO.
Miaka kama kama 3 iliyopita niliwahi kupigiwa simu na mzee mmoja kutoka kijijini, mzee huyo tunafahamiana. Aliniambia niende kituo cha polisi Chang'ombe kwani kijana wake kakamatwa, polisi ndo waliompigia simu. Nilianza safari ya kuelekea kituoni pale, kufika nikaeleza shida yangu, wakaniuliza jina la kijana, nikataja. Walipekuwa kwenye madaftari yao pasipo kuliona kina lake. Nikajibiwa kubwa huyo mtu hayupo kituoni kwao.
Niliandika na kupelekwa sehemu alikokuwa akiishi, majirani zake wakaniambia kubwa alikamatwa jana yake jioni na polisi. Nikarudi kituoni nikawaeleza kuwa aliletwa hapa kwa kujibu wa majirani zake, askari mmoja wa kike akachukua daftari na kukagua, akikosa jina. Wakti huo kaka yake huyo kijana anayeishi Iringa alifika kuja kufuatilia issue ya mdogo wake, alifika na kuzungumza na askari mmoja kisha akanifuata na kunitaka nimwqzime sh. 50,000/- nikampa, baada ya dk kama 7 hivi akitolewa nje kutoka hapohapo kituoni!. Nilipomuuliza kaka mtu imekuwaje? akasema ametoa sh. Laki 2, ile hamsini nilomkopesha ulikuwa imepungua kwani yeye alikuwa na 150,000/- mfukoni.
Mimi walinikatalia katakata kubwa huyo mtu hayupo na sijuwi walijuaje kuwa sikuwa na mpango wa kuwapa hela.