Nimemwaga kisa VALENTINE day.

Malova

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
784
228
Girl Friend wangu kanimwaga kisa nilichelewa siku ya father Valentine. Nilimpigia saa 3 usiku. Hakupokea baadae siku ya pili akaniambia yeye na mimi basi. Kwasababu sikumpigia simu mchana mzima nikaja kumpigia usiku. Sijielewi, nifanyeje?
 
Tokea lini Mwafrika na mavalentine? Hayo yameanza hivi karne ya 21 kwa huku kwetu na labda anazo sababu nyengine hataki kuzitaja.

Tulia wiki nzima uone atafikia wapi?
 
wewe the whole day ulikuwa wapi? Hata kama ningekuwa mimi ningefikiri, u were busy with another, then usiku huo ulimpigia ili tu ionekane ulimkol on V day!
 
Duh, haya mambo ya kuiga Valentine yanatusababishia matatizo.. Kwa upande wangu tena siku hiyo ndio kabisa hata nilikuwa nataka kumpa zawadi naahirisha kwanza..tusiwe tunafuata mkumbo,,lets make our own life..ambalo litatusababisha tuishi kwa furaha na mafanikio. Siyo kila kinachotangazwa tukifuate..unaweza ukajiandalia Valentine zako mwanyewe siyo hii ya Wazungu...
 
wewe the whole day ulikuwa wapi? Hata kama ningekuwa mimi ningefikiri, u were busy with another, then usiku huo ulimpigia ili tu ionekane ulimkol on V day!
Lakini kama issue ni kupigiwa simu, kwanini yeye asingenipigia mimi kwanza? Ishu nyingine inayoniuma zaidi kwanini akimbilie kusema nilikuwa na mtu mwingine bila kujua kilichonisibu nisimpigie simu?
 
Kumwaga kisa hujampigia simu
What the hell
Kwani si kuna mtu unakuwa busy na kazi hata simu hukumbuki
hakujua majukumu yako mpaka alazimishe umpigie simu
So ukimpigia simu ndo umeonyesha unampenda au vipi
Na usipompigia kutokana na kubanwa na majukumu ina maana humpendi kabisa
Duh kweli Father Valentine ameleta mambo
 
Kuna kuwa mbali na simu kw amuda mrefu kutokana na kubanwa
Kuna kutokuwa na vocha kwenye simu na ikakukuta uko mbali na maduka ya kununua vocha na wewe sio mteja wa mpesa au Zap au tigo pesa
Kuna kuwa kwenye mazingira ambayo simu unaiona kituo cha polisi kutokana na kubanwa

Kuna simu kuishiwa charge na uko mbali na maeneo yenye umeme
Mbona mambo ni mengi tuu yatakayokufanya ushindwe kumpigia mtu simu aise
 
pole sana,mabinti wa kibongo kazi kwao kuiga.Nini maana ya valentine,mbona huko zamani haikuwapo je nyakati hizo watu walikuwa watu walikuwa hawapendani?Achani kuiga.
 
ongea nae vizuri ili uweze kujua chanzo la tatizo haswa ni nini huwezi jua labda kuna tatizo lingine ukiondoa valentine
 
Girl Friend wangu kanimwaga kisa nilichelewa siku ya father Valentine. Nilimpigia saa 3 usiku. Hakupokea baadae siku ya pili akaniambia yeye na mimi basi. Kwasababu sikumpigia simu mchana mzima nikaja kumpigia usiku. Sijielewi, nifanyeje?
Huyo anakutafutia sababu tu hana lolote...kama mapenzi unamuoneshea siku zote haina maana akununie kisa hukumtafuta mapema siku ya valentine..labda kama ana jingine. Na akiendelea kuuchuna ujue kuwa alikuwa kalipanga hilo litokee..wala usiumize kichwa sana akunyimae kunde kakuounguzia mashuziii....
 
Labda amekumwaga kwa sababu hujui kiswahili. Rekebisha title, kumwaga na kumwagwa ni vitu tofauti.
 
Shukuru amekusaidia, kuna siku ungepata tatizo kubwa ye anasubiri umpigie, km ni simu nafikiri ye alitakiwa aanze, si ndo anataka uzungu? Mi huwa nasahau siku ya kuzaliwa na zinakuwa ni lawama za dkk mbili, we anakumwaga na unalalamika? Shukuru kwa Mungu amekuepusha mapema
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom